Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,531
Pamoja na kuwa hoja hii kutoka kwa mdau mmoja mtaalamu wa elimu imekaa kimazingira ya kielimu elimu, nafikiri tukiwa bado tunapekenyua ile hoja ya "Ndivyo Tulivyo" kuna haja ya kuulizana kama Mwalimu huyu anavyouliza.
Je Dira ya Elimu yetu ni vipi?
Napenda kumnukuu Mwalimu Selina Mushi
Je Dira ya Elimu yetu ni vipi?
Napenda kumnukuu Mwalimu Selina Mushi
Walimu wenzangu,
Nina swali ambalo limenitatiza kwa muda mrefu sasa, na pengine niliwahi kulidokeza. Na ninaposema walimu sina maana wale walioko darasani tu ila wote tunajikuta tunafundisha kwa namna moja au nyingine kama wazazi, marafiki, dada mkubwa, kaka mkubwa, mwalimu wa dini, nk.
Hili swala ni la kitaalamu kidogo lakini nitalirahisisha na kuliweka katika maisha ya kila siku. Swala lenyewe ni falsafa ya elimu nchini Tanzania. Nini falsafa ya elimu nchini mwetu sasa hivi? Nini muono wa elimu yote nchini ambao unaongoza mission ya elimu katika nchi yetu kwa kipindi kama cha miaka 15 au zaidi iliyopota?
Kwanini nauliza hili swali:
- Ufundishaji katika ngazi zote (pre-school hadi chuo kikuu) unahitaji mwongozo. Mtoto anapokwenda shule akiwa mdogo kabisa, anaanza kwa kupewa dira ya elimu yake anajua kuwa elimu yake inamtaka aelekee wapi. Akifika madarasa ya juu kidogo anaanza kuwa na uwezo wa ku abstract na kuanza ku-reason kuhusu mwelekeo wa elimu. Akifika chuo kikuu ana-question hiyo philosophy na mijadala kama hio inakuwa chachu ya kuendeleza falsafa ya elimu kulingana na mwelekeo wa nchi.
- Kila mara nilipodokeza hili swali, nilijibiwa kwa haraka haraka kuwa naitamani sana ile elimu ya kujitegemea ambayo ilikuwa katika misingi ya siasa ya ujamaa na kujitegemea. Hivyo ndivyo watu wasivipenda kufikiri kwa undani na kujibu kwa haraka haraka kwa kutizama kitu juu juu tu. Naomba tuende beyond siasa ya ujamaa hapa. Haturudi nyuma. Siasa ya ujamaa haipo tena na wala sizungumzii hiyo. Nazungumzia mweleko wa elimu what is the guiding philosophy?
- Tuangalie jinsi Tanzania inavyoyumbishwa na wenye pesa wanaonunua machimbo ya madini, mbuga za wanyama, ardhi za wanavijiji! Angalia wataalamu tunaoletewa wa mvua, madini, kilimo, elimu, afya nk.
- SWALI: Mtoto wa kitanzania aandaliwe vipi tangu akiwa mdogo ili awe na dira imara katika elimu yake, ajenge tabia yake katika misingi hiyo, awe na miiko ambayo anajua kabisa elimu yake imemkataza kuvunja miiko hiyo, ajue kuwa taifa lake linamtegemea katika kutimiza wajibu wake wa kulijenga taifa kwa namna fulani?
- Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Ikiwa watoto hawataonyeshwa kuwa kila mmoja wao ana wajibu fulani wa kutimiza ili nchi isiporomoke, hawataelewa kuwa vitendo vya mtu mmoja kama kusaini mkataba muhimu, kama kutofualitia vitendo vya ufisadi, kama kufumbia macho wizi wa kodi za wananchi, kama kuwaruhusu Sheraton kuwa Royal Palm, kuwa Movenpik ili wasilipe kodi, kama kuwaleta wataalamu uchwara nchini, kama kuanzisha kampuni hewa nk. kunaweza kuporomosha juhudi za nchi nzima si kiuchumi tu bali pia kisiasa. It defies logic to see that individuals think their corruptive actions WILL NOT affect the stability of the nation!! Nadhani dhaa hii inahitajika ifundishwe tangu kindergarten. Na kwa hiyo kuna haja ya kuwepo dira ya elimu yetu. Elimu yetu inalenga nini? Sasa hivi sekta zote za elimu zimeunganishwa katika wizara moja na itakuwa rahisi zaidi kuiweka hiyo dira ya elimu kitaifa ieleweke.
- Tulikotoka:
- Dira ya elimu ya mkoloni ilikuwa kupata wataalamu wachache wa kuitumikiwa serikali ya uingereza
- Dira ya elimu baada ya uhuru ilikuwa elimu ya kujitegemea iliyotokana na siasa ya ujamaa na kujitegemea ili wananchi wapate wlimu ya kuwawezesha kujitegemea kama nchi na binafsi pia.
- Dira ya elimu ya sasa ni nini?
Hasara za kutokuwa na Dira ya Elimu Nchini:
- Everything goes - hakuna mwelekeo wala makubaliano kuwa elimu inalenga nini
- Haijulikani kwanini vitu fulani fulani vinafundishwa au havifundishiwi mashuleni
- Nikianza shule yangu alimradi nafuata general guildelines za wizara I can teach anything hata corruption!
Nadhani swali langu limeeleweka. Nitashukuru sana tukiendelea kuchangia hoja hii.
- Mnaonaje Dira hizi?
- Elimu ya ubepari
- Elimu tegemezi kwa nchi za nje
- Elimu ya kuiga tamaduni za nchi za magharibi
- Elimu ya kuimarisha kunyonywa
- Elimu ya kujitajirisha binafsi na kuliua taifa
- Elimu ya corruption
- Elimu holela Liwalo na Liwe
- Mnaonaje Dira hizi hapa?
- Elimu ya kujikwamua kiuchumi na kujiimarisha kisiasa
- Education for effective global competition
- Mtanzania kwanza: Elimu ya kunufaisha taifa la Tanznaia
- Elimu ya kumwimarisha Mtanzania kiuchumi na kisiasa
- Elimu ya Utu na kuimarika kiuchumi na kisiasa
- Elimu ya Utu, kushindana kiuchumi na kuimarika kisiasa duniani
- nk
Manufaa ya Dira ya Elimu Nchini:
- Hutoa mwelekeo mzima wa elimu nchini
- Hujenga msingi imara wa elimu nchini inaeleweka elimuyetu inalenga nini
- Informs Mission Statements for institutions without mission statements institutions will function haphazardly
- Informs curriculum goals, planning, and materials development
- Informs training of teachers (teacher education programs)
- Informs educational assessment and evaluation (large scale and small scale assessment and evaluation practices)
- Provides direction and forum for further refinement of educational efforts given assessment feedback
Selina