Dira Na Utume

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
Kwa siku kadhaa nilikuwa nimetoweka hapa JF. Kabla ya kutoweka nilishiriki mjadala mrefu kwenye FOCUS 2010 na CHADEMA must reform. Mara baada yake ukazuka mjadala wa Kabwe Vs Wangwe- Kisa cha Mafahali wawili ambao nao umechangiwa na kwa kiasi cha kutosha na naamini ujumbe umefika kwa wahusika.

Baadaye kidogo ukazuka mjadala wa matokeo ya uchaguzi Kenya mintaarafu uchaguzi wa 2010 kwa Tanzania. Katikati ya mjadala huo, kumezuka hoja ya kuiondoa CCM madarakani- lakini swali la ziada limezuka- kwa ajili gani? Nini kifuate baada ya kuitoa CCM madarakani?

Swali hili ni la muhimu sana linalohitaji mjadala wa peke yake. Nafahamu kila chama cha siasa kina dira, malengo na mwelekeo wake ambao umefafanuliwa vizuri katika falsafa, itikadi, na ilani yake.

Lakini swali ambalo ni vyema tukajadili, na hili ni la wananchi wote kwa ujumla bila kujali itikadi. Nini iwe Dira(vision) na utume (mission)- au tunaweza kusema Kauli Mbiu (hapa kuna kazi ya kutofautisha na Slogan) ya chama ama ushirikiano wa vyama ambavyo kwa kuwa nayo wananchi wawe na imani na utayari wa kuwakabidhi mamlaka ya kuongoza dola mwaka 2010 kama mkataba katika ya umma na viongozi watakaochaguliwa?

Kwa mfano; chama cha Democrat cha Marekani:

The Democratic Vision
The Democratic Party is committed to keeping our nation safe and expanding opportunity for every American. That commitment is reflected in an agenda that emphasizes the security of our nation, strong economic growth, affordable health care for all Americans, retirement security, honest government, and civil rights.

Guiding Principles
Our Plan
We have a bold new direction for a secure America. We seek: 1) Honest Leadership & Open Government, 2) Real Security, 3) Energy Independence, 4) Economic Prosperity & Educational Excellence, 5) A Healthcare System that Works for Everyone, and 6) Retirement Security.

Mjadala huu ni muhimu kwa kuwa naamini kabisa ushirikiano wa vyama kama wa CHADEMA, CUF, TLP na NCCR Mageuzi unapaswa kusikiliza matakwa ya umma kwa kiasi kikubwa. Swali hili ni muhimu kwa kuwa linaweza kutoka na ajenda za msingi za uchaguzi wa mwaka 2010.

Na ni vyema dira na utume huo ukawa katika sentensi chache ambazo zinaweza kukumbukwa kwa urahisi na ujumbe kusambazwa kwa urahisi nchi nzima na kuwafikia wananchi mpaka wa ngazi ya chini kabisa.

Mjadala huu ni kwa yoyote ambaye ana Tanzania anayoitaka ambayo anaona bado utawala uliopo haujaweza kuileta. Kama Mahatma Ghandi alivyowahi kusema, "kuwa wakala wa mabadiliko unayotaka kuyaona. Kijua ndio hiki, tusipouanika, tutautwanga mbichi!"

JJ
 
Blah blah blah blah Watu wana njaa ya mabadiliko wewe unaleta theories za vision mision kwani tuko shule hapa.Watu washike silaha waingie mitaani,hiyo ndio sulihisho.
 
Mheshimiwa sana Sozi D. Nabora,
Karibu sana, sasa baada ya kushika silaha na kuingia mtaani nini kifuate kwa maoni yako? Au ndio mambo ya tutajua hukohuko...
 
Huyu myika na siasa za kitoto vipi!

Kaka Eddy

Asante

Mwaga basi hizo siasa za kikubwa ili zitukuze sisi 'watoto'.

kwa maoni yangu huu mjadala ni muhimu kwa sababu kadhaa:

Mosi, CCM imekuwa ikipita na kusema kwamba 'wapinzani hawana sera'. Na wako baadhi ya watu wanaamini kabisa huo uzushi! Namna pekee ya kuondoa uzushi huo ni kuweka sera bayana.

