Ditopile atua Ngorongoro kuiombea CCM kura na kueleza makubwa anafanya Rais Samia

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
870
948
Mbunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amewaomba wananchi wa Ngorongoro kumchagua Shangai awe Mbunge wa Jimbo hilo ili aweze kushirikiana na Serikali kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kuendeleza miradi ya maendeleo iliyokua inatekelezwa na aliyekua Mbunge wa Jimbo hilo William Ole Nasha.

Ameyasema hayo Jana alipofika Jimboni humo kushiriki kampeni za Uchaguzi mdogo katika Jimbo la Ngorongoro na Kumnadi Mgombea wa CCM Ndugu Emmanuel Shangai.

"Serikali ya Rais Samia imefanya kazi kubwa ya kutekeleza miradi ya maendeleo na mimi kama Mbunge mwanamke nitashiriki kikamilifu kuwaeleza wananchi makubwa yaliyofanywa hapa Ngorongoro ili mtupe Shangai akaendelee kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili,"

"Ndani ya Kipindi Kifupi Rais Samia Suluhu Hassan amewaletea Fedha hapa Ngorongoro zaidi ya Milioni 800 kwa ajili ya Ujenzi wa Vyumba vya madarasa 40,kwa mara ya kwanza hamtachangishwa fedha za ujenzi wa madarasa ya Sekondari. Tuleteeni Emmanuel Shangai ashirikiane na Rais Samia kuwaletea Maendeleo"

"Rais Samia pia hajaishia hapo tunajua huku ni Wafugaji na kuna Vijiji vipo mbali, Rais Samia amewaletea Fedha zaidi ya Milioni 560 kwa ajili ya ujenzi wa Shule Shikizi 29 hapa Ngorongoro. Rais Samia anayo nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo wana Ngorongoro"

"Hapa Ngorongoro Wakati wa Msimu wa mvua takribani 60% ya barabara kuu ya wilaya na barabara zinazounganisha vijiji na vijiji zinapitika kwa tabu, Rais Samia amesikia kilio Chenu amewaletea Fedha Bilioni 1.5 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Barabara na Madaraja, haya atayasimamia vyema Shangai mkipa kura za kutosha"

Uchaguzi wa Marudio Jimbo la Ngorongoro unafanyika Disemba 11, 2021 kufatia Kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo William Ole Nasha.
 
Wamefanikiwa sana kwenye Tozo! Vyitu kupanda bei,na kusafiri sana, hilo wamelitelekeza kwa vitendo! Hakika wapinzani walituchelewesha sana
Pendo una ID mbili, na ile ya UGANDA maana heding kwa UGANDA ni replica ya hii

 
Pendo una ID mbili, na ile ya UGANDA maana heding kwa UGANDA ni replica ya hii

Ni yeye
 
Back
Top Bottom