Dira ya Vijana

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
263
13
Nimesoma Mwananchi ya Leo nikaona kauli ya Vijana hawa kuhusu kufanya mageuzi ya uongozi, nikakumbuka kwamba mwaka 2005 waliwahi kuandika kile walichokiita ajenda ya vijana kwenye uchaguzi huo. Nimefanya google search nimekutana na hotuba hii ya kiongozi wao. Je, hawa vijana wanabeba kweli dira ya vijana kama jina lao lilivyo? Nini nafasi yao katika siasa na maendeleo ya vijana kwa ujumla hapa nchini?



WARAKA WA NDUGU DEUS. R. VALENTINE, MAKAMU MWENYEKITI WA TYVA (FEBRUARI 2007 – MACHI 2008) KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUZALIWA KWA TYVA TAREHE 29 JULAI, 2008.
Ndugu zangu wana TYVA,
Kwanza nianze kwa kuwapongeza kwa kuhusika kwa namna moja au nyingine na maendeleo ya kila siku ya asasi yetu.
Binafsi siku zote nimejiskia furaha kuwa sehemu ya familia yetu hii kubwa. Naamini siku zote nina deni kubwa kwa familia yetu hii. Ni jambo lisilohitaji mjadala kwamba asasi yetu kwa kipindi cha takribani miezi kumi na sita imekuwa sehemu kubwa ya maisha yangu. Imenisaidia kupata mambo lukuki ambayo kila binandamu anategemewa kuyapata anapoishi kwenye familia fulani.
Naomba niwashukuru wale wote ambao katika kipindi hichi cha kufanya kwangu kazi na TYVA tumeshirikiana katika kufanikisha mambo mbalimbali for the common good of the association. Naamini ni watu wengi na si ajabu nkashindwa kuwataja wote. I must confess: niliingia TYVA nikiwa sina uhakika TYVA hasa ni nini. Kile tu nilichofahamu ni kwamba nakumbuka kuwa naiona TYVA kwenye vyombo vya habari mara nyingi sana kipindi cha nyuma kidogo nikawa napata faraja sana kuona jinsi vijana wenzangu walivokuwa na hamasa ya kupigania yale wanayoamini. Binafsi sikudhania kama ningeishia kuwa mmoja wa vijana hao. Kwa wale wanaofahamu vizuri historia yangu watakugundua kuwa mimi ni mseminari. Katika mazingira hayo nilikuwa ni mtu niliyelelewa kuwa muumini zaidi wa kiongozi wangu na sheria zinazotungwa na viongozi hao hivyo swala la kutetea imani yangu na msimamo wangu kuhusu mabo mbalimbali halikuwa sehemu kubwa ya utamaduni wangu.
Ukiacha kuiona TYVA kwenye Televisheni nakumbuka ni ndugu yangu Michael Dalali aliyejitahidi kunielezea kuhusu harakati za TYVA baada ya yeye mwenyewe kuanza kuhusika nazo. Ndipo nikaanza kutemeblea tovuti ya asasi yetu mara kwa mara nifahamu hawa wanaTYVA huwa ni watu wa namna gani, huwa wanawaza nini, kilichofuata niliishia kwenda kwenye mdahalo mmoja uliofanyika ubungo plaza nikamkuta kakangu Welwel akiongoza mdahalo ule. Kilichonivutia ni kwamba mama mmoja aliyekuwa anawakilisha serikali pale alikuwa amewekwa kitimoto mpaka nikamuonea huruma. I was amazed with what was happening. Katika kipindi hicho nilikuwa nimeshachana na seminari na nilipokuwa shuleni Loyola nikawa mtu ninayependa sana kutetea yale ninayoamini saa nyingine nikiwaudhi watu wengi. Nadahani ilitokana na kuishi kwa muda kwenye tamaduni ambayo haikunipa fursa tosha kufanya hivo hapo awali. Baada ya mdhahlo ule nilijiskia kuvutika sana na TYVA nilipotambulishwa kwa kakaangu Mayunga alionekana kama mtu wa mzaha hivi nikapata wasiwasi kama na yeye ni mmoja wanaTYVA hiyo ilikuwa kabla sijamkuta kazini. Michael akanitambulisha kwa aliyekuja kuwa mwenyekiti wangu Dada Suma nikaona that serious look on her face nikasema moyoni “this is definitely one of them”. Hatahivyo moja ya vitu ambavyo huwa sivitaji sana ni kwamba nilivutiwa sana binafsi na Ndugu yangu Mnyika only to realize alikuwa amepunguza kujihusisha kwake na TYVA. Ndugu yangu huyu hatahivo amekuwa source ya inspiration kwangu. Nilipoingia ofisini nilijikuta nasoma kila document niliyokuta ina jina lake. Hili swala ambalo naamini hata yeye binafsi hafahamu.