Pili, Baadhi ya watu wamekuwa na hisia kwamba upinzani hauwakilishi matakwa ya wananchi, kazi yake ni kulalamika tu na kukosoa. Mjadala huu utawezesha kujua hayo matakwa ya wananchi ni yapi? Je, kwa upinzani ulivyo sasa umebeba matakwa hayo? Kama si kwa ukamilifu wake, ni mambo gani ya kuzingatiwa?

Tatu; utafiti wa REDET wa hivi karibuni, (Pamoja nakuwa sikubaliani nao kwa kuweka vyama vyote pamoja na kuita tu upinzani badala ya kufanya hivyo lakini pia kutafuta maoni ya wananchi kuhusu ushirikiano wa vyama na pia chama kimoja kimoja katika vyama vyenye uwakilishi kwenye vyombo vikuu vya maamuzi), umesema kwamba katika kipindi cha mwaka mzima uliopita- imani ya wananchi kwa vyama vya upinzani imekuwa kwa 0.8%(soma asilimia sifuri nukta nane) tu! Na sababu za wananchi kutokuwa na imani na upinzani zimetajwa kuwa ni MIGOGORO(kama sababu ya kwanza) na KUKOSA SERA(kama sababu ya pili). Mjadala huu ni muhimu kwa kuwa unashughulikia sababu ya pili iliyotajwa na wananchi. (ingawa ingawa naamini kama utafiti ungehusisha pia maoni ya wananchi kuhusu chama kimoja kimoja matokeo yangekuwa tofauti kwa kiasi kikubwa baina ya vyama).

Samahani kama mjadala unaonekana kuwa academic, nia yangu ni kuwa na mjadala political tu hapa- na kupata maoni ya umma kuhusu NINI IWE AJENDA YA CHAMA AMA USHIRIKIANO WA VYAMA AMBAO UTAPEWA MAMLAKA YA KUONGOZA DOLA MWAKA 2010?.

Huko Kenya- sababu za kushindwa kwa Kibaki pamoja na majigambo yake ya kukuza uchumi zimeelezwa kuwa ni kushindwa kupambana na ufisadi mkubwa, kushindwa kuleta katiba mpya, kushindwa kuweka mazingira mazuri ya ajira hususani kwa vijana, nepotism(yenye sura ya kupendelea kabila lake) na kwa ujumla kushindwa kutimiza ahadi nyingi alizozitoa.

Hapa Tanzania- kwa mujibu wa utafiti wa REDET na hata mijadala inayoendelea hapa JF wananchi wengi wamepoteza imani na JK na CCM kwa sababu zinazoshabihiana na hizo hizo za Kibaki- Kushindwa kupambana na ufisadi mkubwa, kushindwa kuweka mazingira ya maisha bora na ajira kwa vijana, nepotism(yenye sura ya serikali kujaa maswahiba wa Kikwete na wanamtandao maslahi) na kwa ujumla kushindwa kutimiza ahadi nyingi zilizotolewa wakati wa uchaguzi na hata katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.

Sasa kama JK na CCM ni wakuondoka- nini chama mbadala ama serikali mbadala isimamie?inafanye? Ndio nia ya mjadala huu.

Tuendelee

JJ
 
Blah blah blah blah Watu wana njaa ya mabadiliko wewe unaleta theories za vision mision kwani tuko shule hapa.Watu washike silaha waingie mitaani,hiyo ndio sulihisho.

Sozi

Nashukuru

Watu wana njaa ya mabadiliko gani?

Watu washike silaha kuingia mitaani kufanya nini?

Suluhisho gani?


Tusipokuwa na lengo, njia yoyote inaweza kutupeleka popote ambayo ndio sifa kuu ya siasa za blah blah blah blah blah ama kutupeleka kwenye siasa za hasira ya kumwaga damu ambayo ni sifa kuu ya siasa za balaa balala balaa!(Mzaha)

JJ
 
Zifuatazo ni baadhi tu ya nukuu za watafuatao dira, utume na mwelekeo


“Kitila, Kikwete bado hajasukumizwa vya kutosha. Pia naamini tatizo siyo kuungana wala kushirikiana na muungano wenye lengo la kuiondoa CCM madarakani unamsingi mbovu kwani baada ya kuiondoa CCM madarakani what next? Yaliyotokea Kenya ndio haya ya kutaka kuiondoa KANU na baadaye walipopata nchi wapinzani wenyewe wakameguka.

