Diplomasia (Sio Ubabe) Itumike Kurudisha Uhusiano Mzuri Baina ya Tanzania na Taifa la Marekani

Tin guy

Member
Nov 16, 2017
25
45
Kufuatia tukio lililotokea hivi karibuni la Ndugu Paul Makonda (RC wa Dar es Saam) pamoja familia yake kuzuiwa kuingia Marekani limeacha doa la mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Marekani huku kukiwa na maoni tofauti katoka kwa watu; watu fulani wakiipongeza Marekani huku wengine wakiilani.

Haya ni maoni yangu binafsi kama Mtanzania.

Kwanza, wote tukubaliane kwamba Marekani huwa na tabia ya kuingilia mambo ya ndani ya mataifa mengine ikiwa na maslahi binafsi, hususani ya kiuchumi.

Pia Marekani ana uwezo wa kuiwekea vikwazo nchi yoyote hapa chini ya jua kutokana na nguvu yake katika Umoja wa Mataifa ( UN).

Pili, tukubaliane juu ya ongezeko la uwepo wa vitendo vya uvunjifu wa demokrasia na haki za binadamu hapa Tanzania katika awamu hii ya serikali.

Matukio kama: shambulio dhidi ya Lissu, kupotea kwa Azory Gwanda, Ben Saanane, mikutano ya kisiasa kuzuiwa na chaguzi zisizoridhisha katika uwazi ni ushahidi tosha; matukio ni mengi, hayo ni baadhi tu.

Sasa basi ni hivi, Marekani ili akuingilie katika taifa lako huwa anatafuta eneo ulilo dhaifu (mara nyingi udhaifu katika demokrasia) na kulitumia kama fursa.

Marekani imekuwa ikitumia kukosekana kwa demokrasia na haki za binadamu katika nchi fulani kama fursa ya kuziingilia. Kumbuka UN inaitambua Marekani kama kilanja wa dunia na hivyo inaipa mamlaka ya kuingia popote kama sababu zina mashiko mbele ya UN. Ilifanya hivyo kwa Libya, Iraq, DRC Congo, Angola na nchi nyinginezo.

Sasa basi, ili kukwepa hilo lazima taifa lihakikishe angalau linatunza misingi mikuu ya kidemokrasia na haki za kibinadamu kama zinataka Marekani asiwaingilie.

Ukipigana na Marekani kwa vitendo utaumia. Hili ni taifa lenye zaidib ya 20% ya uchumi wa Ulimwengu mzima, lenye 25% ya dhahabu yote ulimwenguni, linalochangia 22% ya bajeti ya UN hivyo kuwa na ushawishi mkubwa katika UN kupitia kura ya Vetto.

Marekani ni taifa No.1 kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia, pia washirika wake ni mamwamba tu. Pia Marekani ndio nchi inayoongoza kutoa misaada Tanzania.

Wengine wanasema eti ajenda ni "ushoga " pia vita vya kuichumi Tanzania inapitia. Nahisi hapana kwa sababu mbona kuna nchi mfano Afrika ya Kusini inayoongoza kuzalisha dhahabu Afrika, Ghana ya pili kwa kutoa dhahabu Afrika na Botswana inayoongoza kutoa Almasi Afrika hatujasikia zikiiingiliwa na Marekani wala kulazimishwa kukubali ushoga?

Kwani Marekani haijaona dhahabu iliyopo Afrika ya Kusini na Ghana na ile Amasi ya Botswana hadi ichague kuchukua dhahabu na almasi ya Tanzania tu? Kwa kuongezea nchi hizi zina gesi asilia na mafuta ya petroli na ardhi ya kutosha yenye rutuba.

Je kwa nini basi Marekani hajaziwekea vikwazo vya kiuchumi hizi nchi ili zimpe madini yazo? Maana nchi hizi zote ni nchi zenye uchumi mzuri katika Afrika.

Jibu ni kwamba Marekani anatamani sana utajiri wa nchi hizo ila anashindwa kupata point ya kuziingilia (entry point) kwa sababu nchi hizo zote zinatawaliwa kwa #demokrasia ya hali ya juu na kuheshimu kwa hali ya juu #haki za #binadamu.

Ona kilichotokea DRC Congo, vita vya wenyewe kwa wenyewe vikafanya mataifa makubwa ikiwemo Marekani na mataifa ya Ulaya kuingia Kongo na kujichukulia madini (dhahabu) na chochote walichotaka kadiri watakavyo.

Ona kilichotokea Angola enzi za Jonas Ssavimbi, vita vya wenyewe kwa wenyewe vikafanya Marekani apate fursa ya kuingia Angola na kuchimba mafuta kadiri alivyokuwa anataka!