Naomba kwa namna ya pekee niwashukuru uongozi nilioukuta TYVA wa ndugu zangu Daniel Welwel, Eric Ongara, Alex Mayunga, Elly Mgumba, Suma Stephen, Edward Kinabo na Tobias Makoba. Nawashukuru wao kwa kuwa waliona mimi na wenzangu tungeweza kuliendesha gurudumu la TYVA wakatukabidhi. Nawashukuru kwa kuwa hawakuwa na busara za Mzee wetu Mugabe za kutoamini uwezo wa watu wengine. Nawashukuru ndugu zangu tuliokuwa pamoja kwenye excom; Dada Suma, Kaka Michael, Dada Cecy, Ndugu yangu Mrisho, Mheshimiwa sana Nango Killian, Ndugu Shilla, Dada Wilfrida, Salma na Kaka yangu na ndugu yangu Aaron. Hawa wote namna moja au ningine walinisaidia sana kukuwa ndani ya TYVA.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama ntaacha kuwashukuru ndugu zetu Friedrichi Naumann Stiftung Fur die Freheit. Mchango wao kwa asasi yetu kwa kipindi ambacho nilihusika nayo sioni namna ya kuwarudishia. Kwa namna ya pekee namshukuru sana Dada yetu Veni Swai kwangu binafsi amekuwa sio tu dada bali ameenda mbali zaidi amekuwa mama. Naijiskia faraja siku zote kwa kufanya nae kazi. Mahusiano yetu na ndugu zetu hawa waliberali sidhani ni jambo la kubezwa kwa namna yeyote.
Nawashukuru wale wote wanachama wa asasi yetu tuliofanya nao kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Wapo wengine ambao hawakuwa wanachama lakini tulifanya nao kazi kwani kama iwavyo kwenye familia kunakuwa siku zote na wanafamilia na kuna kuwa na ndugu wa karibu sana tunaowaita “family friends”. Wapo ndugu wanafamilia kama kaka yangu Khalid wengine mnamuita “The Good Son” alinisaidia kupata ka “Nirvana” on what it means being “the good son”. Watu kama Khalid na wengine wa kizazi chake wamechangia sana mawaidha ili asasi yetu ispoteze kabisa dira yake. Wanachama wa enzi hizi waliojitolea kwa asasi yetu kama Naamala hawana budi kushukuriwa. Namtaja tu Naamala kwa niaba ya wengine wote. Naamini anaendelea na moyo huu.
Nimalizie shukrani zangu kwa kuwashukuru wanachama wa sasa na wale wote wanaoamini kuwa nilikuwa na mchango kwa TYVA. Ndugu yangu Sam, Justin na wengine I appreciate your compliments and I always will cherish them. Nawashukuru hata wale walioona kuwa nimekuwa mzigo kwa TYVA. Naamini wataweza kuonesha kwa wanaweza kuwa watu bora zaidi ndani ya TYVA. Mi ni muumini mkubwa wa dini ya changamoto na niasikia faraja kuishi na watu wenye nia ya kuonesha wao ni zaidi.
Nachukua nafasi hii vilevile kuwaomba radhi wale wote anbao wamekwazwa na uwepo wangu ndani ya TYVA. Naamini ni sehenu ya maisha ya binadamu. Naomba niwahakikishie kuwa sina kinyongo na yeyote aliyenikwaza ndani ya TYVA. Let us not dwell on hurdles let us use them as stepping stones towards further achievement.
Sasa nikisha kusema yote hayo naomba niwashirikishe ndugu zangu tafakari yangu juu ya asasi yetu. Nia yangu ni kuibua mjadala ambao si lazima uwe na mwisho. Mjadala utaotusaidia kurediscover our mission, kuredefine our common good to strengthen what we consider to be our values, mjadala utaotusaidia kutufunulia tafakari juu ya nafasi yetu katika kukuwa na kufa kwa TYVA. Naamini kama tutakuwa na ushiriki mkamilifu mjadala huu utasaidia kuleta maisha kwenye asasi yetu. Naamini ninayoandika ni misimamo yangu hivyo hatuna budi kushirikiana kujadili ili kuweza kuwa na misimamo ya pamoja. Naamini kuwashirikisha uzoefu wangu binafsi ndani ya TYVA utatusaidia kuelewa hali halisi ya sasa ya asasi yetu.
Nafasi yangu ndani ya TYVA:
Kama nilivoeleza hapo awali, niliingia TYVA nikiwa sina uhakika sana TYVA hasa ni nini. Hatahivo nilijikuta nikivutika sana na asasi hii. Nilijitahidi kujifunza zaidi na zaidi kuhusu asasi hii.
Baada ya kipindi cha kama miezi mitano ya kujifunza kwa jitihada binafsi na kwa msaada wa baadhi ya wanaTYVA nilichukua fomu nikaomba kuwa mwanachama. Katika kipindi cha muda mfupi nikaombwa kuangalia uwezekano wa kuwa kiongozi wa TYVA. Viongozi wa muda huo walikuwa wamefikia muda wamekubaliana na ukweli wa mambo kuwa hawakuwa katika nafasi bora kuendelea kuiongoza asasi na kwa uhalisia wake kuiendesha TYVA.
