Diwani ashindwa kusoma tarifa ya kata yake kwenye baraza la madiwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani ashindwa kusoma tarifa ya kata yake kwenye baraza la madiwani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WABHEJASANA, Oct 24, 2012.

 1. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Habari wakuu?!
  Jamani kuna hili ambalo limetokea asubuhi ya leo katika wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza ambapo Diwani mmoja wa kata ya Kasenyi wilayani humo ameshindwa kutoa tarifa ya kata yake kutokana na kushindwa kusoma.

  Hali hiyo imemkuta Diwani huyo ajulikanaye kwa jina la Shindano Sanyiwa ambapo baada ya kupewa nafasi ya kusoma taarifa ya kata yake alijikuta akishindwa kutokana na kusoma neno moja moja kama mtoto wa chekechea anayejifunza kusoma na baadaye ndipo analiunganisha na kulitamka.

  Kutokana na hali hiyo ilimlazimu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Methew Lubongeja kumtetea kwa madai kuwa ana matatizo ya macho na kumuomba Diwani wa kata ya Buyagu Leonard Kadinda aliyekuwa jirani naye kumsomea taarifa yake ,lakini hata hivyo kabla ya mwenyekiti huyo kukamilisha maelezo ya kumuomba Diwani huyo kumsomea Sanyiwa alimrushia harakaharaka diwani mwenzake taarifa hiyo na kuketi chini.

  Baadhi ya madiwani walisikika wakiguna huku wakithibitisha kwamba Diwani huyo anao uelewa mdogo sana katika kusoma na kuandika ingawa anakubalika sana katika kata yake na wananchi wake wanampenda.
   
 2. f

  findu fiki JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watavuna walichopanda, kwanini walimchagua diwani siyejua kusoma madhala yake ndio hayo.
   
 3. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ni diwani wa chama gani maana naona kama umezunguka mbuyu.
   
 4. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Ndo zetu,kama Naibu waziri wa elimu anasema Tanzania imeundwa na Tanganyika na visiwa vya Pemba na Zimbabwe mwaka 11964,tutarajie nini kwa diwani wetu?
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Sifa ya mtu kuwania ama kuwa diwani nadhani ni kusoma na kuandika, kwahiyo sioni tatizo sana hapo ikiwa amekidhi vigezo vya kisheria. Suala la kuungaunga maneno wakati anasoma ndio spidi yake na uelewa wake.

  Ndio maana mimi nataka kwenye katiba mpya tuweke kipengele cha mgombea udiwani lazima awe amefika walau kidato cha nne, na mbunge awe na angalau Diploma ili kuisaidia jamii kupata viongozi wenye uelewa mkubwa japo kidogo.
   
 6. s

  swrc JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nadhani atakuwa anatokea magamba
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  kama hajui kusoma wala kuandika basi inamaanisha hata hiyo report hajaiandika yeye...sasa hiyo halmashauri kama inajua madiwani wao hawajui kusoma kwanini wasiwasaidie kwa kuwapeleka shule? maana inaweza ikawa ni mfanyakazi mzuri anachapa kazi safi sema ndio hivo darasani hakupita..elimu haina mwisho wapelekeni viongozi wenu shuleni wakajifunze kusoma kuandika na kufanya mahesabu
   
 8. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Kama alikuwa anawakilisha report ya mapato na matumizi hapo lazima kigugumizi kije na kama ni wa chama cha kijani si anajua report haina ualisia hata kidogo.
   
Loading...