Hivyo, pengine Marekani akiona kuna uvunjifu wa demokrasia Tanzania anafurahi maana anaona kuwa anakuja kupata fursa ya kuingia Tanzania na kufanya kama alichofanya Iraq, Libya na Ukraine.

Hivyo hamna namna nyingine kwa sasa tunavyoweza kukabiliana na Marekani isipokuwa kuhakikisha tunadumisha demokrasia na haki za msingi za binadamu nchini mwetu.

Tukifanya hivyo, Marekani atakosa ajenda ya kuingilia (entry point) siasa zetu za ndani na hivyo tutakuwa salama.

Walio jaribu kupingana na Marekani/Wazungu kwa vitendo ikiwemo Mugabe walipata taabu sana. Ofcourse, mtu akiwa anakukopesha au kukupa msaada lazima kuna masharti atakupa na ili upate mkopo/msaada lazima uyafate.

Mfano mtu anayekukopesha/ kukusaidia anaweza kukuamrisha kuhusu muda utakaokuja kuchukua mkopo/msaada, jinsi unavyotakiwa kuwa umevaa ukiingia ofisini kwake, jinsi ya kuingia, jinsi ya kutoka, na pengine jinsi ya kutumia msaada/mkopo uliopata.

Pia mtoa msaada/mkopo anaweza kusitisha huduma yake/pengine kuja kukunyangana kabisa akiona wewe ni mgomvi na una matumizi mabaya ya fedha au madaraka kama wewe ni kiongozi.

Hivyo basi pia katika hii mikopo na misaada tunayopewa mataifa hayo yanatoa masharti kama uwepo wa amani, utawala bora, uwazi na uwajibikaji, demokrasia na haki za kibinadamu katika nchi zinazopokea misaada (kama Tanzania).

Bila hayo kutokea nchi hizo husitisha misaada/mikopo.

Pia niungane na wengine kwamba masharti mengine ni magumu kutekelezeka na hivyo bura tunyimwe misaada na tuteseke kuliko kuikubali.

Ni kama mtu anayekupa msaada/mkopo kwa kukutaka umruhusu alale na mkeo! Bila shaka utakataa hata kama kukataa kwako kutapelekea kifo Masharti mengine kama niliyoelezea hapo juu unaweza kuyakubali ila sio hili.

Hapa namaanisha kwamba #Tanzania tunaweza kukubaliana na hayo mataifa katika haki za msingi za binadamu ila hayo mataifa yakifikia hatua ya kututaka tuhalalishe ndoa za jinsia moja hapo hakuna radhi bali kuwaambia wapeleke mbali misaada yao na kama ni vikwazo watuwekee watakavyoweza!

Bora tuteseke na kufa huku tukiutetea na kuulinda utu wetu.

LAKINI KUTOKUHESHIMU HAKI ZA MSINGI ZA BINADAMU NA ZA KIDEMOKRASIA ZISIZO NA UGUMU WOWOTE KUTEKELEZWA KAMA UCHAGUZI HURU NA HAKI, UHURU WA KISIASA NA UHURU WA KUISHI, KUKUTANA NA KUTOA MAONI, UHURU WA KIDINI NA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI KUSITUPELEKEE TUINGIE KATIKA HATARI YA KUWEKEWA VIKWAZO VYA KIUCHUMI NA MAREKANI!
 
Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
3,320
2,000

Asante kwa maono. Huu ndiyo ukweli na kama huwezi basi ngatuka maana Nyerere naye aliondoka kwa manufaa ya taifa kwasababu asingeweza kuongoza kwa misingi aliyoiita ubeberu. Kuna wakati unafanya vitu kwa manufaa ya nchi. Tumekuwa wepesi wa kulalamika sana.
 
Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
2,978
2,000
Makala nzuri sana, ila kuna ng'ombe (wenye kichaa kisichokua na tiba) humu JF watakuja kumwaga kinyesi hapa.

Kuna mambo pia ya msingi sisi kama raia tunapaswa kujiuliza na kuhoji (tuweke mbali maswala ya kichama).

Mfano, juzi Mh Rais amesema "SERIKALI HAINA HELA", na huu ni mwezi wa pili tunaelekea mwisho wa mwaka wa kiserikali (June/July), kwa lugha nyingine tunaelekea kwenye bunge kupanga budget ya matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Hio fedha ya budget za wizara zote itakayopangwa bungeni, tukumbike wanaotupa misaada ya kifedha wameshaanza kutoa matamko ya kukata misaada na kuwekewa vikwazo, sambamba na kuzuiwa kupewa mikopo World Bank.

HOJA; Hizo hela tutazitoa wapi za kutimiza matumizi wa wizara zote??? Tutakopa na kuendelea kuongeza madeni???
 
Top Bottom