Sikuwahi kuwa na uhakika ningeweza kuiongoza TYVA kabla ya kuwa kiongozi. Hii ilitokana kwa kiasi kikubwa na sababu kuwa niliwaona wanaTYVA kama watu tofauti sana. Nakumbuka Tarehe 23 februari 2007 nilombwa na viongozi wa TYVA waliokuwa wakimaliza muda wao kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti. Nilishtuka nikajitahdi kuelezea hali yangu kuwa ndio kwanza nilikuwa nimemaliza kidato cha sita na sikuwa na nia ya kusoma nchini hivo sikuwa na budi kutokuwepo baada ya mwezi wa sita mwaka huo. Nilikuwa kijana ndogo sana. Umri wangu siku hiyo ulikuwa ni miaka 18 miezi mitano, siku 19 na masaa 11. Sikudhani ningeweza kuwa kiongozi wa watu ambao mimi nilidhani I had all to learn from and had nothing to offer to. Sidhani kama kulikuwa na mtu mwenye umri wangu ndani ya ukumbi wa karimjee siku ile.
Katika mazingira ambayo ilionekana TYVA ilikuwa katika hali isiyoridhisha nilijiskia vibaya kuona kwamba ningeweza kuwa mmoja wa watu ambao nilishiriki katika kuiangusha TYVA. Mapenzi yangu kwa TYVA yalikuwa makubwa na kwa sababu nilikuwa siku zote naisikia sana TYVA nikaamini kwamba kitendo cha kuwa kiongozi wa TYVA kingenipa heshima kubwa taratibu nikaanza kuona ningeweza kuwa na mchango mkubwa kwa TYVA baada ya kusikiliza ripoti za utendaji na mjadala mzito juu ya uwezo wa kifedha na uwezo wa kioganaizesheni hususan swala la matawi ya TYVA. Nikapiga moyo konde nikasema si haba, kama kwenda shule ngoja nianze na hii ya TYVA kwa mwaka mmoja.
Hatahivo niliamini sana kuwa nafasi ilikuwa ni kubwa mno kwangu kusema ukweli nilikuwa nimevutiwa sana kufanya kazi ya LAN au atleast uweka hazina. Nikahakikishiwa kwanba nisingekuwa na kazi ngumu hata kidogo kwa kuwa bosi wangu alikuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa. Nilipokumbushwa ni nani nikambuka yule dada serious wa Ubungo Plaza nikasema Aagh!! (now you are talking). Nikawa nimeshajiwekea azimio kuwa endapo ningechaguliwa kama makamu mwenyekiti siku hiyo ajenda yangu kubwa ingekuwa swala la uwezo wa kifedha wa asasi yetu. Hayo mengine yote nikawa nina uhakika bosi wangu angeweza kuyasimamia. Ikawa ilivokuwa, sikuwa na mshindani kwenye nafasi yangu nilienda kujinadi nikiwa nina uwoga mkubwa nikapewa ridhaa ya watu 39 kati ya 42 waliopiga kura siku ile.
Ilinichukua muda sio siri kujua kuwa majukumu yangu ndani ya asasi yalikuwa makubwa sana. Taratibu nikaanza kuona hali halisi nikagundua there was no time for me to learn from the others since those others didn’t really have time to teach me. Nikabaki kujifunza kutoka kwa Michael ambaye ndiye aliyekuwa karibu zaidi kwa uongozi uliopita. Nilikuwa mwoga sana kuharibu mambo na hadhi kubwa niliyoamini TYVA ilikuwa nayo. Nikatumia muda wangu mwingi kuuliza maswali. Nikajitahidi kutumia Warsha ya Kibaha ya Action Planning kujifunza kuhusu TYVA na kupata kujifunza mawazo ya uongozi uliopita ambao wengi wao ndio walikuwa waanzilishi wa TYVA.
Nikaendelea kujipa moyo mambo yangekwenda tu. Nikaja kugundua baada ya majuma mengi kupita kuwa sikuwa na budi kukaimu majukumu ya “bosi” wangu. Kwakweli mpaka hii leo sina uhakika ni nini hasa kilikuwa kinaendelea. Binafsi mara nyingi nimeamini Mwenyekiti wetu hakuwa tayari kutuongoza pale tulipompa nafasi. Naamini tunaoelewa status yake ya sasa isingekuwa rahisi akaweza kujigawa na kutumikia “mabwana wawili”. Hapo naomba nibainishe tuna udhaifu mkubwa wa kujenga viongozi wetu ndani ya TYVA. Tumejikuta mara nyingi tukichagua viongozi wetu out of “desperation”.
Kwa kipindi cha miezi kumi na tatu ambacho nilikua “kazini” TYVA nilikuwa na ndoto nyingi mno kwa ajili ya asasi yetu hasa baada ya kudhani kila mtu angetimiza wajibu wake. Niliiota TYVA yenye wanachama wapya wenye ari kuzidi ya kwangu zaidi ya 150 Niliota TYVA yenye uwezo wa kufanya press conferences kila inapobidi kwa mfuko wake, TYVA inayohitjai tu kufundraise kwa matukio makubwa ya nje, TYVA yenye miradi kadha wa kadha ikiendelea. I must admit, I was overly ambitious and definitely unrealistic.
Kama walivokuwa viongozi waliopita na mimi nikaanguka katika mtego wa kutokukubali kuwa TYVA ilikuwa inadondoka wakati huo. Nakumbuka ahadi za mweka hazina siku ya mkutano mkuu kwamba uongozi uliokuwa unaingia madarani unaachiwa akaunti CRDB yenye afya walau ya ugali maharagwe nikapata moyo.
