Asha Abdala
JF-Expert Member
- Mar 21, 2007
- 1,130
- 44
Ditopile- The saint or a sinner?
Unajua hapa watu wengi wamekataa tusimjadili Ditopile eti kwa kuwa tayari ameshakufa. Lakini watu hao hao wanaokataza Ditopile asijadiliwe, wanamjadili Hayati Mwalimu Nyerere kwa undani wote kama vile si marehemu. Sasa nashauri Hayati Ditopile naye ajadiliwe- Is he the saint or the sinner? Tuanzie na makala ya Karugendo
Dito nilimpenda, nikamchukia, nikampenda baada ya kufa
Niungame wazi kwamba sikubahatika kukutana na marehemu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri wakati wa maisha yake.
Nilimfahamu kupitia kwenye vyombo vya habari.Zamani nikiwa shuleni, nilikuwa nikivutiwa na jina lake refu: Ukiwaona (Usiwaulize) Ramadhani Mwishehe Ditopile wa Mzuzuri.
Nilihisi hakuwa mtu wa kawaida, maana wanafunzi niliosoma nao, waliokuwa na majina marefu na ambayo hayakuwa ya kawaida, walikuwa ni watu wa aina nyingine.Wenye akili sana, wenye uvumbuzi na vipaji vingine kama ucheshi, kupatana na kila mtu nakadhalika.
Hivyo nilihisi kuwa Ditopile, ni mtu wa aina hiyo. Pamoja na kuvutiwa na jina lake, haikutosha kumpenda! Nilimpenda Ditopile wakati serikali ya awamu ya nne ilipoingia madarakani. Kuna mtu mwenye heshima zake alininongoneza kwamba ndani ya serikali ya awamu ya nne, mtu pekee mwenye ubavu wa kuwashambulia na kuwakemea mafisadi wazi wazi bila kificho na woga ni Ditopile.
Hakujali cheo cha mtu, kama mtu ni fisadi, alimwambia waziwazi. Na kwamba mtu huyu, yaani Ditopile, si fisadi!
Ni kati ya watoto wa Mwalimu Nyerere waliobaki waaminifu kwa mawazo ya Mwalimu na wazalendo wa nchi hii.
Kwamba Ditopile hakujilimbikizia mali. Na kwamba kule kupangiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, zilikuwa njama za mafisadi kuhakikisha anakaa mbali na Rais Jakaya Kikwete, ili asiweze kumpatia habari za haraka za wanaoiba fedha za Serikali.
Sifa hizi zilinifanya nimpende Ditopile. Kama sote tunavyojua mafisadi wengi wamefichua makucha yao wakati wa Serikali ya awamu ya nne.
Na mbaya zaidi wengi wao walikuwa wamemzunguka na kumpamba Rais Jakaya Kikwete, kwa kisingizio cha Wanamtandao hivyo mtu wa kuwakemea na kuwakumbusha wajibu wao kwa Watanzania ni mtu wa kupendwa kwa namna yoyote ile.
Hivyo nilimpenda sana Ditopile baada ya kufahamu msimamo wake na mapenzi yake kwa taifa letu.Nimeandika makala hii yenye kichwa cha habari nilimpenda Dito, nikamchukia na kumpenda tena baada ya kufa kwa sababu ya kutokuwa fisadi, kuwa tayari kuwashambuliwa mafisadi, ile ya kuwa mzalendo na kuzipenda kupindukia fikra za Mwalimu, haijaandikwa!
Yanatajwa mengine mengi, lakini hili linafunikwa, labda ni kwa vile tumejenga utamaduni wa kuupenda ufisadi na kuwasifia mafisadi wenye vijisenti vyao kwamba wao ndio wanaume, wao ndio waliofanikiwa kimaishani, wao ndio wenye akili.
Kuna watu waliosikitika kwamba Dito, amekufa maskini! Maana yake alikuwa mjinga, kuacha kutumia nafasi ya uongozi wake serikalini kuiba! Hata watu waliomfahamu zaidi, wale waliokuwa na bahati ya kukutana naye, hawakuiandika sifa hii ya kutokuwa fisadi, sifa hii ya kuwashambulia na kuwakemea mafisadi.
Nimeliona pengo hili na kwa vile ninakiamini kwa asilimia mia moja chanzo cha habari hii, nimeona ni bora nizibe pengo. Tutakuwa hatumtendei haki Dito tusipotaja sifa yake ya kufa bila vijisenti! Lakini labda nielezee ni kwa nini nilimchukia mzalendo huyu. Nilimchukia sana pale aliposababisha kifo cha kijana Hassan Mbonde, dreva wa daladala.
Nilishangaa sana mtu anayechukia mafisadi, mtu anayependa fikra za Mwalimu Nyerere, mwenye kutetea haki za wanyonge, anaweza vipi kufanya kitendo kama hicho. Kukatisha maisha ya kijana mdogo (33), kijana aliyekuwa na matumaini ya kuishi, kijana mwenye familia na watoto wa kulea?
Nilimchukia kupindukia! Nikachukia zaidi pale kesi yake ilipobadilishwa na kufanywa ionekane ni kuua bila kukusudia. Nikachukia zaidi na zaidi pale alipotolewa rumande wakati watu wengine wenye kesi kama hizo wanasota miaka, kabla ya kesi zao kusikilizwa.
