Diwani alia na bei za vifurushi na gharama za uhamishaji miamala

Jul 19, 2020
39
128
Diwani alia na Bei za Vifurushi na Tozo za Miamala

Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolijia ya Habari Inayoongozwa na Waziri Dkt Ndungulile imetakiwa kumsaidia Mhe Rais Magufuli kazi ya kuweka sawa huduma za mitandaoni na miamala hasa gharama za miamala na Vifurushi, Ameitaka wizara kufanya hima na haraka sana kuandaa kanuni mpya za kuzibana kampuni za simu katika maeneo hayo ambayo yamekuwa kikwazo kikubwa kwa wanyonge.

Hayo yamesemwa na Diwani wa kata ya Machame Ndugu Martini Munisi kwenye harambee ya kuzindua ujenzi wa Kanisa la KKKT usharika wa Nguni mtaa wa Marukeni alipoenda kumwakilisha mbunge wa Jimbo la Hai Ndugu Saashisha Mafuwe.

Diwani Munisi ameitaka serikali haswa wizara husika kusikia kilio cha wananchi na kukomesha tozo kubwa zinazofanywa na makampuni ya Simu kutuma na kupokea pesa mfano mtu anatuma pesa elfu thelathini anakatwa shilingi elfu mbili na mia saba karibia asilimia kumi.

Namnukuu "Jambo la kutuma na kupokea pesa siyo anasa, jambo hili linaonyesha wazi wizara husika imekwama kuzibana hizi kampuni za mawasiliano, kutuma pesa na kupokea pesa ni huduma inayotumiwa na wanyonge wengi hivyo wizara ilishughulikie jambo hilo ili jamii iweze kunafaika na huduma hizo na siyo kunyonywa na makampuni hayo"

Ameendelea kusema "Pia huduma ya Internet imekuwa ni ghali sana ukilinganisha na nchi zingine ,Tanzania imekuwa ni ghali zaidi kuliko mataifa mengi ya Africa,Ni vizuri wizara ikafanya kazi kwa maslahi ya wananchi maana huduma za bando zinabadilishwa kila saa na wanatoza ghali sana jambo linalopelekea watu wengi kukwama kwenye baadhi yaa mambo ya msingi na kukwamisha juhudi mbalimbali ikizingatiwa kwa sasa dunia ipo kiganjanjani ,huduma nyingi zinapatikana huko kama Luku,Kulipia bili mbalimbali za serikali na nyinginezo."

Munisi alimaliza kwa kusema "Badala wizara kuja na majibu ya tatizo imekuwa kinyume chake wao wamekuja na namna ya kuhamishiana bando jambo ambalo sio kero kubwa kwa wananchi,Mimi nadhani tupambane na bando kuwa ghali sana,pia bando kuisha bila kuelewa limeishaje."

Source: Zayumba News.

IMG-20210309-WA0023.jpg
IMG-20210309-WA0022.jpg
 
Hili la muamala wa pesa ni wale wabunge wetu wapendwa wa chama chetu pendwa cha ndiooooo kilipitisha iwe hivyo. Sasa nashangaa huyu nae ni mwenzetu halafu ana lalama. Kweli wapinzani walituchelewesha
 
Na mwaka huu kwenye Bunge la bajeti lililo chini ya udhibiti wa chama kimoja kwa zaidi ya 90%, sijui wataongeza tena tozo kwenye nini!! Maana miaka ya nyuma ilikuwa ni kwenye bia, soda na sigara!

Juzi kati hapa wakahamia kwenye miamala ya simu! Miaka yote ubunifu zero! Maliasili zetu kama gesi asilia, nk wanafaidi Wachina, Wazungu na Mamluki wachache! Kazi kweli kweli.
 
Na mwaka huu kwenye Bunge la bajeti lililo chini ya udhibiti wa chama kimoja kwa zaidi ya 90%, sijui wataongeza tena tozo kwenye nini!! Maana miaka ya nyuma ilikuwa ni kwenye bia, soda na sigara!

Juzi kati hapa wakahamia kwenye miamala ya simu! Miaka yote ubunifu zero! Maliasili zetu kama gesi asilia, nk wanafaidi Wachina, Wazungu na Mamluki wachache! Kazi kweli kweli.
Amesahau majuzi tu Mitandao iliangushiwa rungu la faini kama hao Viettel waliambiwa wana mitambo inayohujumu TCRA so ndio kilichokua kikifuatwa wananchi wakamuliwe pesa ilipwe! Mitano tena !
 
Back
Top Bottom