Dira ya Mtanzania: Siri yavuja, Migiro kuwa Waziri Mkuu...!

Kwa kuwa suala hili ni la kikatiba ebu tusome Ibara husika za Katiba yetu. Kwanza tuitazame Ibara ya 51(2) ya Katiba ya JMT:
"Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio wengi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge walio wengi."
Na pia tuisome hapa Ibara ya 51(3)(d):
"Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, Waziri Mkuu atashika kiti cha Waziri Mkuu hadi-
(a) N/A
(b) N/A
(c)N/A
(d) siku Rais atakapomteua Mbunge mwingine kuwa Waziri Mkuu;...".
Je, Katiba inamruhusu Rais kumteua Mbunge wa kuteuliwa kushika madaraka ya Waziri Mkuu?
 
Jamani hepu tujiuliza swali hivi sisi wote tuliochagua wabunge kupitia chama chetu tawala tulikosea kuwachagua au? Kwani wabunge hawa wanaonekana uwezo wao wauongi mwisho wake ni ubunge tu hawafai kuwa mawaziri kwani sasa kila kunapokuwa na hali ya kubadilisha baraza lazima chama chetu kiteue watu wengine kutoka nje ya bunge ikimaanisha kuwa hawa waliopo ndani ya bunge hawafai kushika nafasi hizo wao chao ni ubunge basi! Hebu sisi wenye wabunge wa chama tawala na hata siku moja hatujawa na wazo lakupata mbuke waziri tulibugi wapi? Na hebu tuwaulize wanamatatizo gani moaka chama kinashindwa kuwaamini kwa nafasi zao mpaka kiteue watu kutoka nje ya bunge ndiyo wapewe uwaziri? Naomba kuwasilisha
 
gazeti kanjanja kwa sababu ibara ya 51 (2) iko wazi kuhusu waziri mkuu kuwa mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika jimbo la uchaguzi.
 
Yule mama ni sawa na Pinda tu, wote hawatoshi hata kuwa manaibu waziri..
 
Nimeisikia taarifa hii asubuhi hii kupitia uchambuzi wa magazeti Star Tv.

Habari hii imeandikwa na gazeti la Dira.

Hivi karibuni rais Kikwete alimteua Asharose Migiro kuwa mbunge, uteuzi huu umeibua mijadala na tabiri za kila aina, wengine wakisema lengo ni kumrudisha wizara ya mambo ya nje au wizara yoyote kati ya zinazoonekana kuyumnba hivi sasa. Lakini habari niliyoisikia ya gazeti la dira ndiyo imenishangaza na kujikuta nikijiuliza maswa lukuki kuhusu uwezo wa gazeti hili katika kufuatilia, na kuhakiki habari.

Moja kati ya sifa za Waziri Mkuu ni kuwa awe mbunge wa kuchaguliwa jimboni (hata kama alipita bila kupingwa). Ina maana hawa waandishi wa Dira na wahariri wao hawalifahamu hili?

Uandishi ni taaluma nyeti sana hivyo naomba acheni uvivu wa kufuatilia mambo na kufanya references kwa lengo la kuandika habari zisizo na mashaka kwa maslahi mapana ya jamii. Mnafanya idadi ya wasomaji wa magazeti kupungua kutokana na tabia yenu hiyo isiyo na misingi ya kitaaluma ya kuandika hisia badala ya uhalisia.

Nawasilisha.

Hawezi kuwawaziri mkuu. Katiba yetu inamtaka rais amteue waziri mkuu kutoka wabunge wa kuchaguliwa.
 
Weka Ibara ya Katiba inayosema.kuwa kazima awe ni mbunge wa kutoka Jimboni. Acha Upotoshaji unakurupuka asubuh asubuh bila kupiga Mswaki na domo linanuka unakuja kuweka hoja isiyo na Ushahdi .Madhara ya kusoma Vyuo vya K koo(Green College)
Ni kweli nimesomea Kariakoo, unadhani hilo linanifanya niwe chini yako kiufahamu? wewe utakuwa ni huy mwandihi au aina hiyo ya waandishi, ina maana hujui kuwa its the content that counts?
Mdomo na kunuka kwake ni maumbile tu, lakini hapa sisi tunajadili fikra na ufahamu au ulidhani kuwa tupo kwenye jukwaa la urembo?
 
If this happens will our party (Chadema) have the moral authority to criticize the ruling party (CCM) as our leaders doing the same ----?Just asking!
 
Nimeisikia taarifa hii asubuhi hii kupitia uchambuzi wa magazeti Star Tv.

Habari hii imeandikwa na gazeti la Dira.

Hivi karibuni rais Kikwete alimteua Asharose Migiro kuwa mbunge, uteuzi huu umeibua mijadala na tabiri za kila aina, wengine wakisema lengo ni kumrudisha wizara ya mambo ya nje au wizara yoyote kati ya zinazoonekana kuyumnba hivi sasa. Lakini habari niliyoisikia ya gazeti la dira ndiyo imenishangaza na kujikuta nikijiuliza maswa lukuki kuhusu uwezo wa gazeti hili katika kufuatilia, na kuhakiki habari.

Moja kati ya sifa za Waziri Mkuu ni kuwa awe mbunge wa kuchaguliwa jimboni (hata kama alipita bila kupingwa). Ina maana hawa waandishi wa Dira na wahariri wao hawalifahamu hili?

Uandishi ni taaluma nyeti sana hivyo naomba acheni uvivu wa kufuatilia mambo na kufanya references kwa lengo la kuandika habari zisizo na mashaka kwa maslahi mapana ya jamii. Mnafanya idadi ya wasomaji wa magazeti kupungua kutokana na tabia yenu hiyo isiyo na misingi ya kitaaluma ya kuandika hisia badala ya uhalisia.

Nawasilisha.
MKUU usishangae, huenda MKUU wa KAYA naye haelewi katiba. Ni mara kadhaa amekwenda kinyume
 
Sioni lolote jipya kwa huyu mama mpaka wahangaike nae kiasi hicho.mbona yapo majembe kama Magufuli,Mwakyembe mbona hayaoni?
 
ili kudhihirisha kuwa ccm ni chama cha ki islam kama hisbulah au taliban lazma nafasi zote za juu wapewe waislam
 
weka ibara ya katiba inayosema.kuwa kazima awe ni mbunge wa kutoka jimboni. Acha upotoshaji unakurupuka asubuh asubuh bila kupiga mswaki na domo linanuka unakuja kuweka hoja isiyo na ushahdi .madhara ya kusoma vyuo vya k koo(green college)

hivi unajua kinachoendelea kweli????????????????????????????????????
 
Ni kweli nimesomea Kariakoo, unadhani hilo linanifanya niwe chini yako kiufahamu? wewe utakuwa ni huy mwandihi au aina hiyo ya waandishi, ina maana hujui kuwa its the content that counts?
Mdomo na kunuka kwake ni maumbile tu, lakini hapa sisi tunajadili fikra na ufahamu au ulidhani kuwa tupo kwenye jukwaa la urembo?

ACHANA NA HUYU masakapwela,,hajasoma thread yote,,alafu anakurupuka ku coment,,hajui kinachoendelea hata kidogo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom