Diploma Holder miaka 30 kukosa Mkopo ni ubaguzi

juju000

Senior Member
Apr 2, 2015
151
92
Nimesoma taarifa ya bodi ya mikopo kuhusu marejebisho ya vigezo vya utoaji wa mikopo ya elimu ya juu lakini kuna mambo mawili bado sijayaelewa, na bahati mbaya bodi wamekwepa kuyatolea majibu kwenye taarifa yao.

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG] ni kutokukopesha "diploma holders" wanaojiunga na degree. Bodi haijatoa sababu kwanini hili kundi halikopeshwi. Hivi bado tuna ile assumption kwamba diploma wanaojiunga vyuo vikuu wote ni "in service?" Hivi bodi haijui kwamba kuna diploma holders wana miaka 20, 21, 22 or 23 na hawana uwezo wa kujilipia?

Yani mtu akiwa na diploma anapoteza sifa za kukopesheka hata kama anakidhi vigezo vingine vyote. Kwa mfano kama mwanafunzi ni yatima, hana ndugu wenye uwezo wa kumsomesha, na amechaguliwa kujiunga chuo kikuu kwa alama nzuri, as long as ni diploma holder hakopesheki. Kwangu mimi naona huu ni ubaguzi. Ni vema bodi ije na majibu yanayoingia akilini kwanini hawakopeshi diploma holders?

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]: Ni wanafunzi wenye umri wa miaka 30 na kuendelea kutopewa mikopo. Katika kureview vigezo vyao bodi imesema mwanafunzi yeyote mwenye umri wa miaka 30 au zaidi hatapewa mkopo wa elimu ya juu. Euther awe ametoka form six au ni diploma holder but as long as ana miaka 30 mkopo asahau.

Maana yake ni kwamba hata kama umepata division 1 ya 3 masomo ya sayansi (eg PCB) ukachaguliwa kusoma degree ya sayansi, (lets say MD pale MUHAS), halafu wewe ni yatima, lakini as long as una miaka 30 sahau kuhusu mkopo. Inabidi ujisomeshe mwenyewe.

Nadhani hapa bodi wanalazimisha watu kufoji umri. Mtu aliyezaliwa 1987.aseme kazaliwa 1992 ili tu apate mkopo. Nadhani Bodi wanatakiwa kuja na majibu ya kueleweka ni kwanini wanafunzi wenye miaka 30 hawakopesheki?

Wapo wabunge, na mawaziri na wanataaluma (wengine maprofesa) ambao walijiunga na elimu ya juu wakiwa na miaka 30 au zaidi. Na serikali haikua na ajizi ikawasomesha wote. Leo wengine ni maprofesa, wengine mawaziri (ninayo orodha ya baadhi yao). Lakini haohao leo wanaweka vigingi wenzao wasipite kwenye njia ambazo wao walipita. Najatibu kutafakari kama Nyerere nae angeweka kigezo cha umri chuo kikuu kuna maprofesa na mawaziri ambao leo sijui wangekua wapi.

Kwa maoni yangu vigezo hivi viwili vya bodi ni vya ubaguzi. Tuwe na vigezo ambavyo vitaweka fair competition baina ya wanafunzi wote wanaoomba mkopo. Mtu akikosa awe kweli hajatimiza vigezo. Lakini kusema sijui miaka 30, sijui diploma sikubaliani navyo. Unless Bodi watoe ufafanuzi wa kueleweka kwamba ni kwanini diploma? Ni kwanini miaka 30??

Malisa GJ
 
yaani nashindwa hata kuelewa hivi hivyo ni vigezo au ubaguzi, tuache siasa serikali inatubagua kwa kweli duu
 
Nashukuru kamanda wamrchanwa live bungeni kama wamefilisika na watatumiamiujiza gani kugawa izo millioni 50 kila kijiji wakadai kuwa kuwa tayari fedha hzo zipo kwenye mchakato; nakaribia mwaka uishe ngoja tunyamanze tuu coz vitisho inbox vimeanza
 
kwanini hawakuvitoa mwanzo ili wasiokidhi wasitumie gharama zao,? au walikuwa wanazikusanya zakuanzia kukopesha?
 
kwanini hawakuvitoa mwanzo ili wasiokidhi wasitumie gharama zao,? au walikuwa wanazikusanya zakuanzia kukopesha?
hapo tu mimi ndo naumia nikikumbuka tabu niliyopata kwanza pesa ya kuapply huo mkopo ilikuwa shughuli bs 2 Mungu alisaidia now wanasema hatupewi kwanin wasingesema mapema kabla atujapoteza pesa zetu
 
bado nalia na utumbo walioufanya tcu na mwenzake nacte kwanini sasa wasiwape nafasi walio na hizo gpa ya 2.7-2.9 waendelee na degree sasa wao wamepandisha ma vigezo uku mkop wenyew hamna wapo wenye uwezo wa kujilipia kila kitu ila majipu hayawezi kuisha kwa stairi hii...................................
 
Dah mie ni diploma holder ni mezaliwa 27/12/1987 sijui kama mwaka kesho nitafikiliwa mkopo?
 
kama una diploma ni halali kunyimwa mkopo because unakopesheka na taasisi nyingi kama PSPF etc ......labda kama haufanyi kazi serikalini ndo inakula kwako
 
Back
Top Bottom