Blah blah blah blah Watu wana njaa ya mabadiliko wewe unaleta theories za vision mision kwani tuko shule hapa.Watu washike silaha waingie mitaani,hiyo ndio sulihisho.
Hilo sio suluhisho bwana Sozi. Hiyo njaa ya mabadiliko walikuwa nayo wasomali kwa kumchoka sana Gen Mohammed Siad Barre, na kweli wakamng'oa. Kilichofuata baada ya hapo sote tunakiona hadi leo, hakuna utulivu. Kosa lao? Waliung'oa utawala bila maandalizi makini ya kuweka utawala mwingine, likawepo ombwe (vacuum) ambalo factions nyingi zikawa zinagombea kulijaza, ikawa anarchy hadi leo.
Kama tumemchoka mbebaji wa chungu chetu cha asali, tuandae mbebaji mwingine kabla hatujamnyang'anya huyo chungu hicho, la sivyo tukisema tumnyang'anye kwanza ndipo tutafute mbebaji, anaweza akakosekana, matokeo yake tunamwaga kila kitu.
Tuandae kwanza timu yenye uwezo wa kuchukua madaraka, yenye acceptance nchi nzima, na yenye vision inayokubalika, ndipo tushawishi watu jamani ondoeni CCM madarakani wekeni chama B kwa sababu kadha kadha kadha.
Unapowaambia watu waikatae CCM wakati hawaoni alternative, hawawezi kukukubalia. Pengine baadhi yetu wanaamini alternative ipo, lakini wapiga kura walio wengi hawajaliona hilo! Kazi ya kufanya ni kuwaonesha hiyo alternative na kuwashawishi juu ya suitability yake, na jinsi ilivyo bora kuliko utawala uliyopo.
Nina mfano rahisi. Kipindi fulani huko Bongo nilishiriki katika kampeni moja ya utunzaji wa mazingira, na mojawapo ya ujumbe tuliokuwa tunawapa watu ni kupunguza idadi ya mifugo na kuachana na ufugaji wa kuhamahama. Walikuwa wanatusikiliza tu, hawasemi kitu. Lakini baadae mzee mmoja akanifuata na kuniambia "mmekuja tu kutembea, hakuna kitakachobadilika hapa!" Sababu aliyonipa ni kuwa wao hawajui kazi nyingine, na namna ya kufuga wanayojua wao ndio hiyo, sasa tunataka waache halafu wataishije? Ile kampeni kusema kweli tulifeli kwa sababu ya kukosa maandalizi makini.
Nataka tuelewe kwamba watanzania wanao uwezo wa kutathmini na pale wanaporidhika na kitu huwa wanakichukua. Mifano ipo mingi. Katika majimbo ambayo wananchi waliridhika kwamba alternatives walizopewa ni bora kuliko CCM, walichagua hizo. Tumeyaona hayo Karatu, Kigoma, Tarime, Pemba, Biharamulo, Moshi mjini na sehemu nyingine ambako wananchi wamechagua upinzani. Hata sehemu ambazo mchuano wa uchaguzi ulikuwa mkali (tuseme ambako upinzani ulipata 40% ya kura au zaidi), tunaweza kusema gauge ya kukubalika ilikuwa inapanda, na kuna matumaini ya chama kilichopata kiasi hicho kwamba kina nguvu pale, nina uhakika yapo majimbo ambayo upinzani haukushinda lakini ulikaribia sana, hayo pia ni matumaini makubwa yanayopaswa kulelewa ili next time ushindi upatikane. Changamoto iliyoko kwa upizani ni kuzalisha wagombea wengi wenye uwezo wa kuichachafya CCM nchi nzima, yaani majimbo yote nchini CCM wawe wanahangaika kama walivyoangaika Kigoma, Moshi mjini, Karatu, Pemba, Ubungo nk, hapo wananchi wataona kweli kuna uchaguzi. Maana uchaguzi unapaswa uwe fursa ya kuchagua kimoja kati ya kadhaa ambavyo vyote vinafaa, lakini mwananchi anatafuta chenye kufaa zaidi. Sasa iwapo mwananchi ataona anapaswa kuchagua kati ya gari bovu linalotembea na kitu kingine ambacho hana uhakika kama ni gari au kibanda, basi anaona bora hilo gari bovu, atasogea sogea!
Kama huko Lindi, Mtwara na kwingineko hawajapata kuona mgombea wa upinzani wa kukaribia kufanana na kina Zitto, Ndesamburo, Wangwe, Mnyika na wengine wa namna hiyo, tuna haki gani ya kuwalaumu kwa kuichagua CCM? Vyama vya siasa vina wajibu wa kujijenga nchi nzima na kuwa na "bank" ya wagombea wazito na wazuri nchi nzima, hapo hata wananchi wanaelewa tukiondoa CCM tunaweka hawa hapa tunawaona. Hii ndio changamoto tuliyonayo kabla ya kuzungumzia kumng'oa rais wa CCM (maana kuna wanaodhani ati kuchagua rais wa upinzani ndio kuiondoa CCM madarakani! bado kabisa!) Kuiondoa CCM madarakani ni kuondoa mfumo wote, na ili hilo lifanikiwe tunahitaji mfumo mbadala ulio tayari kuchukua nafasi hiyo mara. Tujenge na kuuimarisha huu mfumo mbadala kwanza.