Kadiri muda ulivokwenda nikagundua swala la msingi halikuwa akautni au miradi. Swala la msingi lilikuwa ni WATU. TYVA ni asasi ya Watu, Watu ndio wanachama, Ndio viongozi, pasipo hawa TYVA haipo. Nilikuja kugundua TYVA imekuza kizazi na kama ilivo kwenye jamii zetu hasa zile feudal societies za kimasai, kinyakyusa na kinyamwezi wanayaelewa haya. Kwamba jamii inaishi kwa kurithishana vizazi na katika hili kwa muda husika TYVA tulienda mrama.
Mimi naamini nilikuwa ni mmoja wa watu wachache wachache tuliokuwa tumebaki TYVA kipindi hicho. Hatahivi leo nasikitika kuwa katika kipindi cha uongozi wangu azma hii ya kuongeza rasilimaili watu kwa kiwango nilichokiota mimi haijafikiwa. Naamini hili ni moja ya maeneo ya udhaifu wa uongozi wetu.
Je, TYVA imekufa:
Si jambo la kushangaza kuwa kuna watu ambao leo hii wanaamini kuwa tumekufa. Wale waliokuwa wanaangalia habari kama mimi enzi zile na hawatuoni oni, wale wanaoingia kwenye tovuti yetu wakakuta haipo tena, wale wanaokuja ofisini Mwenge na kukuta hatupo wale wanopita Afrikasana na kudhani labda wamekosea si TYVA sisi.
Wapo wale wanaoshangaa mtu anayeitwa Elizabeth Riziki anjitambulisha kama Mwenyekiti wa TYVA. Inasikitisha kuwa baadhi ni wanachama waanzilishi wakiteta “ama kweli TYVA imekufa”. Wapo wenye uwezo mdogo wa kifikra walioshindwa kuitofautisha TYVA na Mnyika au TYVA na kina Daniel na Eric na Elly na Alex. Hawa ni wale ndugu zangu ambao bahati mbaya (naomba Mola awahurumie) wameamua kuishi na mawazo mgando.
Wapo vilevile wale ambao wanavutiwa na swala kwamba majina mapya yanatajwa ndani ya TYVA pasipo hata kujua uwezo wa viongozi hao. Wapo wadadisi ambao wanataka muda wote kuwafahamu vongozi wao na uwezo wao, tunawaona kwenye yahoo group na ofisini.
Ni ukweli usiopingika kuwa TYVA imepitisha kizazi na sasa umefikia wasaa kwa ajili ya kizai kingine ndani ya asasi yetu. Ni jambo la msingi kwani familia yetu ina haja ya kuwa Dynamic kama tunataka kuendelea. It is only by being so we will become progressive. TYVA ninayoifahamu mimi ni kama Dini, ni familia, ni jamii, ni kundi la watu wasio na uwezo mdogo wa kusimamia wanayoamini, watu wenye kuamini katika nguvu ya hoja na uhuru wa kila kundi jamii kujenga hoja ya utume wake na hivyo kuisimamia.
Naomba niruidie nukuu moja maarufu sana ndani ya TYVA kutoka kwa ndugu yetu Fanz Fannon. “Kila kizazi kina utume wake, hakina budi kuutekeleza au kuusaliti utume huu”. Ebu tujiulize: TYVA tuna utume? Je sisi TYVA ya sasa wote ni kizazi kimoja? Je, kama tuna zaidi ya kizazi kimoja, tuna zaidi ya utume mmoja? Naamini hii ndio hoja ya msingi kuliko zote ndani ya asasi yetu kwa sasa na kushindwa kwetu kutoa majibu maswali haya ndio kutaashiria kufa na kutoweka kweu kama jamii.
Naomba niibue tu hoja hiyo na niiachie hapo ili nitoe ukumbi kwa kila mmoja wetu apate nafasi katika kuchangia mjadala huu ambao ndio utaamua kufa au kuishi kwetu. Tafadhali tusiache mjadala huu utupite tu hivihivi.
Binafsi naamini TYVA imekufa lakini haijafa. Kama tutakufa tu na kuendelea na kufa kwetu tutaendelea kuwa kwenye vitabu vingi vya kumubkumbu na tutaweza kuwa maarufu kwa kiasi kikubwa tu. Hatutakuwa wa kwanza kufa na kama tunavofahamu kuwa mara nyingi marehemu anakuwa na sifa kebe kebe ukilinganisha na sisi wafu watarajiwa. Hatuna budi kutambua kuwa muda wote tunaoishi ni marehemu watarajiwa. Imani ya ndugu zangu wahindu ambao ni sehemu ya jamii ninamoishi kwa sasa wanaamini kuwa tumeumbwa in such a way tunapokufa tunapewa nafasi ya kuishi kuonesha zaidi mema tuliyoyatenda ili hali tulikuwa watenda wema wakati tunakufa. Naamini zipo dini nyingine kadhaa zinazoamini hivi. Binafsi ni muumini kiasi fulani wa dhana hii.
Ni wajibu wetu sasa kutambua kama tunahitaji kufa kwanza ili tupate nafasi nyingine ya maisha ndio tuweze kurudi pale tunapostahili.