Na anayefikiria kuwa Raila ndiye ataiunganisha Kenya na kuleta yale matumaini naye anaweza kujikuta na matatizo kwani baada ya miaka mitano (assuming ndiye mshindi) wa Kenya watajikuta wana matatizo yale yale na watatamani Kibaki arudi n.k !

Kuungana msingi wake usiwe kuingoa CCM bali matokeo yake yawe ni CCM kuanguka! Tafuteni msingi wa kuungana uwe ni nini?”

(Mzee Mwanakijiji)

Msingi wa kuungana ni kukusanya nguvu na kuiondoa CCM. Kuiondoa CCM madarakani ni kuondoa mafisadi na wezi waliotapakaa ktk kila kila sehemu ya serikali. Kuiondoa CCM kutaipa fundisho kuwa Watanzania sio wajinga na wamechoshwa na mashenanigans yao na wanataka timu na safu mpya ya uongozi ulio bora na unaojali maslahi ya taifa kwa ujumla na si matumbo yao. Hopefully CCM itakaa chini na kuona wapi walichemsha, kufix kasoro walizonazo, na kukaa mkao wa kula just in case hiyo timu mpya nayo inachemsha.

(Nyani Ngabu)

“Mwanakijiji: CCM is itself a problem which is in turn a source of so many other problems troubling our country. Kwa hiyo kuitoa CCM tu already ni achievement. Unajua ukiwa unaumwa na umeshambuliwa na wadudu wanaosababisha huo ugonjwa unachotaka kwanza ni hao wadudu wafe/watoke, na unajua kabisa kwamba hao wadudu wakitoka utakuwa umepona, na ukipona maanake utaendelea na shughuli zako kama kawaida. Kwa hiyo tatizo letu la kwanza hapa ni CCM kuwa kikwazo cha sisi kufanya kazi zetu za kawaida za kujiletea maendeleo kwa wao ku-diverge attention yetu-matokeo yake hatuwezi kusoma, kulima, kufanya kazi vizuri maofisini, n.k. kwa sababu tumenyong'onyeshwa na huyu kirusi CCM. Kwa hiyo mzee wangu kumtoa CCM itafungua milango kwa mambo mengine mengi sana.

That said, nimeshasema hapa siku za nyuma kwamba tatizo la nchi yetu/zetu sio kukosa sera au ajenda; ajenda zipo tu sio za kutafuta: kujenga mabarabara,kumaliza njaa, kutokomeza maradhi yanayozuilika (malaria, etc) etc etc. Hata ukamwake mwanafunzi wa drs la 7 kuwa rais wa nchi lazima afanye haya kama ana uwezo na commitment. Ugomvi wetu na CCM ni kwamba wamepoteza uwezo na committment ya kuyafanya mambo ya kijamii. Kazi yao imebaki kupeana zamu ya kuongoza ili wachuna mali kisha waporomoshe majumba milimani kama alivyofanya kakako Mkapa”

(Kitila Mkumbo)

“Sasa JF hatuwezi kukaa tu hap kupiga domo tu, lazima tuwajibike kwa kuwasaidia ndugu zetu, hasa kwa mawazo, kumbuka bin-adam huenda chini pale anapofikiri yupo juu na kwamba hahitaji msaada wa mawazo! Uzuri wa mchezo wa mpira huonwa na kusemwa na watazamaji sio wachezaji, kwenye hili la Wangwe watazamaji tumeshaona kuna mdudu kakauona!”

(Mzee Es- FMES)

“Sasa lengo liwe nini? Kwa vile kubadili watu siyo tatizo kubwa zaidi na ambalo ni rahisi kulishughulikia, basi wapinzani watakapoamua kushirikia wasiweke lengo kuondoa watu bali kubadili mfumo na kuleta mabadiliko katika nchi. Mabadiliko ya muundo na mfumo uliojenga ufisadi ambao kubadilishwa kwake ndiko kutasababisha kuanguka kwa CCM.

Leo hii Kenya wamewaangusha Mawaziri 16 na bila shaka watamuondoa Rais wao lakini watafanya hivyo kama matokeo ya kuamua kuangusha mfumo mbovu uliopo licha ya mafanikio ya kiuchumi chini ya Kibaki.

