Diwani abbasi tarimba,dc wa kinondoni mr jordan rugimbana na ufisadi wa million 350 loh nchi hii?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani abbasi tarimba,dc wa kinondoni mr jordan rugimbana na ufisadi wa million 350 loh nchi hii??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Oct 30, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,442
  Likes Received: 5,695
  Trophy Points: 280
  Wakati Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Yusuf Mwenda, akiwa tayari amemuagiza Mkaguzi wa Ndani kuchunguza mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Hananasif, tayari suala hilo limefikishwa katika kamati ya Bunge.
  Suala hilo linaelezwa kufikishwa katika kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa inayoongozwa na Mbunge wa Vunjo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Augustine Mrema.
  Kamati hiyo inatarajia kuutembelea mradi huo Novemba 3, mwaka huu baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan, anayeelezwa kutoridhishwa na hatua za Meya Mwenda.
  Taarifa zinasema hatua hiyo inalenga kuendeleza kile ambacho baadhi ya wananchi wamekuwa wakidai uhasama wa kisiasa uliotokana na kura za maoni baina ya Diwani wa Kata ya Hananasif, Abbas Gullam Tarimba na Mbunge Azzan.
  Habari zinasema kuwa pamoja na Diwani Tarimba kushiriki katika hatua za awali za kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa jengo hilo, kulifanyika mabadiliko mengine ya gharama za mradi huo wa jengo la ghorofa moja na madarasa 16.
  Awali gharama za mradi huo kulingana na mkataba wenye kumbukumbu namba HMK/KH/VOL1/0005/001 uliosainiwa Februari 7, mwaka 2007, na Diwani Tarimba zilikuwa Sh milioni 539.8.
  Mradi huo uliokuwa ukitekelezwa na kampuni ya Trace Building Services Limited, chini ya Mohammed Rwiza aliyetajwa kama Mkurugenzi Mtendaji, unaelezwa kubadilishwa gharama kutoka Sh milioni 539.8 hadi kufikia Sh milioni 817.6.
  Diwani wa Kata hiyo, Abbas Tarimba, alipotafutwa ili kulizungumzia suala hilo na hasa baada ya kuwapo kwa taarifa kuhusu ujio wa kamati hiyo hakupatikana baada ya kuelezwa kuwa alikuwa safarini nje ya nchi kikazi.
  Mbunge Azzan alipoulizwa kuhusu suala hilo , hakutaka kusema lolote kwa madai kuwa yeye ni sehemu ya kamati hiyo, hivyo kuongelea jambo hilo ni kuingilia uhuru wa kamati.
  Hata hivyo, alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo, Meya Mwenda alikiri kupokea taarifa kuhusu ujio wa kamati hiyo, japokuwa alisema ni ziara ya kawaida inayotokana na hoja zilizomo katika taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).
  Alisema ikiwa wajumbe wa kamati hiyo, watahitaji kujua suala la mradi wa shule hiyo ya Hananasif, watapewa maelezo kwa vile tayari taarifa ya mkaguzi wa ndani itakuwa imekamilika.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni (DC) Jordan Rugimbana, aliwataka wanasiasa wilayani humo kuacha tabia ya kushambuliana katika mambo yasiyo ya msingi, badala ya kusimamia maendeleo.
  “Kwa vile Meya aliagiza uchunguzi, sioni kama kulikuwa na sababu suala hili kufikishwa katika kamati ya Mheshimiwa Mrema, lakini hiyo yote ni dalili za kutaka kuonyeshana ubabe,” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
  Hata hivyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge Augostine Lyatonga Mrema, alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu ziara hiyo, alisema ni ya kawaida na haina mahusiano na migongano ndani ya CCM.
  Mrema pia aliwataka wajumbe wa kamati hiyo kujikita katika hoja zinazojenga maendeleo ya wananchi, badala ya kubeba mambo binafsi yanayohusu tofauti za wanasiasa, kwani kwa kufanya hivyo dhama yao katika kamati hiyo itapotea.
  Mrema aliongeza kwamba kamati yake haiendi Kinondoni kwa ajili ya mradi wa Hananasif, badala yake akasema kuna hoja za muhimu zilizo katika taarifa ya CAG zilizotokana na ukaguzi ambazo zinapaswa kutolewa ufafanuzi.
  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
Loading...