Naomba nifafanue kwanini nasema TYVA ipo kwenye hali ya kifo. Kama nilivvokwisha tanabaisha hapo awali TYVA ni watu. Tukiingalia asasi yetu siamini tunayo rasilimali hii kwa kiwango kinachostahili. Ili asasi yetu iishi inahitaji kuliko jambo jingine lolote watu ambao ni wanachama na vingozi makini. Nikirejea maneno yangu wakati wa Action Planning “TYVA was no just meant for every young person, it was meant for Vijana makini ambao ndio watakaotumika kuwafikia vijana wote ambao wanahitaji kukombolewa kutoka kutoshirikishwa na kutopewa nafasi ya kutosha na jamii yetu”. Hivyo kama tunavoamini kwenye utume wetu (kama bado tunauamini) tutaweza tu kuwawezesha vijana wa kitanzania kama sisi wenyewe tutajenga na kuwekeza katika uwezo wa wanachama wetu
Hali ya sasa ya wanachama weu kwa maana ya idadi na uwezo ni mahututi hatuhitaji ubishi katika hili. Watu wanaofanya kila kitu ndani ya TYVA ni walewale. Hii ni hatari ambayo inaweza kuibua madaraja ya wanachama ndani ya asasi. Tukawa na wanachama wa daraja la kwanza wenye haki zaidi ndani ya TYVA na wanchama wa madaraja ya chini wasioweza hata kueleza utume wa TYVA ni nini. Watu wa namna hii huwa wanabaki tu kuwa kama waangaliaji wakati wenzao wakifaidi matunda ya kuwa wanaTYVA. Siku zote nimeamini na nimewaeleza wanaTYVA kuwa kama tutaitumia vizuri asasi yetu ina fursa kwa ajili yetu sote swala ni kuziona tu.
Tuna haja sasa kuwekeza katika wanachama wetu ili kazi ya viongozi isiwe tena kuwaonesha na kwatafutia wanachama fursa bali wanachama wawe ndio waendeshaji wakuu wa asasi na ndio wawaoeneshe viongozi hizo fursa. Leo hii inashangaza kuwa na wanachama ambao wanabaki wametutusa tu macho kwenye mkutano mkuu mpaka unajiuliza hivi hawa kweli wanasikia ninachosema?!!. Kusema ukweli, uzoefu wangu katika mkutano mkuu mwezi machi mwaka huu ulinisikitisha. Naamini kwa TYVA niliyokuwa naiona mimi kungeibuka mijadala mizito mizito wanachama wakiwabana viongoi wao wakitaka kufahamu kwa kina mustakabali wa asasi yao na ndiyo kazi yangu kama mwenyekiti wa mkutano ingeonekana. In the most unfortunate event ikawa kwamba mkutano ule ukawa mwepesi zikaibuliwa hoja nzito wanachama hawaelewi uzito wa hoja hizo wakabaki kushangaa wachache waliotoa mawazo yao na kuwapigia makofi. Mkutano ule ulikuwa mwepesi mno naweza kusema ni sawa na kikao cha baraza la wazee na askofu wa jimbo lao. Ushiriki wa wanchama katika mkutano ule ni kiashiria kikubwa cha ufu ndani ya TYVA.
Ukiacha suala la ushiriki mbovu wa wanachama linakuja swala la uwezo wa wanachama wenyewe. Jamani lazima tufikie hatua tukubali hatuwezi kubeba beba tu kila mtu ili mradi daftari letu la registry linajaa. Tunahitaji kuwa na Strategic Recruitment Mechanisms zitakazotuhakikishia kuwa kila mwanachma mpya tunaempata kuna kamchango anakuwa nacho kwamba kila mwanachama ni sawa na walau tofali au mchanga katika ujenzi wa nyumba yetu ya TYVA.
Katika hili la recruitment kuna mamabo mawili. Kwanza ni kutafuta wanacham wenye uwezo mkubwa. Pili ni kuhakikisha tunawekeza katika wanachama wetu. Nawapongeza wote wanaojihusisha na kajimradi ketu ka “school of TYVA” kwani kanaweza kutumika kama msingi mzuri wa kuwajenga hawa tunaowaita wanachama wetu. Hatuwezi kuafford at this stage kuwa na wanchama wasiojua hata mission statement ya asasi ni nini. Ndio hapa ambapo nchi nyingi za kiafrika tunapoendelewa kushindwa hadi hii leo. Ili mtu aweze kushiriki katika ujenzi wa jambo lolote ni muhimu mno kwanza akalifahamu na kulijua jambo lenyewe. Kama unataka watanzania wawe wazalendo kwa nchi yao ni lazima wakailelewa kwanza historia ya nchi yenyewe. Vivyo hivyo kama tunataka wanachama wazalendo na wanaoweza kweli kuwa na mchango kwa TYVA ni lazima twafundishe wanachama wetu historia yetu wakailelewa.