Sasa tunapoamua kuweka lengo la kuleta mabadiliko katika mfumo na muundo basi ni rahisi zaidi kama Taifa kubadilishana uongozi. Hata hivyo kuna sababu nyingine au msingi mwingine ambao wapinzani wanaweza kuutumia kama msingi wa kuungana kwao”

(Mzee Mwanakijiji)


“Mathlan Chadema wanaweza kuwa waamini kuwa maendeleo yetu yatatokana na kilimo na wakakipa nafasi zaidi ya CCM lakini tunapofikia kulinda maslahi ya viingizio hivi hakuna sera ila ni uzalendo wa kusema na kukubali kinachovunwa kuwa kipo isipokuwa... balaa blaa blaaa”

(Mkandara)

“You need to sit out for a minute and do some soul-searching and hopefully next time around you'll come back better, with a purpose and a clear direction of where you want to take the country.”

(Nyani Ngabu)

Tuendelee kujadili…
 
nionavyo mimi nchi yetu kwa sasa inahitaji wazalendo zaidi kuliko mambo mengine.migogoro ndani ya vyama vyetu inatuumiza sana wafuasi na wapiga kura.Mimi ninadhani hao jamaa wa jirani yawezekana uzalendo uko juu kuliko bongo.huu ni mchango
 
Mnyika mara nyingi nazikubali hoja zako mkuu,lakini ni lazima ukumbuke ya kuwa mijadala mirefu haitusaidii sana ktk nchi hii katika kuleta mabadiliko.

Tuna ugonjwa wa kusahausahau wapi tumeanzia na sasa tuko wapi tuwapo katika mijadala hiyo hasa kunapokuwepo na uvurugaji wa makusudi toka kwa watawala.Mabadiliko thabiti yanataka nia na mkakati wa kimapambano kama wenzetu wa Kenya walivyojipanga na sasa wao wananchi ndio wenye mamlaka na sio watawala.

JM,sikatai, mijadala ni kama chachu ya harakati mbalimbali lakini hayo tusubiri 2010 ili tufanye yale ambayo watawala wetu hawayategemei (kuwang`oa)kisha tuanze hiyo mijadala kwa manufaa ya nchi yetu.
Kumbuka baada ya Zitto kusimamishwa Bungeni,hakukuwa na mijadala ila ujumbe ulienezwa kwa waTZ kwa style ya kimbunga jangwani na madhara iliyopata CCM waulize Mawaziri na Wabunge watakueleza.
Muhimu watu wahamasishwe kuchukia tawala fisadi na Kitaeleweka tuu.
 
nionavyo mimi nchi yetu kwa sasa inahitaji wazalendo zaidi kuliko mambo mengine.migogoro ndani ya vyama vyetu inatuumiza sana wafuasi na wapiga kura.Mimi ninadhani hao jamaa wa jirani yawezekana uzalendo uko juu kuliko bongo.huu ni mchango

Hivi hii migogoro inayoongelewa ni ipi hasa? Ni ile ya akina Mrema miaka ile? Sasa hivi ni chama gani hicho chenye mgogoro?

Tusije tukawa tunaishi Tanzania tofauti!
 
Mnyika mara nyingi nazikubali hoja zako mkuu,lakini ni lazima ukumbuke ya kuwa mijadala mirefu haitusaidii sana ktk nchi hii katika kuleta mabadiliko.Tuna ugonjwa wa kusahausahau wapi tumeanzia na sasa tuko wapi tuwapo katika mijadala hiyo hasa kunapokuwepo na uvurugaji wa makusudi toka kwa watawala.Mabadiliko thabiti yanataka nia na mkakati wa kimapambano kama wenzetu wa Kenya walivyojipanga na sasa wao wananchi ndio wenye mamlaka na sio watawala.
JM,sikatai, mijadala ni kama chachu ya harakati mbalimbali lakini hayo tusubiri 2010 ili tufanye yale ambayo watawala wetu hawayategemei (kuwang`oa)kisha tuanze hiyo mijadala kwa manufaa ya nchi yetu.
Kumbuka baada ya Zitto kusimamishwa Bungeni,hakukuwa na mijadala ila ujumbe ulienezwa kwa waTZ kwa style ya kimbunga jangwani na madhara iliyopata CCM waulize Mawaziri na Wabunge watakueleza.
Muhimu watu wahamasishwe kuchukia tawala fisadi na Kitaeleweka tuu.

