Dissertation/ Thesis, Project editing, proof reading and general help | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dissertation/ Thesis, Project editing, proof reading and general help

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by McMoze, Dec 19, 2011.

 1. M

  McMoze Member

  #1
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dear all,
  Experienced experts in proposal writting, dissertation editing and general help available for you at a very affordable cost. In case you are in need for such help you simply give us a call at, 0767670307.

  Make your project look smart and get your degree right away
   
 2. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nyie ndio mnaoua Elimu ya Tanzania. Waacheni wanafunzi wafanye wenyewe. Kwani huko makazini nani atawasaidia?
  Najua mnatafuta pesa lakini mnaua kizazi cha wa Tanzania.
   
 3. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Kiongozi ni kweli asilimia mia! Vile vile nimesikia kuna program moja ambayo inatambua kama hizo dissertations/thesis ni genuine au fake!
   
 4. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  ndugu yangu huo ujasiriamali mnaufanya una mustakabali mbaya kwa nchi yetu, kwani inaandaa kizazi kisichoweza kufikiri na kufanya maamuzi based on analysis. Ni kati ya vitu/ubunifu ambao serikali ingezipiga vita na marufuku kabisa. Kwa ufupi ni kwamba hazifahi kabisa.
  Mimi kuna jamaa mmoja wa mba-mzumbe, alishakuja kwangu nimsaidie kunyoosha proposal yake, which is good kwani aliiandika yeye. Nilifanya hivyo, then baada ya proposa kuwa nzuri na kupita kwa supervisor akarudi na kusema ohoooo, unajua niko busy halafu inaonekana utanisaidia; hivyo tukubaliane bei ili nimfanyie; hakika nilimwambia kwamba ni kweli nahitaji pesa lkn sitaki kushiriki au kuwa sehemu ya madudu atakayokuwa anafanya kwenye jamii/kazini.
  Such kind of entrepreneurshp we call it "destructive entrepreneurship" because of its negative impacts to the society.
   
 5. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Acheni wanafunzi wasumbue akili zao wenyewe!.
   
 6. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  hii ni rubish!!!!. hata anayeweka hili tangazo uwezo wako utakuwa ni wa kubabaisha tu , kama si mwizi wa wazi kuibia vijana wasiojiweza au wavivu kielimu basi hujui unatenda nini. nachukua hii namba ninakupigia, na nitakutana nawe. ila jiandae, nakupa miezi miwili utafute kazi nyingine, la sivyo, utaishia kupata vijana wa sekondari
   
 7. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  The best students learn things the hard way. Acha supervisor amrudishe aandike upya hata zaidi ya mara ishirini. Ndo kujifunza huko. Hakuna laini laini. Stop ruining our brothers and sisters you ****
   
 8. M

  Mtandu Member

  #8
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani, kwani kawalazimisha? Yeye kasema anachoweza kufanya kusaidia na kama hutaki basi acha kupeleka kazi zako. Maana kama kweli wewe umesoma ungejua 'editing' na 'proof reading' sio kudumaza elimu. Hiyo ni taaluma ya watu wachache na sio kila mwanafunzi wa Masters or PhD ni editor au ana ujuzi wa ku-proof read. Hata ma-professor wanapeleka kazi zao kuwa edited na wataalam. Sasa ubaya hapo ni nini? Mbona kuna watu wanaandika humu mambo ya kipuuzi zaidi na hamlalamiki? Tulizaneni akili.
   
 9. K

  Kolero JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 493
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu unachosema ni kweli lakini hao wahusika wa pande zote mbili watazingatia hayo? Isije ikawa ni kuanza kuandikiwa kila kitu na hapo ndipo wasiwasi ulipo, hiki ni kitu muhimu sana katika taaluma kikichakachuliwa basi ujue ni janga la kitaifa.
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,918
  Trophy Points: 280
 11. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Huu nao ni ufisadi na unastahili kukemewa kwa nguvu zote!

   
 12. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #12
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Utashangaa wanaojidai kutaka kufanya hivyo wana shahada za kughushi. Mie mwanangu anasomea udaktari hapa Kanada. Sijui kama mna uwezo wa kuandika mambo yakaingia akili za maprof wa hapa hasa ikizingatiwa kuwa hata nyie mnaotangaza upuuzi huu hamna ujuzi. Tufanye hivi, nafanya PhD yangu kwenye CRS. Sijui huo ujuzi wa kuandika Dessertation yangu mnaupata wapi au nyie ni kama Mungu mnajua kila kitu. Acheni utapeli wa kipumbavu. Kama ni kutapeli angalau tumieni na akili.
   
 13. JAPUONY

  JAPUONY JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jamani wana JF naomba nitoe shule kidogo kuhusu Mradi walioufungua hao ndugu zetu. Kwanza siyo mradi Mgeni hapa nchini na kwingineko Duniani. Ni kitu kinafanyika katika vyuo vikuu vingi na maarufu kuliko vyuo vyetu vya kibongo. Nakubaliana na mawazo kuwa watu wafanye kazi independently ili kujenga umahiri katika fani yoyote ile amabayo mtu anasomea au anayofanyia utafiti. Lakini tukumbuke kuwa proof reading of dissertation (s) siyo kumfanyia mtu utafiti wala kumwandikia mtu wawazo. Nikuwa mtu anakuwa amekwisha fanya tafiti na ameandika matokeo ya utafiti wake. Ripoti inaweza kuwa kurasa zaidi ya 100! kusoma ripoti nzima wewe mwenyewe kwa maana ya kuupitia upya unaweza usigundue makosa kwa maana mawazo uliyatoa wewe na uliyaandika wewe kwahiyo kugundua makosa siyo rahisi kama vile unyoofu wa sentensi, koma, kituo kikuu na alama nyingine nyingi. Mtu mwingine tofauti na mwandishi ni rahisi kufanya editing kwa namana hiyo.

