Kwa mujibu wa ukurasa wa serikali ya Tanzania (Tanzania Government) kwenye facebook Mh Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Bw. Diodorous Kamala ni miongoni mwa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kwenye mahafali itakayofanyika 'kesho'.
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa Ndugu Kamala (Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Nkenge na Waziri wa Zamani wa Afrika mashariki) tayari alishakuwa "Dokta" na amekuwa akifahamika hivyo sawa na rafiki yake wa siku nyingi Ndugu Emmanuel Nchimbi (PhD).
Swali la msingi ni lini Kamala alipata shahada ya Uzamivu (PhD) kiasi cha kustahili kuitwa Dokta? Na je kama hakuwa Dokta (naamini hivyo vinginevyo asingekuwa ana graduate kesho) ndio kusema alikuwa nanalipwa mshahara asiostahili akiwa Mhadhiri pale Mzumbe wakati stahili yake ikiwa ni Mhadhiri Msaidizi? Na je hizi sifa za kitaaluma si ndio zilizombeba mpaka kuwa Mbunge mwaka 2005? Je, ni adhabu gani kisheria anapaswa kupewa mtu ambaye amedanganya kuhusu taaluma yake? Huyu ana tofauti gani na aliyekuwa Mbunge wa Temeke ndugu Kihiyo ambaye alivuliwa ubunge kwa kudanganya elimu yake?
Ni miaka kama miwili hivi iliyopita aliibuka Mtu anayeitwa Kainerugaba Msemakweli na orodha yake ya mafisadi wa Elimu ambapo pamoja na watu wengine Dk Kamala, Nchimbi, Makongoro, Mary Nagu na Lukuvi walitajwa kwamba hawakuwa na sifa za kielimu zilizokuwa zinaonyeshwa kwenye tovuti ya Bunge na baadhi yao akiwemo Mh Balozi Kamala walitishia kwenda mahakamani kitu ambacho hawajakifanya mpaka leo.
Waheshimiwa wakiongozwa na Mh Kamala wana uhalali bado wa kuendelea na nyadhifa zao kwa kashafa hii?
Post kwenye ukurasa wa serikali kwenye facebook

"PONGEZI KWA WAHITIMU CHUO KIKUU MZUMBE.
3,050 Kuhitimu kesho wakitunukiwa Degrees kwenye maafali ya 11, katika Chuo kikuu cha Mzumbe. Kati ya hao, yupo balozi wetu anayetuwakilisha nchini Ubelgiji(Belgium) Mhe. Diodorus Kamala.
Mungu awaongoze katika kulijenga Taifa letu"