Diploma ipi inauzika mtaani kati ya hizi?

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,446
16,301
Habarini wakuu, kuna mzee kanipigia kutoka maeneo yetu vijijini ndanindani kule, anaomba ushauri wa kupewa idea ya kijana wake akajiendeleze kwa kipi kwa matokeo aliyopata kidato cha nne mwaka jana.

Kijana ana division IV ya point 26 na hivi ndivyo ubao wa matokeo yake unavyosoma

Civics-------------------->C

History------------------>D

Geography------------>D

Kiswahili--------------->B

English------------------>C

Biology------------------>F

B/Mathematics----->F​

Sasa katika pitapita zangu nikapata kozi zifuatazo ambazo anaweza kuapply kulingana na matokeo yake. Nachoomba wajuvi wa mambo nisaidieni kujua kozi ipi hapa ina uafadhali na haitamuangusha dogo pindi amalizapo, hata kama hataajiriwa lakini hatakosa japo vi-intern na volunteering za hapa na pale maana najua ajira kwa sasa ni mbombo ngafu.

1. Ordinary Diploma in Land Management Valuation.

2. Ordinary Diploma in Urban and Regional Planning.

3. Ordinary Diploma in Freight, Clearing and
Forwarding.

4. Ordinary Diploma in Logistics and Transport
Management.

5. Ordinary Diploma in Shipping and Port
Management.

6. Ordinary Diploma in Shipping and Logistics
Management.

7. Ordinary Diploma in International Relations and
Diplomacy.

8. Ordinary Diploma in Public Relation and Marketing.

9. Ordinary Diploma in Procurement and Supply.

10. Ordinary Diploma in Marketing.

11. Ordinary Diploma in Marketing Management.

12. Ordinary Diploma in Business Administration.

13. Ordinary Diploma in Accountancy.

14. Ordinary Diploma in Community Development.

15. Ordinary Diploma in Social Work.

16. Ordinary Diploma in Law.


NB: Kijana ni mtoto wa mkulima hana connections zozote na hajawahi kufika hata mjini
 
Me ningechagua kati ya:

1, 2, 12, na 16

1 na 2 nahisi baadae zinaweza kua deal.

12 na 16 naamini rahisi ata kujiajiri au kujishikiza sehemu bila ata mtaji mkubwa.

Last but not least, ongea na dogo direct yeye anapenda nini. Usikute anapenda mambo ya IT maana sijaona hapo.

Pia kama anaweza, angerisiti masomo ya: Biology na Mathematics itamsaidia kupata nafasi vyuo vya Engineering ambapo atapata fursa zaidi.
 
Me ningechagua kati ya:

1, 2, 12, na 16....
Asante sana mkuu.

Tatizo dogo aliacha Physics & Chemistry, hakuzisoma kabisa.

Huyu dogo kwa kifupi afya na engineering hawezi kupagusa unless akasome Biology, Chemistry, Physics & B/Mathematics upya.

Unforgetable
 
Asante sana mkuu.

Tatizo dogo aliacha Physics & Chemistry, hakuzisoma kabisa.

Huyu dogo kwa kifupi afya na engineering hawezi kupagusa unless akasome Biology, Chemistry, Physics & B/Mathematics upya.

Unforgetable
Akipata D ya Geography, Biology na Mathematics anapata Chuo. Niamini mimi.
 
Tatizo lipo hapo kwenye koneksheni sasa

Tunakosa koneksheni(in mfalme's voice)

Unforgetable
Kuna mdau kaongelea veta hapo juu, ni bonge la mchango chukua bila kusita.
Siku hizi veta ni bonge la fani-kapige umakenika wa magari/pikipiki, umeme wa magari au majumbani. Akisoma umeme KALEMANI amuita na mambo safi safi huko KALEMANINI pesa ipo maisha yanaenda
 
Habarini wakuu, kuna mzee kanipigia kutoka maeneo yetu vijijini ndanindani kule, anaomba ushauri wa kupewa idea ya kijana wake akajiendeleze kwa kipi kwa matokeo aliyopata kidato cha nne mwaka jana....
Mkuu, kwa ninavyofahamu ni lazima apitie Astashahada ndiyo ataingia Stashahada kwa hao walioishia Kidato cha nne.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aende chuo cha Ardhi morogoro au Cha Tabora kule kuna course nzuri sanaa ambazo ni very marketable.. sisi ambao tumesoma degree zao tumeajiriwa na hao waliosomaga diploma katika hivyo vyuo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom