Diwani atiwa mbaroni kwa tuhuma za kubaka

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Diwani mteule wa kata ya Kijitonyama kwa Ali Maua, Mhe. Juma Athumani Ulole Ulole anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kutaka kumbaka binti mmoja kwa ahadi ya kumtafutia kazi huko Mashariki ya Kati.
Ulole Ulole ni diwani mteule wa kata hiyo kwa tiketi ya CHADEMA ingawa matokeo ya uchaguzi huo yalibatilishwa na mahakama hivyo kubatilisha ushindi wake.
Kwa mujibu wa binti aliyedaiwa kutaka kubakwa, diwani huyo alimuita katika guest house moja na kufanya jaribio la kufanya nae mapenzi ambapo binti huyo aligoma na baadae kwenda kutoa taaarifa kituo sha polisi.
Chanzo: ITV
Kwa mtazamo wangu, kuna jambo linataka kutendeka hapa, maelezo ya polisi yanadai kuwa, diwani ali-attempt kumuingilia binti kwa nguvu, wakati ibinti mwenyewe anadai kuwa diwani aliomba penzi, na si kulazimisha kama taarifa ya polisi inavyodai. Na kama ni kweli aliyoyasema binti kwenye chombo cha habari, kwanini kesi ya msingi isiwe ni ya kuomba rushwa ya ngono badala ya jaribio la kubaka?
Kuna kila dalili ya huyu binti kutumiwa na watu fulani, hasa aliyekuwa mgombea udiwani wa kata hiyo kwa tiketi ya CCM, Ndugu Said Bulembo aliyeshindwa katika uchaguzi huo licha ya kutumia fedha kuhonga wapiga kura pamoja na chakula. Wasiwasi unakuwa mwingi kutokana na mazingira husika, kuna jaribio la kubaka linalofanyika gesti wajameni?
 
Sasa sisi tufanyeje? mwache a-face mziki wake..vipochi manyoya mnapenda ila consequences zake mnazikimbia.
 
Sehemu ya neno 'atiwa' ulitakiwa uweke 'aswekwa'

haya mambo yapo wanafanya wengi tu, huyu ajali tu kama zingine...waafrika sisi na vinyumba vidogo rasmi na visivyo rasmi! pole wetu
 
Hivi huyu si ndiye aliyekomalia bi mkubwa wa mjengoni afungue njia baada ya kuifunga kinyume cha sheria au nimekosea?
 
Hivi huyu si ndiye aliyekomalia bi mkubwa wa mjengoni afungue njia baada ya kuifunga kinyume cha sheria au nimekosea?
Kama hajakosea popote hana haja ya kuogopa au ku-panic, ila kama anayo ya kwake basi sheria ifate mkondo wake..ndo raha ya utawala wa sheria.
 
Hivi huyu si ndiye aliyekomalia bi mkubwa wa mjengoni afungue njia baada ya kuifunga kinyume cha sheria au nimekosea?

Thats him...
Ndio maana nina wasiwasi kuwa hii kesi ni ya kupikwa.
 
Kama hajakosea popote hana haja ya kuogopa au ku-panic, ila kama anayo ya kwake basi sheria ifate mkondo wake..ndo raha ya utawala wa sheria.

Mashtaka ni ya kubaka, ila jamaa hakubaka, kwa mujibu wa huyo 'aliyebakwa' ila aliombwa utamu ili akatafutiwe kazi Arabuni.
 
Nashukuru kwa masahihisho mkuu.
Sehemu ya neno 'atiwa' ulitakiwa uweke 'aswekwa'

haya mambo yapo wanafanya wengi tu, huyu ajali tu kama zingine...waafrika sisi na vinyumba vidogo rasmi na visivyo rasmi! pole wetu
 
NI HIVI !

Huyu mpiganaji kila kukicha anawanyima wamagamba usingizi!
Kwa muda wa mwaka mmoja tuuu tangu aukamate udiwani huyu kamanda alifanya mambo makubwa ambayo wamagamba hawajawahi kuyafanya ndani ya kata ya kijitomanya tangu tupate uhuru! wamagamba hawajaanza leo kumpiga zegwe mara ohhh anajenga barabara za chini ya kiwanga, ohoo diwani gani anavaa kanda mbili, ohoo hana mvuto, ohoo mabomba yenyewe hata kama yanatoa maji ni ya kichina, mengineyo mengi tuu. Baada ya kumshinda mahakamani kimizengewe tuliwaambia itisheni uchaguzi na sisi tutamsimamisha huyu huyu mvaa ndala na kombati tuone kama 2010 alibahatisha, sasa wanaogopa waanza kumuandalia zengwe ili asishiriki kwenye uchaguzi wa udiwani, ni hivi binafsi nipo tayari kulipa nauli tena ya ndege toka huku nilipo adi kwenye kata yangu ya uchaguzi kwa ajili ya kumchagua mvaa ndala 'kamanda Ulole'
Kwani hao wamagamba akina jarufu, peter,bulembo, azzan,kisusi, chaurembo n.k kwa miaka yote wameleta maendeleo gani ndani ya kata K'nyama zaidi ya kuwamaliza vijana kwa vikete vya 'unga'

Ukweli utajulikana mahakamani baada ya 'mbakwaji' kutoa ushahidi!
 
HIVII KWA AKILI ZA KAWAIDA TUU HUYU DEM ALIENDA GUEST HOUSE KUFANYAJE? KAMA ANAAKILI TIMAMU NAMAANISHA SI CHINI YA 18 YEARS HAKUNA CHA KUBAKWA WALA NINI ALIELEWA GUEST NI KUKUKURUKA TU,!AU NDO ALIDHANI HAPO GUEST NI UGJAIBUNI?
ngurubange tu hilo
 
Binti flora ina maana kazi ya guest house ni
Kwa ajili ya kufanya ****** tuu
 
Siku hizi kesi hizi ni ngumu sana na kama polisi wanaingia kwa gia hiyo wahesabu wameshindwa.
 
Back
Top Bottom