Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Mnyonge hasa ni nani Tanzania, ni kipi anachostahili, nani afanye nini na ni yapi madhara ya kutumia dhana hiyo isivyostahili.
1. Mnyonge ni mtu asiyeweza kujipigania yeye mwenyewe ili kuweza kujipatia mahitaji yake ya msingi.
Kwa mantiki hiyo, ni kweli tuna wanyonge nchini ambao ni 'walemavu' na 'watoto yatima'.
2. Tunashauri serikali ifikirie uwezekano wa kuanzisha mfuko maalum wa kuwasaidia wanyonge ambapo watakuwa na vituo maalum kila wilaya na wataendelezwa kupitia mfuko huu.
Hii ni kwa sababu makundi haya hayawezi kujihudumia yenyewe, hayajapenda kuwa hivyo na yana haki yakuishi maisha ya kibinadamu kama watu wengine, hivyo chini ya kanuni ya 'distributive justice' serikali ina wajibu wa kusaidia makundi haya.
Huwa inasikitisha sana kuona watu hawa wanatelekezwa wanaishi kwa kuomba omba.
Inatakiwa sehemu ya kodi inayokusanywa kutoka kwa wale wenye uwezo wa kuzalisha, itumike kusaidia wanyonge hawa.
Jambo hili sio geni, ndio maana wanunuaji wa umeme kwa mfano, wanakatwa makato flani kwa ajili ya kusaidia wasio na umeme vijijini wapate umeme chini ya mpango wa REA. Hiyo mpango kama huu unatakiwa kutengenezwa kwa ajili ya makundi tajwa hapo.
3. Utumiaji wa neno wanyonge, kumaanisha watanzania wa kawaida, watu wazima, wenye afya na akili timamu si sahihi na ni hatari.
Hii ni kwa sababu inawajengea watu negative mentality kuhusu uwezo wao kwenye kujenga maisha yao wenyewe na kuchangia maendeleo ya nchi yao.Kwa lugha nyepesi, tunatengeneza kizazi kibachoamini kina haki bila wajibu, hiyo kinastahili kutendewa na chenyewe hakina la kufanya ili kuboresha hali ya kimaisha.
Mafanikio au kufeli kwenye maisha huanza na fikra/ mentality, kuna mentality ya umaskini, mtu akiwa nayo hawezi kuwa tajiri. Kuna mentality ya kushindwa, mtu akiwa nayo hawezi kuweza n.k kuna mentality ya kuweza ambayo ni hatua ya kwanza ya mafanikio.
Ni vizuri tukaijengea jamii ya Watanzania positive mentality 'ya kuweza' kama hatua ya kwanza kuelekea kwenye maendeleo.
Aidha, kwa kuwa kweli tuna wanyonge kwenye jamii yetu 'walemavu na watoto yatima" uundwe mfuko maalum wa kuwasaidia kama watu wenye mahitaji maalum badala ya kuachwa wazunguke wakiombaomba.
wanyonge ni sehemu ya jamii yetu, ni binadamu wenzetu na wa na haki hivyo ni vyema kusaidiwa.