Disemba 9 kila mwaka: Tunasherehekea uhuru wa nchi ipi?

Katiba inaitambua Tanganyika kama Tanzania bara kwa hiyo tunasherehekea uhuru wa TANZANIA BARA. Hakuna nchi inayoitwa Tanganyika.

Hivyo ina maana Tanganyika ilishakufa?????

mbona Zanzbar bado ipo???????

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!
 
Nimetoa mfano john akiitwa peter kuna tofauti kwenye mwili wa john, sio watu wote waitwe peter, uelewa mdogo unajinasibu kujua. SIJASEMA DUNIA NZIMA IWE JINA MOJA

Kama ulishaitwa John iweje uitwe tena Petro bila yua ridhaa yako???

Huu mfano bado hauleti maana katika kuf kwajina Tanganyika na kubakia kwa jina Zanzbar katika Tanzania.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kama ulishaitwa John iweje uitwe tena Petro bila yua ridhaa yako???

Huu mfano bado hauleti maana katika kuf kwajina Tanganyika na kubakia kwa jina Zanzbar katika Tanzania.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Unaweza kuwa hupendi kusikia Tanzania bara, ila ujue ridhaa ipo na ilitolewa na kiongozi mkuu ambaye alipewa dhamana na wananchi, unataka ridhaa ya wahuni??? rais aliyekuwepo alitoa ridhaa hiyo na akaendelea kuchaguliwa kwa miaka zaidi ya ishirini tangu abadili jina, hiyo ni tosha ridhaa ya wananchi. Tanganyika ni Tanzania bara kwa mipaka na kila kitu.
 
Tanzaniza ni muungano wa nchi mbili,kuna Zanzibar na Tanganyika na wote tulipata uhuru nyakati tofauti.Inanichanganya nikisikia watu wanasema miaka 49 ya uhuru wa Tanzania.

Msaada wenu unahitajika sana,nipe elimu mimi sijui faida za muungano lakini nitalinda na kuheshimu mawazo ya wazee wangu na kutetea muungano kwani wote ni wamoja kihistoria mkoloni ndio alileta utofauti.

Usinipotoshe niambie ni Tanganyika au Tanzania
.

Hakuna nchi inayo itwa Tanzania/bara iliyo pata Uhuru 09.12.1961! No upotoshaji mkubwa wa historia ambako watoto na wajukuu zetu hawatatuelewa kwa nini tulikua tunajidanganya kiasi hiki.

Nchi iliyo pata uhuru tarehe hiyo ni Tanganyika! Kituko zaidi ni nchi ya Zanzibar ambayo usherehekea Mapinduzi ya Umwagaji damu tarehe 12.01.1964 badala ya siku ilipopata Uhuru wake! Historia imeandikwa kwa matakwa ya kikundi fulani badala ya ukweli halisi.
 
Semeni kwanza ni nani aliipa nchi yetu hilo jina la 'Tanganyika' alafu tumlinganishe na aliita 'Tanzania bara' ndio tujue ni yupi mwenye haki/uhalali wa kutoa jina la yetu nchi.
 
Hakuna nchi inayo itwa Tanzania/bara iliyo pata Uhuru 09.12.1961! No upotoshaji mkubwa wa historia ambako watoto na wajukuu zetu hawatatuelewa kwa nini tulikua tunajidanganya kiasi hiki.

Nchi iliyo pata uhuru tarehe hiyo ni Tanganyika! Kituko zaidi ni nchi ya Zanzibar ambayo usherehekea Mapinduzi ya Umwagaji damu tarehe 12.01.1964 badala ya siku ilipopata Uhuru wake! Historia imeandikwa kwa matakwa ya kikundi fulani badala ya ukweli halisi.

Ulitaka wazanzibari washerehekee uhuru feki ambapo muingereza alikabidhi nchi kwa vibaraka wake waarabu akaendelea kula 10%?
 
Ulitaka wazanzibari washerehekee uhuru feki ambapo muingereza alikabidhi nchi kwa vibaraka wake waarabu akaendelea kula 10%?

Sasa Zanzibar ilipata Uhuru lini? Januari 12 wanahadhimisha Mapinduzi,mbona hawasemi wanahadhimisha siku ya Uhuru wa Zanzibar? Usimeze kila kitu,vingine utabebeshwa mimba!
 
Sasa Zanzibar ilipata Uhuru lini? Januari 12 wanahadhimisha Mapinduzi,mbona hawasemi wanahadhimisha siku ya Uhuru wa Zanzibar? Usimeze kila kitu,vingine utabebeshwa mimba!

Sisi wazanzibari wenye kujitambua, tuna ufahamu uhuru tulipata kwa muengereza Dec 1963, hao wauwaji wa wazanzibari kwa uchu wao wa madaraka wanajua mapinduzi ndio uhuru kumbe mapinduzi ndio kupokonywa uhuru na Tanganyika
 
Tanzaniza ni muungano wa nchi mbili,kuna Zanzibar na Tanganyika na wote tulipata uhuru nyakati tofauti.Inanichanganya nikisikia watu wanasema miaka 49 ya uhuru wa Tanzania.
Usinipotoshe niambie ni Tanganyika au Tanzania
.
Watangazaji wako very right, tunasherehekea miaka 53 ya uhuru wa Tanzania na sio Tanganyika, kwa sababu maandimisho ni present, kilichopo sasa!, japo ni kweli iliyopata uhuru ni Tanganyika, which doesn't exist any more, kilichopo sasa ni Tanzania, tunasherehekea uhuru wa Tanzania.

Jee wewe mkuu JayJay siku ulipozaliwa ulizaliwa na jina?!, unaposherehekea siku yako ya kuzaliwa, jee unasherehekea siku ya kuzaliwa yule mtoto aliyezaliwa siku ile bila jina, au huyu Jay Jay aliyepo?!.

Na kama ni mwanamke, tuseme umeolewa na Pasco, hiyo Jay Jay was a maiden name, sasa ameolewa anaitwa Mrs. Pasco, siku ya kuadhimisha birthday yako tutaadhimisha siku ya kuzaliwa ya Mrs. Pasco, sio ya Jay jay wala ya yule mtoto asiye na jina!.

Tanganyika doesn't exist any more, kilichopo sasa ni Tanzania, na eneo la ilipokuwa Tanganyika ndio Tanzania bara!.

NB Apology in advance in case Jay Jay is a male!.

Pasco.
Wajameni ni katika kukumbushana tuu kuwa maadhimisho ya leo ni ya Uhuru wa Tanzania, na sio wa Tanganyika!.
Nawatakia sikukuu njema ya Uhuru na Jamhuri.
P
 
Rest in peace mzee mtikila mtanganyika pekee aliekuwa anaitetea Tanganyika na siku kama ya Leo angekuwepo lazima amgeibuka pale mwanza na bendera ya Tanganyika akiadhimisha.

Miaka 58 ya Tanganyika huru
Miaka 55 ya Tanzania
 
Daah. Hii haiingii akilini, sidhani kama hii inaweza kuwa ni taafiri ya kisheria, labda kisiasa tena, tena siasa za ujanja ujanja.

MTU angesema Uhuru wa Tanzania Bara ningumuelewa sio Uhuru wa Tanzania. Huu ni upotokaji na upotoshaji mkubwa
 
Back
Top Bottom