Diwani afariki baada ya kuapishwa ........... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani afariki baada ya kuapishwa ...........

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 19, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,984
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Diwani afariki baada ya kuapishwa


  na Francis Godwin, Iringa


  [​IMG] DIWANI wa Kata ya Gangilonga, Abubakar Mtamike, amefariki ghafla siku chache baada ya kuapishwa. Akitoa taarifa ya kifo cha diwani huyo, Mstahiki meya wa Mnaispaa ya Iringa, Aman Mwamwindi, alisema taarifa ya kifo amezipokea jana majira ya saa 12 asubuhi kutoka kwa mke wa marehemu.
  Mwamwindi alisema kabla ya kifo chake diwani huyo alikuwa ni miongoni mwa madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ambao walifika kuapishwa juzi pamoja na kushiriki zoezi la kuthibitisha jina lake kama Meya na Naibu Meya, Gervas Ndaki, na baada ya hapo aliondoka kurudi nyumbani kwake eneo la Wilolesi kwa ajili ya kujipumzisha baada ya kuanza kujisikia vibaya.
  “Diwani alianza kuumwa siku mbili kabla ya kuapishwa na siku ya kuapishwa mimi nilimtumia usafiri, ili afike kuapishwa na baada ya muda nilimsaidia kurudi nyumbani baada ya hali yake kuonekana ni mbaya toka akiwa katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa....kweli tumepata pigo kubwa sana kwa kifo cha diwani huyo,” alisema Meya Mwamwindi.
  Kwa upande wake, Rehema Mtamike ambaye ni mke wa marehemu, alisema mumewe alikuwa akisumbuliwa ugonjwa wa vidonda vya tumbo pamoja na BP ya kupanda na kuwa pamoja na kutibiwa katika hospitali mbalimbali, juzi asubuhi alianguka ghafla na kufariki.
  Alisema mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika leo kijijini kwake Mdandu, Wilaya ya Njombe.
  Mbunge wa Viti Maalum, Ritta Kabati (CCM), Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa, Gervas Ndaki, pamoja na mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), wameeleza kusikitishwa na kifo hicho na kusema kuwa pengo hilo ni kubwa ndani ya Manispaa ya Iringa.
  Wakati huo huo juzi vituo vilitawaliwa na zoezi la madiwani hao kuapishwa baada ya baadhi ya madiwani kushindwa kuapa na mwingine kujaza fomu yake kwa kutazamia kwa diwani mwenzake hadi jina.
   
 2. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2010
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Pole Tanzania! Unampeleka diwani asiyeweza kujaza fomu kwenda kusimamia watendaji wasomi wilayani?
   
 3. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Wengi wetu tulichagua kwa USHABIKI NA SI UBORA!

  Poleni watu wa Iringa kwa kifo cha diwani. Mola amsamehe na amlipe yaliyo mema.
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  R.i.p.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Apumzike mahala pema peponi!
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Tangulia diwani wangu MBELE YAKO NDO NYUMA YETU....uangaziwe mwanga wa milele wewe diwani na upumzike kwa amani
   
Loading...