Diwani Auawa Kikatili; Binti Zake Wabakwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani Auawa Kikatili; Binti Zake Wabakwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Aug 24, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Aug 24, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Diwani Auawa Kikatili; Binti Zake Wabakwa
  Diwani Huyo Alikatwa Mapanga Jumamosi Iliyopita Saa Sita Usiku Nyumbani Kwake.

  Diwani wa CCM Kata ya Bugarama, wilayani Kahama Peter Kisiminza (50) ameuawa kinyama kwa kukatwa mapanga nyumbani kwake katika Kijiji cha Buyange.

  Baada ya kumkata mapanga watu hao waliokuwa wamemvamia usiku wa manane pia walifanya unyama mwingine kwa kuwabaka watoto wake wawili wa kike na kisha kuiba mali na kutoweka.

  Kwa mujibu wa taarifa za awali zilizotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Diwani Athumani, diwani huyo alikatwa mapanga Jumamosi iliyopita saa sita usiku nyumbani kwake.

  Kamanda huyo alisema siku hiyo Bw. Kisiminza akiwa nyumbani kwake usiku amelala alivamiwa na watu watatu waliovunja mlango na kuanza kukata mapanga na kuchukua simu yake ya mkononi. Baada ya kutoka nyumbani kwa diwani huyo walikwenda kuvamia kwa mwananchi mwingine kijijini hapo Buyange, Bw. Mussa Robert ambaye naye walimkata mapanga na kuiba simu tano, baiskeli moja na kifaaa kifaa kimoja cha umeme wa solar vyote vikiwa na thamani ya shilingi 567,000. Baada ya kutoweka, watu wa familia hiyo walipiga yowe kuomba msaada ndipo wasamaria wema walipofika na kumchukua Kisiminza na Robert waliwakimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Segerema mkoani Mwanza kwa matibabu.

  • Kisiminza alifariki saa nane mchana juzi.
  • Robart alipata matibabu na kuruhusiwa siku hiyo hiyo kutokana na kuwa na majeraha madogo.
  Kamanda huyo alisema Jeshi la Polisi linendelea na msako na uchunguzi zaidi kusaka watu waliohusika ambapo limetoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano ili waliohuika wakamatwe.

  Tukio hilo la kuuawa kwa Diwani ni la pili katika kipindi kisichozidi miezi miwili baada ya diwani mwingine wa Lagangabilili, Bariadi, Simba Sita 45 (UDP), kuuawa kwa kupigwa risasi na majambazi.

  Majambazi hao baada ya mauaji, walipora pikipiki aina ya Lifan namba T 693 BCN, fedha taslimu Sh 55,000 na simu ya mkononi aina ya Nokia.

  Katika uvamizi huo, Nyebu Kadundu (60), aliuawa.  Majira | HabariLeo
   
 2. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,814
  Trophy Points: 280
  Unyama huu!
  Poleni sana ndugu jamaa na marafiki.
   
 3. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  RIP Diwani na pole kwa waliobakwa,

  I hope National IDs zinaweza kusaidia kupunguza matukio kama haya! Mtu akifanya ujambazi, basi watu sahihi wanachukua vipimo stahiki na kuanza Investigation.
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hivi kumbe zitakuwa na msaada kiasi hicho..
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,070
  Likes Received: 5,553
  Trophy Points: 280
  poleni wafiwa
  ila kuangalia kwa nyuma kuna giza nene nyuma ya pazia..akuna watu wa dili kama madiwani so yawezekana aliahidiwa mtu tenda akala hela zao mwisho wa siku watu wakageuza matokeo kama ccm muijuavyo hiyo ndio shida hata dar hako kamcehzo kapo sana sana akuna tenda bila 20 percent sema vijijini wamekosa subira wanawahi mapema..huku mtu atampigamikwara ma email kibao mwisho unasikia diwani kakatwa uume
  wamechoka
   
Loading...