Sasa changamoto inakuja hiyo historia yetu yenyewe iko wapi?? Wote sisi tuna wajibu wa kuiandika historia yetu. Leo hii asasi nyingi za wenzetu zimekufa na sisi wenyewe tunaelekea huko kwa kuwa hatujaandika historia yetu. Tusipoiandika tutajikuta tunairudia kwani siku zote wanasema historia inajirudia pale tusipoifahamu. Sasa tujiulizie kama tutakaa kuirudia rudia tu historia yetu tutafika lini huko mbele tunapotaka kufika. Wamarekani waliliona hili siku nyingi, leo hii kijana wa kimarekani anasoma historia ya nchi hiyo throughout his or her academic career. Ningeshauri kwa sasa tukae chini wale wa kizazi kilichopita na sisi wapya tuandae maandishi ya historia yetu especially wakati huu tunapoelekea kutimiza miaka kumi. Hii itasaidia kupunguza pengo kati ya wale wanaonekana kuijua zaidi TYVA na wale wanaoshangaa shangaa hivyo wale wanaodhani wana haki zaidi kwa TYVA kwasababu ya kuijua watapunguziwa kiburi chao.
Si jambo jema wanachama wakaendelea kuhangaika kuijua tu historia ya TYVA.
Tunahitaji kuunda mifumo ambayo itatusaidia kuhakikisha wanachama wanaendelea kukuwa na kuifahamu na kuwa na mchango zaidi kwa TYVA kadiri wanavoendelea kuwa wanachama.
Much as TYVA inawahitaji wanachama wanachama wanaihitaji TYVA. Huu ni ukweli ambao sisi wanachama wote hatuna budi kuukubali na kuufanyia kazi. Kama nilivokwisha kutaja hapo juu hatuwezi kuwaachia viongozi jukumu la kutushirikisha kwa sababu mwisho wa siku viongozi wetu wanatokana na sisi wenyewe wanachama kwahiyo tukiwa wote na mtazamo wa namna hii tutajikuta wote tunabaki kuishangaa TYVA yetu. Tusipokuwa makini tutajikuta viongozi wetu wakitutumia na kujifaidisha wenyewe. Hatuna sababu ya kuwaamini viongozi kiasi hichi. Kama tutajenga tabia hii ya kuwaamini sana viongozi wetu tutaendelea kuelekea kifoni. Siamini kama TYVA inatakiwa iwe asasi rahisi kiasi hicho inakuwa haina raha ya kuiongoza. Huu ndio ujumbe wangu kwa kizazi kipya cha TYVA.
Nashukuru kwamba kuna dalili nzuri tu za kukijenga kizazi hiki. Tumewaona kwenye yahoo group, kwenye training na maeneo mengine vijana kadhaa wapya kina Sam na wenzake. Leo hii tutaposhindwa kuwekeza kwao tutaendelea kufa. Lazima tubadilishe mtazamo tutoke nje ya kaofisi ketu twende kutafuta wanachama wenye dalili hizi kwa juhudi zote kokote tunapoweza kuwapata. Changamoto inabaki kuwekeza katika uwezo wa kizazi hiki.
Ni jambo lililo wazi kuwa maendeleo ya TYVA yanategemea kwa kiasi kikubwa tena sana hali ya maendeleo ya wanachama wenyewe.
Dhana ya Uongozi ndani ya TYVA
Kwa namna nilivoifahamu TYVA kabla sijawa kiongozi wa asasi yetu sikutarajia kazi ya kuongoza asasi hii ingekuwa nyepesi hata kidogo.
Sina budi kukubali kuwa tuna utaratibu mbovu wa kupata viongozi wetu. Utaratibu hata ulioniingiza mimi binafsi uongozini una udhaifu mkubwa. Naamini na mimi ningekuwa mvivu kaitka kujifunza kuhusu asasi yetu si ajabu ingefia mikononi mwangu.
Katika taasisi zote kubwa na madhubuti duniani kunakuwa na utaratibu ambao unajenga na kuhakikisha kuna namna mahsusi ya kuupata uongozi wake. Utaratibu wa kuchagua viongozi wetu out of desperation una athari kubwa sana kwenye uendeshaji wa asasi yetu.
Tunayaona yanayotokea leo kwenye moja ya vyama vikubwa kabisa vya siasa nchini kwetu. Leo hii chama hiki naweza kusema kimeparanganyika kwa sababu ya kuikana mifumo iliyokuwepo na kufungua milango yake kiholela. Wahenga walisema ukifungua milango ili kupata hewa safi unaweza kukuta mapaka mbu na kunguni wakiingia. Utaratibu huu ndio umefanya chama hiki kiyumbe baada ya kunguni kujaa kwenye mwili wake.
Sasa tujiulize hiki ni moja ya vyama vikubwa kabisa na kilikuwa na mifumo yenye misingi madhubuti lakini bado kikaweza kushambuliwa na kunguni. Sembuse sisi ambao mpaka hivi sasa hatuna hata hiyo mifumo ya namna hiyo.
Kama nilivoeleza hapo awali kama tutafanikiwa kufanya ile strategic recruitment ni dhahiri kuwa tutakuwa tunatengeneza viongozi imara bila wasiwasi. Inatakiwa tufikie hatua tuje kwenye uchaguzi tuna watu wewngi wenye uwezo wa kuwa viongozi si tufike kwenye uchaguzi tuanze kutafuta watu wanaoweza kuwa viongozi wetu. Wanachama wanaweza kuwa na mchango mkubwa in this direction kwani wao ndio wanawachagua viongozi. Sio tunakaa tu kwenye mkutano tunasikiliza irrational statements watu wanatulilia lilia tu tunaamua kuwapa kura zetu out of sentiments. Hizi si busara hata kidogo.
