Distributive justice; Mnyonge ni nani Tanzania na ni kipi anachostahili

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Mnyonge hasa ni nani Tanzania, ni kipi anachostahili, nani afanye nini na ni yapi madhara ya kutumia dhana hiyo isivyostahili.

1. Mnyonge ni mtu asiyeweza kujipigania yeye mwenyewe ili kuweza kujipatia mahitaji yake ya msingi.

Kwa mantiki hiyo, ni kweli tuna wanyonge nchini ambao ni 'walemavu' na 'watoto yatima'.

2. Tunashauri serikali ifikirie uwezekano wa kuanzisha mfuko maalum wa kuwasaidia wanyonge ambapo watakuwa na vituo maalum kila wilaya na wataendelezwa kupitia mfuko huu.

Hii ni kwa sababu makundi haya hayawezi kujihudumia yenyewe, hayajapenda kuwa hivyo na yana haki yakuishi maisha ya kibinadamu kama watu wengine, hivyo chini ya kanuni ya 'distributive justice' serikali ina wajibu wa kusaidia makundi haya.

Huwa inasikitisha sana kuona watu hawa wanatelekezwa wanaishi kwa kuomba omba.

Inatakiwa sehemu ya kodi inayokusanywa kutoka kwa wale wenye uwezo wa kuzalisha, itumike kusaidia wanyonge hawa.

Jambo hili sio geni, ndio maana wanunuaji wa umeme kwa mfano, wanakatwa makato flani kwa ajili ya kusaidia wasio na umeme vijijini wapate umeme chini ya mpango wa REA. Hiyo mpango kama huu unatakiwa kutengenezwa kwa ajili ya makundi tajwa hapo.

3. Utumiaji wa neno wanyonge, kumaanisha watanzania wa kawaida, watu wazima, wenye afya na akili timamu si sahihi na ni hatari.

Hii ni kwa sababu inawajengea watu negative mentality kuhusu uwezo wao kwenye kujenga maisha yao wenyewe na kuchangia maendeleo ya nchi yao.Kwa lugha nyepesi, tunatengeneza kizazi kibachoamini kina haki bila wajibu, hiyo kinastahili kutendewa na chenyewe hakina la kufanya ili kuboresha hali ya kimaisha.

Mafanikio au kufeli kwenye maisha huanza na fikra/ mentality, kuna mentality ya umaskini, mtu akiwa nayo hawezi kuwa tajiri. Kuna mentality ya kushindwa, mtu akiwa nayo hawezi kuweza n.k kuna mentality ya kuweza ambayo ni hatua ya kwanza ya mafanikio.

Ni vizuri tukaijengea jamii ya Watanzania positive mentality 'ya kuweza' kama hatua ya kwanza kuelekea kwenye maendeleo.

Aidha, kwa kuwa kweli tuna wanyonge kwenye jamii yetu 'walemavu na watoto yatima" uundwe mfuko maalum wa kuwasaidia kama watu wenye mahitaji maalum badala ya kuachwa wazunguke wakiombaomba.

wanyonge ni sehemu ya jamii yetu, ni binadamu wenzetu na wa na haki hivyo ni vyema kusaidiwa.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Baadhi ya nchi zilizoendelea, watu wasio na ajira vile vile huwekwa kwenye kundi la wanyonge na hivyo kulipwa kima cha chini kila mwezi ili waweze kujikimu. Hata hivyo hili kwa africa sio wazo zuri, kwani kulingana na tamaduni zetu, watu wengi wataamua wasifanye kazi kwa makusudi, ili wawekwe kundi la wanyonge na waishi kwa ruzuku
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,650
2,000
Mnyonge sio lazima awe na udhaifu wa viungo vya mwili au hali zao kama ulivyoonesha, mnyonge mbaya zaidi ni yule mwanasiasa anaeacha kutumia akili yake kwenye mambo ya msingi badala yake anabadilika hovyo kutegemeana na nani ndie bosi wake, huyu kwangu ndie mnyonge zaidi ya hao wanyonge mnaowazungumzia nyie.

