DIT inaongoza kwa kufelisha wanafunzi? Tatizo ni nini hasa? Nini kifanyike?

Jamani hatutaki wahandisi Feki, tumechoka na majanga ya kila siku yanayosababishwa na wahandiki wasiomudu fani zao. Hii sio fani ya kubahatisha. Hata ikitokea darasa zima wamefeli, basi isitokee standadaizesheni ili chuo kisionekane hakifelishi. Kufeli ni kufeli, afeli mmoja, wengi au wote, kote ni kufali, kwa maana ya wanafunzi wameshindwa kumeet minimum qualification kuwawezesha kuendelea au kupata vyetu nukta
 
Na huo ubia na wachina nao ndio unazidi kushusha hadhi ya taaluma hapo DIT, pamoja na kuteua wakuu wa idara kwa kuangalia nani ni "yes sir". Utashangaa mkuu wa idara hana quality yoyote ya kumfanya awe na nafasi hiyo lakini ndiye mkuu wa idara.

Kwa ujumla Kondoro amefikia mwisho wa upeo wake wa uongozi, hadi hapo atakapostafu au kuondolewa hapo dit, vinginevyo tutarajie ubora wa elimu kuzidi kudorora.
Nadhani mkuu mpaka dakika hii atakuwa ameupata huu ujumbe!
 
Jamani hatutaki wahandisi Feki, tumechoka na majanga ya kila siku yanayosababishwa na wahandiki wasiomudu fani zao. Hii sio fani ya kubahatisha. Hata ikitokea darasa zima wamefeli, basi isitokee standadaizesheni ili chuo kisionekane hakifelishi. Kufeli ni kufeli, afeli mmoja, wengi au wote, kote ni kufali, kwa maana ya wanafunzi wameshindwa kumeet minimum qualification kuwawezesha kuendelea au kupata vyetu nukta
Hapa, hatuangalii mambo kwa upande mmoja wa shillingi! Kufeli tunajua kupo! Ila inawezekana vipi darasa lenye wanafunzi 46 wakafeli wanafunzi 26? Nusu ya darasa wamefeli! Inamaana hao wanafunzi walipataje nafasi ya kusoma hapo kama uwezo wao ni mdogo? Tatizo ni nini hasa? Ndiyo maana tunajadili!
 
mie ni engineer wa dit BENG telecom,kuna kamwalimu kanaitwa ngomuo ndo tatizo kubwa la dit,anataka kuonekana yeye ndo anajua kila ki2..
 
Sababu ya kufeli mie kusema ukweli siwezi kuijua. Mitihani sijaiona, wala wanafunzi sijaongea nao.

Ila ninachoweza kuongeza kwenye hii mada ni kushare na nyiniyi experience kutoka kwa ndugu wangu anayesoma huko. Yeye ansoma I.T. Kwahiyo fikiria masomo ya programming , networking etc... Sasa alinidokeza mwezi wa Saba kwamba kule chuoni hawana internet mwezi wa nne sasa. ! Nikammuliza sasa hizo assignment mnafanya research kivipi akaniambia kupitia material ya waliopita.

Sasa likaja swali la programming. Wao wanaruhusiwa kutumia computer (kumbuka hazina internet) masaa machache kwa wiki tuu- siku nyingine hawawezi kwasababu wanafunzi wamejaa. Programming wanakaa darasani wanamsikiliza mwalimu anavyoandika ubaoni !.... Nikasema Mungu wangu unajifunza programming kwa kutumia ubao , akasema ukitaka msaada kutoka kwa wanafunzi wanaoelewa (akili zinazo chaji) wanakuambia leta hela kwanza ndio nitakuelekeza.

Sijasema hili ndilo tatizo ... kuna idara nyingine pia engineering n.k...nao wamefeli. Lakini ni mchango wangu labda utasaidia kupanua mawazo kidogo

B.P (2010)

mwambie aje informatics-udom hapa tjila ki2 kipo bt ajipange coz rate ya kudisco inakimbizana na dit.
 
Back
Top Bottom