“Mnafanya vikao hamniambii, mnafanya training hamnishirikishi kwa kuwa wewe ndiyo mwenyewe TYVA, ama sio? Halafu nisikie mnaniambia kitu”. Nimeamua kuyanukuu maneno haya ya kiongozi mmoja wa TYVA ambaye alinitumia ujumbe mfupi wa maneno kwenye simu yangu ya kiganjani kama wiki moja kabla siajondoka. Kwanza namsikitika kiongozi huyu kwani inaonekana alikuwa hata hafahamu mimi kwa kipindi hiko sikuwa kiongozi wa TYVA ni dalili ya umbali wake na asasi. Pili in any case siamini mi nilikuwa mtu ninayehusika na yeyote kati ya training wala vikao vya excom hizo ni kazi za katibu na TCB. Tatu inasikitisha kiongozi mkubwa wa TYVA analilia training sasa kina Pamela wangeenda lini. Kiongozi huyu hafahamu hata jambo la muhimu kwamba ni busara zaidi kuwaachia wanachama kupata fursa hizi na katika training ile ya Girraffe ilikubalika kimsingi viongozi wasiwepo na wanachama wapewe nafasi zaidi. Mbaya zaidi huyu ni kiongozi anayefahamika kuwa amehudhuria training nyigi tu za TYVA ndani na nje ya nchi kwa zaidi ya miaka mine. Huu ni ufisadi tunaohitaji kuushugulikia haraka sana.
Kwakweli sikufurahia ujumbe huu na niliona busara kumtaarifu katibu mkuu only to realize na yeye alikuwa amepata exactly the same message. Kiongozi huyu hayupo peke yake na tusipozishughulikia haraka elements za namna hii tukendelea kuiua asasi yetu.
Hatahivo naamini wanachama wanahitaji kulaumiwa katika hili kwani tumekuwa wapole mno kwa viongozi wetu. Siamini kama wanastahili ukarimu huu. Lazima tuwe wakali tuchukie tabia zote wanazoweza kuwa nazo viongozi wetu ambazo zitatukwamisha. Kama sasa tunaona mambo yanaenda mrama hatuna budi sasa kuandaa na kuongoza mapinduzi yenye kulenga kuboresha hali ya mambo.
Wale ndugu zangu tuliokuwa Girraffe tunazungumza ile hadithti ya ukweli kuhusu mapinduzi ya Anatoglu watakumbuka mapinduzi hayo yamekuwa na mchango mkubwa mno kwa asasi yetu. Hatuna budi kuangalia namna gani sasa tutawashughulikia viongozi wote waliokuwa mzigo kwetu pamoja na mifumo yote ambayo inatukwamisha hivi sasa kusonga mbele. Binafsi mimi ni muumini wa mapinduzi na huwa naamini katika uwezo wa mapinduzi kuleta maendeleo. Tuisome leo katiba yetu tuwafuatilie viongozi wetu na kila jambo linalotukwamisha.
Leo hii nchi zote zinazotmba kuwa imara na zenye demokrasia imara zilijengwa kutokana na mapinduzi. Ndugu zetu wafaransa walimkata kichwa mfalme wao, waingereza walimkimbiza mbali mfalme na kumpa masharti pale walipoamua kurudisha hadhi ya ufalme ndani ya nchi yao. Wamarekani wenyewe wamepigana vita miaka mingi tu ndio wakaipata nchi yao.
Tunafahamu jinsi asasi za wenzetu zilipojikuta pabaya kwasababu ya uongozi mbovu na wanachama dhaifu. Inafikia hatua viongozi wanapitisha tu miaka bila hata kufanya mkutano mkuu. Hatuwezi kukubali TYVA ika “one man show”. Tutawapa sana kiburi viongozi wetu kama tutawaachia wafanye kila kitu kwasababu kama tunavofahamu haki hutokana na wajibu hivobasi tukiwaacha badhi yetu “wakawajibika” zaidi basi ni swala la wazi watapata haki zaidi na asasi yetu itazidi kumomonyoka.
Tunahitaji sasa kutengeneza a “modus operandi” itakayotusaidia kupata the best of the best kuiongoza asasi yetu. Tusianguke kwenye udhaifu wa nchi zetu nyingi zinazoendelea. Ukifuatilia historia ya marekani utagundua unahitaji sana kwa na kipaji cha ziada kuongoza nchi ile hata nchi nyingine nyingi zilizoendelea. Huu si wakati wa kuacha tukaongozwa na mambumbumbu.
Kizazi kipya ndani ya TYVA
Matumaini ya asasi yetu kuepukana na kifo yanategemea kwa kiasi kikubwa uhai wa kizazi kipya cha TYVA – TYVA chipolopolo.
Ni wajibu wa vizazi vilivyopita kuangalia na kuona ni namna gani vinaweza kuchangia katika kukuza kizazi kipya.
Kushindwa kwetu kuivunganisha vizazi hivi ndio kunasababisha hali iliyokuwepo hivi sasa. Kama nilivosema kwenye mkutano mkuu tuna haja ya kuredefine our rason d’etre, our values that have kept us moving and the principles upon which our association is built. Tunahitahitaji intergenerationa mingling ili kuweza kufanikiwa katika hili. Leo hii kina Diana Kamara wamjue Baruani ni ni ndio tutaweza kwenda.