Ukishakuwa mnyonge kichwani wewe lazima utadumaa tu, na mbaya zaidi pole kwetu tuliokabidhi nchi kwa wanyonge wa aina hii ambao hawana hata misimamo wasiojua nchi ielekee upande upi, ndio maana hili taifa bado linapigana na maadui wale wale watatu zaidi ya miaka hamsini toka tupate uhuru, huo unyonge mnaouzungumzia nyie wa wananchi zaidi umesababishwa na unyonge wa akili wa viongozi wa nchi yetu.

Ukitaka kusolve hilo kwanza, wale viongozi wafundishwe umuhimu wa kutumia akili zao kwenye mambo ya msingi yanayolihusu taifa, sio kubadilika hovyo mitazamo yao kuangalia nani anaongoza nchi.

Akija kiongozi mbovu wana support ubovu wake kwa unyonge wa akili zao hata kama utaliangamiza taifa ndio maana leo tunapiga kelele na ripoti ya CAG, matokeo yake wananchi wanaendelea kusababishiwa umasikini usiokuwa na maana, zikiwemo huduma mbovu za afya wakati mapesa mengi yanayopotea kwa uzembe wa viongozi wetu.
 
Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
498
1,000
Mnyonge hasa ni nani Tanzania, ni kipi anachostahili, nani afanye nini na ni yapi madhara ya kutumia dhana hiyo isivyostahili.

1. Mnyonge ni mtu asiyeweza kujipigania yeye mwenyewe ili kuweza kujipatia mahitaji yake ya msingi.

Kwa mantiki hiyo, ni kweli tuna wanyonge nchini ambao ni 'walemavu' na 'watoto yatima'.

2. Tunashauri serikali ifikirie uwezekano wa kuanzisha mfuko maalum wa kuwasaidia wanyonge ambapo watakuwa na vituo maalum kila wilaya na wataendelezwa kupitia mfuko huu.

Hii ni kwa sababu makundi haya hayawezi kujihudumia yenyewe, hayajapenda kuwa hivyo na yana haki yakuishi maisha ya kibinadamu kama watu wengine, hivyo chini ya kanuni ya 'distributive justice' serikali ina wajibu wa kusaidia makundi haya.

Huwa inasikitisha sana kuona watu hawa wanatelekezwa wanaishi kwa kuomba omba.

Inatakiwa sehemu ya kodi inayokusanywa kutoka kwa wale wenye uwezo wa kuzalisha, itumike kusaidia wanyonge hawa.

Jambo hili sio geni, ndio maana wanunuaji wa umeme kwa mfano, wanakatwa makato flani kwa ajili ya kusaidia wasio na umeme vijijini wapate umeme chini ya mpango wa REA. Hiyo mpango kama huu unatakiwa kutengenezwa kwa ajili ya makundi tajwa hapo.

3. Utumiaji wa neno wanyonge, kumaanisha watanzania wa kawaida, watu wazima, wenye afya na akili timamu si sahihi na ni hatari.

Hii ni kwa sababu inawajengea watu negative mentality kuhusu uwezo wao kwenye kujenga maisha yao wenyewe na kuchangia maendeleo ya nchi yao.Kwa lugha nyepesi, tunatengeneza kizazi kibachoamini kina haki bila wajibu, hiyo kinastahili kutendewa na chenyewe hakina la kufanya ili kuboresha hali ya kimaisha.

Mafanikio au kufeli kwenye maisha huanza na fikra/ mentality, kuna mentality ya umaskini, mtu akiwa nayo hawezi kuwa tajiri. Kuna mentality ya kushindwa, mtu akiwa nayo hawezi kuweza n.k kuna mentality ya kuweza ambayo ni hatua ya kwanza ya mafanikio.

Ni vizuri tukaijengea jamii ya Watanzania positive mentality 'ya kuweza' kama hatua ya kwanza kuelekea kwenye maendeleo.

Aidha, kwa kuwa kweli tuna wanyonge kwenye jamii yetu 'walemavu na watoto yatima" uundwe mfuko maalum wa kuwasaidia kama watu wenye mahitaji maalum badala ya kuachwa wazunguke wakiombaomba.

wanyonge ni sehemu ya jamii yetu, ni binadamu wenzetu na wa na haki hivyo ni vyema kusaidiwa.
Tanzania hakuna Wanyonge Kuna MASIKINI wa Kutupwa
 
MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,689
2,000
Viongozi wanapora haki za wananchi, Kama Fedha zao za akiba Mafao PSSSF na NSSF na kujilipa... halafu wanaita wananchi wanyonge'

Wabunge walipitisha sheria ya kupora FAO LA KUJITOA bungeni 2018
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
denooJ unenichekesha kweli. Hahhhahahh
Ila kweli kuna unyonge watu fikra na unyonge huo ndio hatari zaidi. Kwa bahati nzuri ni kwamba unyonge wa aina hiyo unajengwa na unaweza kubomolewa kutokana na utashi wa watu.

