Dira na itikadi ni nyenzo muhimu katika siasa


M

Mghaka

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
320
Points
195
Age
57
M

Mghaka

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
320 195
Katika dunia ya siasa ya miaka 90 na kurudi nyuma itikadi katika siasa ilikuwa ni utambulisho wa nchi na chama kwa jamii, baada ya kuanguka kwa taifa la Urusi utambulisho wa itikadi ulikosa nguvu tena na kuwa siasa zilihamia katika kuelezea mitazamo inayobebwa na wanasiasa (personality in politics or politics in personality). Katika mabadiliko mengi yaliyofuata miaka 90 katika nchi za Asia, Afrika na yale tunayoyaona leo katika nchi za uarabuni haikuwa siasa bali vuguvugu la kutaka mabadiliko kwa sababu ama ya ukosefu wa haki za msingi za watu au kuchoswa na mfumo usiokubali mahitaji ya msingi ya mabadiliko kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia kizazi kipya.

Katika vuguvugu la mabadiliko yenye msukumo wa kivuguvugu na msukumo wa 'common feelings" viongozi wengi ni opportunist na wanabebwa na ukweli kuwa wananafasi ya kubeba bendera ya upepo wa mabadiliko na kuwasemea kwa nguvu wanaohitaji mabadiliko hayo. Mazingira ya mabadiliko haya huunganisha watu kama vile wasafiri ambao baada ya mwisho wa safari yao si wamoja tena. Tanzania tusisubiri kuingia katika mkumbo wa aina hii na wanasiasa au vyama vya siasa visitupeleke huko. Si nchi nyingi sana ambazo kiukweli zimewaunganisha wananchi wao kwa itikadi na dira, Tanzania tuliwahi kupata bahati hii lakini kila kukicha tunaipoteza na sasa lazima tuidai kwa viongozi wetu, suala si CCM tu kuwa haina itikadi na imesahau historia yao (Bashiru, Taz.Daima/mdahalo wa Star TV asubuhi 17/11/2012) bali vyama vyote kwa sasa mtaji wao ni matatizo ya wananchi, ndio hili ni jambo jema sana na ndio siasa lakini it has to be hooked into your party ideology and vission.

Muda tulio nao si rafiki kufikia mwaka 2015 lakini unatosha kwa akili kubwa kutupatia itikadi na dira ya kisiasa ambayo kwa sasa katika nchi yetu ni bidhaa adimu. Ilani ya uchaguzi si mafikira ya hewani bali ni mfululizo wa hatua za kuchukua DHIDI YA HALI ISIYORIDHISHA KWA MANUFAA YA KIMAENDELEO na huhesabika kama ahadi ya chama kinachoomba ridhaa ya kuongoza kwa wapiga kura. Na mara baada ya chama chochote kushinda uchaguzi ilani yake inakuwa ni mkataba wa hiari na wananchi wa taifa lile kwa ujumla wao bila kujali itikadi zao.

Nimewahi kuandika katika ukurasa wa JF kuhusu CDM kuchagua kuwa na vitu hivi mapema na kuhakikisha vinawafikia watu wote kwa haraka na tuhakikishe kuwa tunawaanda makada wetu kushika usukani wa kuineza itikadi na dira yetu ambayo itatuzalia ilani ifikapo mwaka 2014/2015. Narudia tena amkeni. mifano ya itikadi ipo mingi (Ulinzi na matumizi sahihi ya rasilimali zetu kwa maendeleo yetu, Elimu sahihi kwa wananchi kwa ujenzi wa taifa, uadilifu, uwajibikaji na ulinzi wa rasilimali kwa maendeleo ya nchi n.k). Nyerere aliifikiria nchi yetu kwa wakati huo akaongoza chama kuandika itikadi ya ujamaa na kujitegemea ebu igeni mfano huo mtatutoa hapa tulipo na kusafiri umbali mwingine wa miaka 50 tukiwa wamoja na kama taifa. kazi kwenu wanasiasa Waghaka tupo kwa ajili ya kuwasaidia


Kila nikiamuka asubuhi nahisi nasutwa kuitendea jema nchi yangu, kwa vipi? katika hali ya kiwango cha chini ni pamoja na kukaa chini na kufanya uchokozi kama huu ili kutengeneza jukwa dogo la kuwafanya watu wajumuike kiakili kwa ujenzi wa taifa lao, ninayo furaha kuwakaribisha katika mjadala huu mdogo.
 

Forum statistics

Threads 1,294,754
Members 498,027
Posts 31,187,127
Top