Divided Perspective; Laana na Mashangilio

Jamani ni kweli wapinzani walekeze nguvu za kuwaelimisha watu wengi vijijini lakini hata sisi pia wenye ndugu vijijini tutumie fursa hiyo kuwaelimisha ndugu zetu kuhusiana na UFISADI unaofanywa na hawa MAJAMBAZI wa CCM. Watu vijini wanafanywa kama Mazuzu yaani aibu sana.
 
Nimefanya Kazi Vijiji Vingi Vya Nchi Yetu, Pasaka Nilikuwa Maruku Bukoba, Karamagi Alipata Wakati Mgumu Kuhutubia Mkutano Kwenye Shule Moja Ya Sekondari Ambayo Imeitwa Jina Lake, Wananchi Wanataka Jina Lake Liondolowe, Hakupata Mapokezi Ya Mafuriko Kama Ya Chenge Na Lowa-hasa, Ni Kweli Kuwa Wanachi Wengi Wanajua Kuwa Shida Kubwa Walizo Nazo Zimetokana Na Ufisadi, Hasa Bill Za Juu Za Umemme, Bei Ya Dizeli Na Kupanda Kwa Bei Za Vyakula, Sasa Hivi Nipo Vijiji Vya Lusewa Mkoani Ruvuma, Hawajui Mengi Kuhusu Ufsadi Ila Walisikia Kujiuzulu Kwa Mawaziri Kutokana Na Richmond, Magazeti Hapa Yanafika Labda Siku Walimu Wakienda Songea Kupokea Mshahara, Ila Ukweli Ni Kuwa Wamepoteza Imani Na Jk, Utawaona Vikundi Vikundi Wakizingira Mtu Mmjoa Mwenye Radio Katikakti Wakisikiliza, Wiki Ijayo Nitakuwa Shinyanga Huenda Nitapata From Horse Mounth Kulikoni Chenge Kupata Mapokezi Hayo, Jambo Moja Nidhahiri, Ukiangalia Kwa Makini Ile Picha Ukiacha Viongozi Wa Chama Ccm Amboa Nisehemu Ya Ufisadi, Wengine Ni Vijana Waliochoka Na Maisha Kula Kwao Taabu!!! Hivyo Siku Hiyo Kula Kwao Kulikuwa Kwa Chenge
 
watoto wa mjini wanasema "habari ndio hiyo",je kijijini wanasemaje......"kazi ipo" hii ni ya tmk wanaume.... chenge vs lowassa wamekubalika kwa wezi wao katika vijiji vyao... sasa kazi iko jijini dar 'rais mkapa" kazomewa live,je hao mafisadi watapita karikao au manzese...sijui itakuwaje...watauwawa maana wananchi wanataka kujua pesa zao zilipoenda na kwanini hawajue nini tunataka hilo....ccm ni vichaa sana,tena rais anakazi ya kutuambia mafisadi wote wataenda rumande lini,yeye rais azunguke mikoani,ulaya,america na asia,atowe mawazo yake na kujiuliza lakini ajue tunataka mafisadi wote waingie rumande kabla ya mwenzi wa 7,kwani ndani ya bunge ajue ccm wenye uzalendo na nchi yao watalipuka kama tsunami,tena itamualibia hata yeye rais....
 
Nafikiri haya maswala yanahitaji strategy waliwengi tunatokea vijijini, watu kama elfu tatu kila mtu mwenye mtu kijijini ukiwa unamwandikia barua ndugu ndugu yako, mjomba wako, shangazi yako msikose kuweka mstali mmoja, miwili ya kuelezea hali halisi inayokabili nchi yetu, jinsi Viongozi wachache walivyoujichukulia pesa za nchi yetu(EPA, Richmond, vijisenti vya IPTL nk) na kuwa zao.

Tuwakaririshe(kama wimbo vile) jamaa zetu kuanzia vijijini na miji yote kwa ujumbe mfupi kama mwalimu alivyotukaririsha nyimbo mbali mbali wakati wa kumtoa idi Amin DADA.

Namna hiyo tutapandikiza mbegu itakayoweza kuwaondoa mafisadi haraka sana. naomba kila mwenye influence yoyote katika jamii aliyopo asiwe anamalizia bila kuongelea UFISADI na jinsi wanavyotumia pesa kuwalagai watanzania wakati watanzania wakiendelea kuwa masikini.

Wito wangu huu siyo ubaguzi na nisingependa tumbague mtanzania yeyote lakini MAFISADI ni hatari sana naomba na nitaendelea kuomba tuwabague na tuwatenge katika jamii zetu.

Tuwatenge kuanzia ktk vyama vya kijamii, ktk makanisa, katika misikiti na kila aina ya function kama inavyowezekana. Hii ni kwa sababu wameonyesha kutokuwa na huruma kwetu watanzania na jamii zetu kwa ujumla.
 
Kakindo,

I am curious to know what Opposition will do from now going forwards. How can we reach the minds of Watanzania waachane na woga, waanze kufikiria na kujijenga kama watu huru wenye kuamua mambo wenyewe bila kushurtishwa, uhuru wa kujituma na kuona maendeleo yao bila kuvunja sheria, kutambua kuwa Katiba iko kwa ajili yao na si dhidi yao na la mwisho kabisa ni kuwa kutokukubaliana na CCM ni jamboa la kawaida na si dhambi kuu ya kugongwa mhuri wa milele kuwa "Msaliti"!
 
Look how happy they are...like ngabu says..ndivyo...


shujaa.jpg

Lak hapa tukiangalia vizuri ni kwamba Wana CCM ndiyo walikuwa na shauku ya kumpokea chenge. Watu wengine unaona walikuja kuangalia magari. unaona hata bahadhi hawana habari na vijisenti
 
Nimeongea na nyumbani Tanzania leo, na nimeambiwa ni jinsi gani watu wananunuliwa kwa Khanga, Tisheti, Pilau, kofia na chupa ya Wanzuki. Huu msafara wa bariadi, kila mtu alinunuliwa kuanzia Mzee Kundya mpaka yule mkulima.

How do we connect these fellow citizens back to reality?

How does opposition reach out and tell Mtanzania kuwa ana nguvu za kufanya maamuzi ya haki bila kushurtishwa na kutishwa?
 
Rev. Kishoka,
Nimesema dawa ninayo na sintapenda kuiweka hapa hadharani kwa sababu CCM tutakuwa tunawaanda viongozi kama hawa kujiwekea kinga.. Ila naweza kukupa Hint moja..
TANU waliweza vipi ku capture mioyo ya Wadanganyika hawa hawa waliokuwa wakiandamana kuwapongeza watawala wetu Waingereza?...
Ni mbinu gani ilitumika kwa wananachi kuanza kufikiria Uhuru wao wa kweli wakati mzungu alikuwa akiabudiwa kuwa mbora kuliko viumbe wote?..Let's go back to the basic bob tutashinda tu...
 
Back
Top Bottom