Diplomasia ya Magufuli versus diplomasia ya Uhuru Kenyatta

Kwanza unatakiwa uelewe mganga hajaruhusu safari za ng'ambo.
Pili.. Yule ni UHURU.. na huyu ni POMBE.. Yaani mtoto wa RAIS kwa mtoto wa MKIMBIZI.
Mwisho.. na kichaga hakijui vzr mzee baba.
 
Tukubaliane kwamba 'bottom line' ya huu uzi ni TZ vs Kenya.

Kuhusu hili suaka la diplomacy na ziara za nje za ma rais Kenyatta vs. Magufuri kuna mambo kadhaa ya kuangalia:

1. Hakuna nchi ya Afrika mashariki na Afrika kusini mwa jangwa la Sahara kwa ujumla yenye mafanikio na heshima kidiplomasia kama Tanzania. Hii ilijengwa na kina Nyerere, Salim S. Salim, Hashim Mbita, 'Arusha Peace Processes' za Rwanda, Burundi, DRC, South Sudan, nk. Kumbuka vile vile kusini mwa Sahara kuacha vita vya Ethiopia na Eritrea, TZ ndio nchi pekee iliyopigana inter-state war ya muda mrefu na kushinda.

2. Marais wenye vipindi viwili hupenda kutumia kipindi cha pili kutengeneza 'legacy' zao kabla ya kuondoka madarakani. Kenyatta yuko kwenye 'term' yake ya mwisho. Hata Trump, kipindi chake cha pili atakuja Afrika ingawa aliziita 'sxxt hole countries'.

TZ msijilinganishe na Kenya. Kenya wana matatizo ya kimdingi ambayo hayana utatuzi ('intractable structural issues') za ukabila, ufisadi, nk.

Uhuru Kenyatta hata alale chumba kimoja na Trump, Thereza May na Xi Jinping hawezi kutatua the real problems za Kenya!!

Sehemu kubwa ya faida ya hizo deals anazofanya huko zitaishia mifukoni mwa wajanja wenzake!! Na ndio maana mazungumzo yao na Switzerland na England yalitawaliwa na suala la kudhibiti mabilioni ya hela zilizoibiwa Kenya na kifichwa huko.

Wapigaji wa Kenya si wa mchezo mchezo!!

Sisemi kama namtetea Magufuli kutokusafiri. Nachosema tu ni kwamba watu wasi 'panick' kwa kujilinganisha na safari za Uhuru Kenyatta.

Tutafute njia nyingine ya kudadavua faida ('efficacy') ya ziara za nje kwa TZ badala ya kujilinganisha na Kenya.
 
Back
Top Bottom