Dirisha la kutuma maombi ya Ajira za Ualimu lafunguliwa rasmi. Vigezo vyawekwa wazi, namba ya NIDA yawa kigezo muhimu

026 216 0210
Namba ya bure TAMISEMI
unapiga kuuliza tatizo lolote!
Pigeni kuuliza kuhusu miaka na tarehe mbona zinarudi nyuma?
Mfano 5 September itakua 4 September
We ulivouliza wamekwambiaje
 
Wameongeza mda
IMG-20200918-WA0011.jpg
 
Mara ngapi wanatoa tangazo la ajira? Hizo ni ajira za wanyonge, acha wapiganie kwasababu wanyonge hutumiwa kama daraja la kuwanufaisha watu.

Nchi za kiafrika ni za kijinga sana. Wameona kipind cha uchaguzi, ndiyo wanatoa viajira uchwara. Kama walishindwa kuajiri tangu 2015. Wala siamini hizo ajira zao mpaka kesho kutwa.

Wewe bila shaka tayari una ajira
 
Unafanya nini baada ya kukimbia huko?
Mwaka jana zilitokea nafasi kama hizi. Mimi nilipangiwa kazi halmashauli ya Mpwapwa Dodoma kama mwalimu wa Physics & Mathematics. Bila kusahau kua mimi sijasoma ualimu ila kwa sifa kama walizosema hapa ilikuepo hiyari yakuamua kuwa mwalimu.

Kufupisha story, ualimu nilifanya siku 4 nikaacha (Siku niliyoenda kesho yake nikaondoka, baada ya wiki mbili nikaenda tena nikakaa siku tatu nikaondoka milele, jumla siku nne). D.E.O alitaka nimsujudie, sikukubali. Siku zote 4 nilizokua kituo cha kazi sikupatikana hewani maana laini zangu za voda na tigo kule hazishiki kabisa.

Kuna gari moja tu linalotoka kule kwenda mjini. Linaondoka saa tisa usiku. Ukilikosa hilo hakuna tena safari. Kwakifupi kupanga safari yakwenda mjini ni kupanga mkesha.

Jumapili hilo gari halisafiri. Kwahyo ukikesha usiku wa ijumaa kuamkia jumamosi, utasafiri ufike mjini saa tatu asubuhi na ili jumatatu uwe kazini itabidi jumamosi hiyohiyo saa saba mchana uwe kwenye gari hiyo hiyo maana huo ndo muda wakurudi. So una chini ya masaa manne kukamilisha kilichokupeleka mjini. Ila unasafiri kwa zaidi ya masaa 13 kwenda mjini.

Nimechanganya mengi hapo ila shortly, nafasi ni chache watu ni wengi (Ni nafuu zaidi kama una Physics & Mathematics). Mazingira ya kazi ni Magumu. Mshahara ndo ivo tena. Kada ya ualimu inadharaulika.

Sikukatishi tamaa nasema uyafahamu mazingira yako ya kazi. Focus kwenye vision yako no matter how hard the situation seems to be. In my case at that time I chose to flee. I wouldn't recommend the same choice for you.

Niliambulia hela ya kujikimu thought.
 
Back
Top Bottom