Chakaza

Nakushukuru kwa mchango wako kuhusu Dira na Utume. Naona umeshatoa mapendekezo tayari. Kumbuka ule moto wa Buzwagi uliwaka baana ya kukolezwa na hoja ya ufisadi wa BOT na kupitishwa kwa bajeti iliyopandisha gharama za maisha hata baada ya wapinzani kuwasilisha bajeti mbadala. Jumla ya haya ndio ilizaa UJUMBE, ulioamsha wananchi kwa kiwango ulichoelezea.

Nikisoma katikati ya maneno yako naona dira na utume unapendekeza: "Kuwa na serikali yenye kupambana na ufisadi na kusimamia vizuri rasilimali za Taifa katika kujenga fursa za maisha bora kwa wananchi wote".

Kwa mapendekezo yako, huu ndio ujumbe ambao ushirikiano wa upinzani unaweza kuwa nao na kwa kuwa nao huo wananchi wataunga mkono, upinzani utachukua dola na kuleta mabadiliko yanayokusudiwa. Nimekupata vizuri?

JJ
 
Hivi hii migogoro inayoongelewa ni ipi hasa? Ni ile ya akina Mrema miaka ile? Sasa hivi ni chama gani hicho chenye mgogoro?
Tusije tukawa tunaishi Tanzania tofauti!

Kitila na Tzpride,

Na hapa ndio ulipo msingi wangu wa kukosoa ule utafiti wa REDET- uamuzi wa ku-generalize, ume-influence maoni ya wananchi.

Kama swali lingekuwa ni sababu zipi wananchi zinawafanya wasiwe na imani na CHADEMA per se, matokeo yasingekuwa: Sababu ya Kwanza MIGOGORO, sababu ya pili: KUTOKUWA NA SERA. Na naamini kabisa kiwango cha wananchi wenye imani na CHADEMA katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kingeongezeka zaidi ya 0.8% iliyotajwa na REDET.

Naamini hili katika utafiti wao unaofuata REDET na hata taasisi nyingine zitazingatia hili. Suala la migogoro kwa sasa si hoja kuu kiasi hicho. Ndio maana kwa maoni yangu suala la kupatiwa mwelekeo thabiti ni nini upinzani upaswa kufanya ukichukua dola?

Na ni kwa namna gani upinzani unaweza kuchukua dola? Haya ni masuala ambayo sisi kwa ndani tunayo mitazamo yetu, lakini kwa kuwa vyama vya siasa ni taasisi za wanachama na umma kwa ujumla, mjadala kama huu hapa ni wa muhimu kupata mawazo na maoni mbalimbali

JJ
 
kwa sasa nafuatilia kwanza uchaguzi wa kenya baadae nitachambua mada zako, ila nahitaji maelezo ya kina viti maalumu mligawanaje. kwa taarifa ccm wameajiri program officers kila mkoa wenye MBA na Phd kuratibu shughuli za chama kitaalamu zaidi. ccm unayoijua siyo ya 2008, kama huamini kamulize profesa shayo au Dr.Katunzi. Wangwe na Zitto wanafununu na kinachoendelea, ndio maana wakashauri angalau 40mil zipelekwe mikoani kilamwezi kuimarisha chama, mmekuwa wabishi.
 
nionavyo mimi nchi yetu kwa sasa inahitaji wazalendo zaidi kuliko mambo mengine.migogoro ndani ya vyama vyetu inatuumiza sana wafuasi na wapiga kura.Mimi ninadhani hao jamaa wa jirani yawezekana uzalendo uko juu kuliko bongo.huu ni mchango

Kama nimekuelewa: Dira/Ajenda ya msingi ni: kuweka madarakani serikali yenye viongozi wazalendo.

Nashukuru. Swali la kujiuliza- ili wafanye nini? Nini matokeo ya kuwa na viongozi wazalendo? Unaweza kuwa na viongozi wazalendo, lakini hawajui wapi taifa lielekee, je- tutafika?

Tuendelee kujadili, na amini- mawazo mbalimbali yanayotolewa hapa tutayafanyia kazi.

JJ
 
kwa sasa nafuatilia kwanza uchaguzi wa kenya baadae nitachambua mada zako, ila nahitaji maelezo ya kina viti maalumu mligawanaje. kwa taarifa ccm wameajiri program officers kila mkoa wenye MBA na Phd kuratibu shughuli za chama kitaalamu zaidi. ccm unayoijua siyo ya 2008, kama huamini kamulize profesa shayo au Dr.Katunzi. Wangwe na Zitto wanafununu na kinachoendelea, ndio maana wakashauri angalau 40mil zipelekwe mikoani kilamwezi kuimarisha chama, mmekuwa wabishi.