Kinachotokea sasa ni kizazi kipya ambacho hakika hakijawa full blown na upande mwingine tuna kizazi kingine abacho kinaonekana kuwa mbali na asasi. Nakumbuka kumshirikisha ndugu yangu Welwel kwamba labda tuna haja ya kuunda “Dira – Social Club” kama mkakati wa kuwaretain wanachama wetu ambo inasemekana wanaelekea kwenye greener pastures. Si ajabu kamkakati ka namna hii katatusaidia kuwaonganisha ndugu zetu ambao katika wakati huo walikuwa wameonganishwa kwa karibu na asasi lakini wanaonekana kuwa mbali zaidi baada ya kuachana na asasi. Mkakati wa namna hii unaweza hata kuwasaidia kushirikishana fursa nyingi ambazo wanakuwa nazo. Si mbaya kama watoto waliotokana na mama mmoja TYVA kuendelea kuishi kifamilia baada ya kuachana na asasi. Naamini ni jambo jema kama tutakuwa na utaratibu ambao utawakutanisha ndugu zetu hawa walau mara moja kwa mwezi. Wote tunakumbuka kuwa TYVA ilianza kwa kusherekea birthday za watu safari hii tuna nafasi nzuri ya kuendelea kusherekea harusi za watu, sherehe za kuzaliwa watoto zao na kadhalika katika spirit ile ile ya TYVA.
Ili TYVA iweze kuendelea ni lazima wakubwa wetu hawa wakubali kuwa wana wajibu kwa TYVA. Kama ilivo kwa wanachma wote tuna wajibu wa kuhakikisha TYVA haifi.
Ni wajibu wa viongozi wetu sasa kuunda mifumo ambayo itahakikisha tunaleta pamoja vizazi vyote vya TYVA kwa ajili ya kutafakari na kuujadili upya mustakabali wetu hasa wakati huu tunapoelekea kwenye mchakato wa kuunda mpango mkakati mpya wa miaka mitano.
Tuchambue sasa ni yapi kulingana kizazi kilichopo ndiyo yanaweza kweli kutufikisha tunapodhania tunataka kuelekea. Kushindwa kwetu sote kutimiza wajibu huu ndio kutaamua kufa au kutokufa kwa asasi yetu.
Kizazi kilichopita kilifanya mengi katika asasi yetu naamini itakuwa aibu kwao kukuta TYVA imebaki masizi. Ni wajibu wa wanachama wote kujitambua sasa ni kizazi gani tunachotokea kwa nia nzuri ya kuhakikisha tunaweza kushiriki kikamilifu katika ujenzi mpya wa TYVA. Tusitumie vizazi hivi kujigawa bali viwe chanzo vya mahusiano imara zaidi ndani ya familia yetu.
Hitimisho
Ujumbe wangu huu wa leo ni mada ndogo tu ninayopenda kuwasilisha ili kuibua mjadala mpana zaidi utaotusaidia kujitambua kama asasi na hivo basi kuweza kutengeneza njia bora za mafanikio.
Hivi sasa tupo katika kipindi mahususi sana tukielekea katika kutengeneza mpango mkakati wa pili wa asasi yetu. Tusibweteke tusijichukulie wadogo wala tusijione wakubwa sana. Let us rediscover our rason d’etre let us spearhead the renaissance of TYVA.
Ningeshauri kila mmoja wetu katika nafasi yake asikubali kupitwa na mjadala huu muhimu.
Tuipende TYVA, tupendane ndani ya TYVA ili TYVA iweze kurudisha mapenzi kwetu.
Wakati tunafanya yote haya tukumbuke TYVA ni njia amabyo wote tukiipita vizuri itatufikisha mbali tusipende kupitia vichochoro vyenye makorongo wakati barabara ya lami ipo.
Tukumbuke TYVA ni dini, kushindwa kwetu kuifundisha dini yetu vizuri hasa kwa vizazi vinavyotufuata kunadhoofisha asasi yetu. Ebu tujifunze kwa wakatoliki, waislamu na madhehebu mengine yaliyobaki imara mpaka leo kwa kuweza tu kusimaia values zao na kuhakikisha wafuasi wanapata mafunzo kamili juu ya dini yao. Dini yetu ni changa sana ukilingainisha na dini hizi kubwa, Je sisi tunafanya nini katika hili??
Nilikuja TYVA nikapita sina uhakika nitarudi lakini naamini nitaendelea kuwa mwanafamilia mwaminifu katika familia hii tajiri.
Natutakia wote kila kheri katika mjadala huu na michakato yote itakayotokana na mjadala huu.
Our lives begin to end, when we remain silent about things that matter,
It is better off dying with living thoughts than living with dead thoughts: Che Guevara
Aluta Continua!!!!

Deus R. Valentine,
Loyola College (Autonomous),
Madras University,
Chennai 600 034,
51 Sterling Road,
Nungambakkam,
Chennai,
Tamil Nadu,
South India,
India.
Cell: +91 984 05 43 985
Email: deusrweye@yahoo.com
 
Back
Top Bottom