  Kingine nikuwa, proof reading kwa mtu wa Masters na PhD inafanyika kwa mtu ambaye tayari anajua kuwa anataka nini na siyo kweli kuwa kila wazo la proof reader ataikubali. Lazima wata-negotiate namna ya kuweka wazo linaloonekana kuwa linahitaji kuboreshwa katika ripoti. Lakini pia ieleweke kuwa proof reading inasaidia kuokoa muda wa uandishi wa ripoti ya utafiti au kitu chochote kile kama vile articles nk. Niwaulize ninyi mnaobisha kuwepo kwa kazi hii kuwa Wahariri wa Magazeti wanadumaza akili za wanaoandika articles au makala katika magazeti?

  Katika masomo ya Sayansi na Hisabati (science and mathematics subjects) kuna matumizi ya calculator, hivi, zinafaa kutumika mashuleni?Hivi, calculator zinadumaza ubongo za wanafunzi wetu Tanzania?Kuna matumizi ya computer katika kufanya mambo mbali mbali hata katika planning, kuchora majengo, kufanya mahesabu nk; hivi, nayo hayafai?

  Hebu fikiria hawa watu na mabango yao hapa chini, je wangeenda kwa proof reader haya makosa yangeonekana?

  SCOOL ; YOUR WELLCOME; Nk.

  [​IMG] [​IMG]

  Kwaheri wandugu!
   
 14. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,368
  Trophy Points: 280
  Jamani acheni uNYAMBARI NYANGWINE. Mnadumaza elimu.
   
 15. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #15
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Japuony you got it right.

  Wengine wanaishia kututishia kuwa wako Kanada na watoto wao wanasomea udaktari nao wakisomea CRS...upuuzi mtupu kama PhD scholar ndo fikira zimegotea hapo
   
 16. u

  utantambua JF-Expert Member

  #16
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
 17. a

  anonimuz Senior Member

  #17
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 102
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kwanza, hawa jamaa hawafanyi proof reading peke yake, wanaandika dissertations pia (soma post yao vizuri). Sasa kwa mtu ambaye anachukua PhD, writing ni sehemu kubwa ya kuwa scholar. Huwezi kuwa PhD holder and then utegemee kufanya tu research bila kuwa na uwezo wa kuandika results/findings zako mwenyewe. If you cannot write then going for a PhD is, lightly put, a terribly-stupid move. This goes to most Masters programmes as well.

  Pili, hata kama wangesema wanafanya proof reading alone (editing, as they put), bado nisingewaunga mkono coz that's what supervisor's are for. Na supervisor anakuwa ni mtu ambaye ana knowledge ya kutosha kwenye area ambayo unaifanyia research so atafanya marekebisho sio tu kwenye grammar, formatting etc ila pia kwenye content. Sasa, unless hawa jamaa zetu wanaojitangaza hapa ni group ambayo ina scholars (PhD holders, researchers, etc) wa kila fani duniani hapa, there's no way utaniambia wanaweza kufanyia editing ya dissertation ya mtu yeyote. That's simply implausible.

  Halafu hiyo mifano yako iko way off. Tuchukue mfano wako wa tangazo la SCOOL. Tu-assume kuwa mimi ni fine artist (analogous to a researcher), kazi yangu kuandika matangazo kwenye mabango (analogous to writing a dissertation). Ninaenda kijijini na ninahitajika niandike tangazo la mgahawa, sijui kama mgahawa unaitwa RESTAURANT (analogous to correct research content), akili yangu inaniambia mgahawa unaitwa SKUL (analogous to wrong research content) na inakuwa spelled SCOOL (kama mfano wako unavyosema). Ninamuomba fine artist mwenye kujitangaza kuwa anafanya editing na wrtiing ya matangazo (analogous to jamaa zetu hawa). Huyu jamaa anaweza kuwa editor mzuri na mwandishi mzuri ila kwenye knowledge, not so much (jamaa zetu ni writers na editors wazuri, ila hawawezi kuwa na knowledge ya kila field duniani). So hana uwezo wa kubadilisha content (SCHOOL inabaki kuwa SCHOOL, na siyo RESTAURANT). So ana-edit SCOOL kuwa SCHOOL (awesome editing) na ananiandikia tangazo (what a relief!).

  Two things: First, as far as the spelling (analogous to grammar and formatting) goes, we are good. Ila content bado tumechemka, tumeweka bango la SCHOOL kwenye mgahawa. Pili, mimi kama fine artist ninatakiwa niandike mwenyewe hilo tangazo kuongeza experience na kuwa na genuine portfolio, that doesn't happen here.
   
Loading...