Nashukuru.

Hao waratibu nadhani ni vyema mngeanzia pale ikulu ili serikali iongozwe kwa dira nzuri zaidi na mngewekeza pia makao makuu ya chama ili CCM iweze kutoa dira bora zaidi kwa taifa. (Joke)

Mwisho wa siku wananchi hawatapima chama kinachotawala kwa idadi ya makada walioajiriwa bali kwa matokeo ya uongozi wa chama katika kuleta mabadiliko katika hali za wananchi hususani kwa kutekeleza ahadi zilizotolewa. Hayo ya viti maalumu, ruzuku nk tumeshayajadili sana hapa.

Na nimetoa maoni yangu katika maeneo kadhaa. Tembelea hizo thread za "CHADEMA must reform" na "FOCUS 2010" utapata majibu ya maswali uliyoibua. Hapa tujadili kuhusu "DIRA/AJENDA/SERA" ya serikali mpya itakayokuwa madarakani mwaka 2010.

Ukitoka mjadala wa Kenya karibu hapa kieleweke.

JJ
 
Hivi kwa nini tunaogopa mijadala? Tatizo liko wapi kama mjadala utakuwa academic? Mimi binafsi ningefurahi kama mkitueleza mtatufikishaje huko mnakotaka kutufikisha kwa kutumia rasilimali ambayo tunayo.

Ningependa mtueleze mtatuondoaje kwenye ujinga uliotanda kwa kutumia kipato chetu wenyewe. Mtueleze vipi mtatuhakikishia wake zetu na watoto wetu hawafi wakati wa uzazi. Mtueleze vipi mtaulinda urithi (mbuga za wanyama, mazingira masafi, miji yetu ya kihistoria n.k.)tulioachiwa na babu zetu ili na wajukuu wetu waweze kuufaidi. Mtueleze mtatuhakikishiaje kuwa haki inatolewa kwa wote bila upendeleo wa aina yeyote.

Mtueleze vipi mtakuwa nasi katika safari hii ndefu kutoka hapa tulipo bila wenzetu kutuacha sis tukisukuma gari kwenye matope wakati wenzetu mmekaa ndani kwenye kiyoyozi. Mtueleze mtafanyaje yote haya kwa kutumia kipato tulichokuwa nacho na si ndoto za alinacha. Mtueleze mtafanya nini ili makosa ambayo wenzenu wameishayafanya hayatarudiwa.
 
Kazi tunayo! Haya sasa, hii dira na utume upi huu? Naomba nielewe.

Syllogist

Inawezekana DIRA na UTUME ni dhana tata na tete! na pengine zimekaa kiasasiasasi. Nimetoa mfano hapo wa Dira ya chama cha Democrat cha Marekani- Dira(Vision) ni kule unapoelekea, ni hali ambayo unataka mwishowe uifikie. Wakati, utume(mission) ni njia na namna ya kufikia kwenye dira ama ni ngazi ya kupanda kuelekea kwenye unapokutaka. Kwa maneno machache- dira ni dhamira, na utume ni jinsi unavyodhamiria kuifikia dhamira. Kwa lugha nyepesi, dira ni tutakacho, na utume ni namna ya kukipata tutakacho.

Anyway, MODS- naona mjadala umekua mgumu kutokana na kichwa chenyewe: Naomba ubadili jina la mada liwe; DIRA YA SERIKALI MPYA YA 2010" ama "AJENDA YA UKOMBOZI" ama "UJUMBE WA MABADILIKO". Chagua mwenyewe utayaoona inafaa. Asante.

JJ
 
Hapana, Mkuu Mnyika. Tunapenda mno majibu mepesi mepesi. Ndiyo maana tunawakumbatia sana mamasia wauongo kila wanapojitokeza. Tubanane humu humu na kwa wale wanaoona hii ishu ni ya kisomi zaidi waende kwenye habari nyepesi nyepesi. Mimi binafsi ingawa si msomi ningependa nipate furs ya kuwasikiliza wale wanaotaka kutuongoza wakibadilishana mawazo na wananchi wao kana kwamba nao ni watu wazima wenye uwezo wa kufikiri.
 
Back
Top Bottom