Kuna mtu kwenye kuzungumzia unyonge wa kifikra na unavyoweza kujengwa na kuathiri, akatolea mfano wa kukuza mtoto wa tembo kwenye kundi la ng'ombe, akiwa mkubwa na yeye anadhani ni ng'ombe kumbe tembo hahahaha. Au ukimfunga kamba kwa muda mrefu hata ukimfungulia haondoki tena, anadhani bado amefungwa
 
Hii dhana ni kama inafurahisha kusema ukweli japo inasikitisha pia, siku hizi naona watu wameanza kuikataa dhana ya kuitwa wanyongwe, yaani wanasiasa wametujaza ujinga sasa tunagoma sisi sio wanyonge tena, hivi utaachaje kuwa mnyonge kama huna ajira ya kukupa kipato cha kuishi bado unamtegemea mzazi licha ya kumaliza chuo?, au ajira ipo lakini kipato ni kidogo kisichoweza kukidhi mahitaji yako? hapa lazima tukubali hili ni taifa la wanyonge, labda chakujipa moyo ni vile huu unyonge wetu umesababishwa zaidi na sera na maamuzi mabovu ya viongozi wetu, hatujapenda sisi kiwa wanyonge.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Huu dhana ni kama inafurahisha kisema ukweli japo inasikitisha, siku hizi naona watu wameanza kuikataa dhana ya kuitwa wanyongwe, yaani wanasiasa wametujaza ujinga sasa tunagoma sisi sio wanyonge tena, hivi utaachaje kuwa mnyonge kama huna ajira ya kukupa kipato cha kuishi bado unamtegemea mzazi licha ya kumaliza chuo?, au ajira ipo lakini kipato ni kidogo kisichoweza kukidhi mahitaji yako? hapa lazima tukubali hili ni taifa la wanyonge, labda chakujipa moyo ni vile huu unyonge wetu umesababishwa zaidi na sera na maamuzi mabovu ya viongozi wetu, hatujapenda sisi kiwa wanyonge.
Kuhusu suala la ajira ni jambo serious sana ambalo kwa kweli linahitaji watu wakae chini na kufikiri kwa kina ni nini kifanyike. Ni suala complicated kidogo
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,650
2,000
Kuhusu suala la ajira ni jambo serious sana ambalo kwa kweli linahitaji watu wakae chini na kufikiri kwa kina ni nini kifanyike. Ni suala complicated kidogo
Kama kuna jambo lolote ambalo ni chanzo cha unyonge wetu lazima lijadiliwe tu, usilipe title ya seriousness, hata afya na ukosefu wa madawa navyo ni serious pia, hivyo hapa ni kuamua tu, waanze na kipi kwa namna ipi then wakamalizie na kipi.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Kama kuna jambo lolote ambalo ni chanzo cha unyonge wetu lazima lijadiliwe tu, usilipe title ya seriousness, hata afya na ukosefu wa madawa navyo ni serious pia, hivyo hapa ni kuamua tu, waanze na kipi kwa namna ipi then wakamalizie na kipi.
Sio waanze, 'tuanze' kuna kautamaduni ka kila mtu kudhani ni mwenzake. Yaani kila mtu anafikiri kuna mtu/ watu wanatakiwa kufanya, halafu huyo anayefikiriwa na yeye pia anafikiria kuna watu, sio yeye
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,650
2,000
Sio waanze, 'tuanze' kuna kautamaduni ka kila mtu kudhani ni mwenzake. Yaani kila mtu anafikiri kuna mtu/ watu wanatakiwa kufanya, halafu huyo anayefikiriwa na yeye pia anafikiria kuna watu, sio yeye
Waanzie kule bungeni Azizi.

Huku mitandaoni tumeshamaliza hayo siku nyingi kuyajadili.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom