Diwani afariki baada ya kuapishwa ...........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Diwani afariki baada ya kuapishwa


na Francis Godwin, Iringa


amka2.gif
DIWANI wa Kata ya Gangilonga, Abubakar Mtamike, amefariki ghafla siku chache baada ya kuapishwa. Akitoa taarifa ya kifo cha diwani huyo, Mstahiki meya wa Mnaispaa ya Iringa, Aman Mwamwindi, alisema taarifa ya kifo amezipokea jana majira ya saa 12 asubuhi kutoka kwa mke wa marehemu.
Mwamwindi alisema kabla ya kifo chake diwani huyo alikuwa ni miongoni mwa madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ambao walifika kuapishwa juzi pamoja na kushiriki zoezi la kuthibitisha jina lake kama Meya na Naibu Meya, Gervas Ndaki, na baada ya hapo aliondoka kurudi nyumbani kwake eneo la Wilolesi kwa ajili ya kujipumzisha baada ya kuanza kujisikia vibaya.
“Diwani alianza kuumwa siku mbili kabla ya kuapishwa na siku ya kuapishwa mimi nilimtumia usafiri, ili afike kuapishwa na baada ya muda nilimsaidia kurudi nyumbani baada ya hali yake kuonekana ni mbaya toka akiwa katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa....kweli tumepata pigo kubwa sana kwa kifo cha diwani huyo,” alisema Meya Mwamwindi.
Kwa upande wake, Rehema Mtamike ambaye ni mke wa marehemu, alisema mumewe alikuwa akisumbuliwa ugonjwa wa vidonda vya tumbo pamoja na BP ya kupanda na kuwa pamoja na kutibiwa katika hospitali mbalimbali, juzi asubuhi alianguka ghafla na kufariki.
Alisema mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika leo kijijini kwake Mdandu, Wilaya ya Njombe.
Mbunge wa Viti Maalum, Ritta Kabati (CCM), Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa, Gervas Ndaki, pamoja na mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), wameeleza kusikitishwa na kifo hicho na kusema kuwa pengo hilo ni kubwa ndani ya Manispaa ya Iringa.
Wakati huo huo juzi vituo vilitawaliwa na zoezi la madiwani hao kuapishwa baada ya baadhi ya madiwani kushindwa kuapa na mwingine kujaza fomu yake kwa kutazamia kwa diwani mwenzake hadi jina.
 
Pole Tanzania! Unampeleka diwani asiyeweza kujaza fomu kwenda kusimamia watendaji wasomi wilayani?
 
Pole Tanzania! Unampeleka diwani asiyeweza kujaza fomu kwenda kusimamia watendaji wasomi wilayani?
Wengi wetu tulichagua kwa USHABIKI NA SI UBORA!

Poleni watu wa Iringa kwa kifo cha diwani. Mola amsamehe na amlipe yaliyo mema.
 
Tangulia diwani wangu MBELE YAKO NDO NYUMA YETU....uangaziwe mwanga wa milele wewe diwani na upumzike kwa amani
 
Back
Top Bottom