Niliona hakuna haki katika nchi hii, niliona ni mtindo wa kulindana! Kuna jamaa yangu anayeishi Zanzibar alinitumia SMS ya kifo cha Dito, nikamjibu ngoja atangulie, akakutane na kijana aliyekatisha maisha yake, maana kule hakuna cheo wala kujuana, akanijibu Acha roho mbaya.
Kusema kweli, nilimchukia sana Dito kwa kitendo kile na jinsi alivyoshughulikiwa baada ya kitendo hicho.
Nikampenda tena Dito baada ya kifo chake. Kwa nini? Tanzia ya kwanza niliyoisoma juu ya Dito ni ile iliyoandikwa na Happiness Kabatazi, 'Tanzania Daima', Jumanne, Aprili 22.
Binti huyu ninamheshimu sana anavyoandika. Huyu ni mpambanaji, mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu. Nikashangaa sana, alivyoandika Namlilia Ditopile. Nikashangaa alivyompamba, pamoja na kufahamu kitendo cha kukatisha maisha ya kijana Hassan Mbonde dereva wa daladala.
Nikakwazika kwa mwanaharakati wa haki za binadamu kumlilia muuaji. Tanzia ya pili niliyoisoma ni ile ya Aristariko Konga. Huyu naye ni mpambanaji mwingine, naye kwenye 'Raia Mwema' ya Aprili 23 aliandika hivi: Ditopile Mzuzuri alikuwa kama muarobaini wa mazingira ya hasira, chuki, visasi na simanzi.
Nikaendelea kushangaa zaidi muarobaini wa mazingira ya hasira, chuki, visasi na simanzi, gari lake ligongwe, atoe bastola? Tanzia ya tatu ni ile ya Maggid Mjengwa, kwenye 'Raia Mwema' ya Aprili 23, huyu naye ni mwanaharakati wa kutupwa, ila naye anamlilia Dito kwa aina yake.
Tanzia ya nne ni ile ya Jabir Idrisa katika 'MwanaHALISI' ya Jumatano Aprili 23, huyu pamoja na kumlilia Dito, anatoa ushuhuda wa watu wengine waliomfahamu Ditopile kama vile Price Bagenda aliyemkariri akisema: Mchumi huyu ni mtu wa mizaha sana; sikumuona kujenga chuki na mtu hata siku moja.
Ikitokea amekukasirisha atatafuta kila njia mpatane haraka iwezekanavyo. Kila tulipokutana alizungumza mambo makubwa ya nchi, hali ya siasa na mwelekeo wa taifaalionyesha moyo huu tangu akiwa kijana wa TANU na CCM. Na hii ya Bagenda ikavuruga mawazo yangu, inawezekana vipi mtu asiyejua kujenga chuki na mtu, gari lake ligongwe atoe bastola?
Tanzia hizi kutoka kwa watu ninaowaheshimu na kuwaamini, zilinichanganya mawazo. Kwa vile msiba huu umetokea nikiwa Dar, niliamua kujitupa mitaani na kusaka habari zaidi juu ya Dito.Inashangaza sana!
Kumbe Dito hakuwa mgovi, hakuwa na majivuno wala dharau kwa watu wa kawaida. Watu wengi nilioongea nao, wanasema walishtushwa sana na tukio la Dito, kumfyatulia risasi yule kijana Hassan Mbonde, dereva wa Daladala.
Hawakumbuki kumwona Dito akiwa na hasira kiasi hicho katika maisha yake. Wengi wanaamini alirogwa na mafisadi!
Alitupiwa juju, akili yake ikabadilika! Wenye imani hizi za kurogwa wanalishikia hili bango na wanamtaja kabisa mlengwa! Maana, kuna habari za mitaani kwamba Dito, alipowekwa gerezani, kuna mafisadi walifanya sherehe. Na walikuwa wakifanya kila njama ili aendelee kubaki ndani.
Nimeelezwa mengi juu ya Dito hadi hasira yangu ikayeyuka. Kumbe huyu ni kati ya watu wachache hapa Tanzania waliotumia muda wao wote, nguvu zao na akili zao kulitumika taifa letu? Ni kati viongozi ambao hawakujilimbikizia mali? Ni kati ya viongozi ambao hawakuficha fedha nchi za nje.
Huwezi kuwa una fedha nchi za nje ukahangaika maporini kufanya biashara ya Asali. Ditopile amekufa akiwa anafanya biashara ya Asali.Wengi tulifikiri alifanya kitendo kile cha kumfyatulia Hassan Mbonde risasi kwa kiburi cha kuwa karibu na Rais Jakaya Kikwete na kwamba labda hakujuta kwa kitendo hicho.
Lakini ukweli nilioupata kwa watu waliokaribu naye ni kwamba kitendo hicho kilimtesa sana na hakukikubali wala kukipokea rohoni mwake hadi siku ya kufa kwake.Hakuamini kama yeye ndiye aliyetenda kitendo hicho.
Ilimtesa sana! Ule mtindo wa kuvaa kofia aina ya pama mahakamani zilikuwa ni mbinu za kutokubali kitendo kile. Amekufa akiwa na maneno Hujafa, hujaumbika midomoni mwake.
Mungu amlaze mahali pema peponi, kwa vile yeye ndiye mwenye kupima, tumwachie yote! Ipo siku atawafichua wabaya wa Marehemu Ukiwaona (Usiwaulize) Ramadhani Mwishehe Ditopile wa Mzuzuri.