Diodorous Kamala kupata PhD kesho - Alikuwa Dokta feki?

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,928
2,000
Kwa mujibu wa ukurasa wa serikali ya Tanzania (Tanzania Government) kwenye facebook Mh Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Bw. Diodorous Kamala ni miongoni mwa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kwenye mahafali itakayofanyika 'kesho'.

Kama kumbukumbu zangu ziko sawa Ndugu Kamala (Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Nkenge na Waziri wa Zamani wa Afrika mashariki) tayari alishakuwa "Dokta" na amekuwa akifahamika hivyo sawa na rafiki yake wa siku nyingi Ndugu Emmanuel Nchimbi (PhD).

Swali la msingi ni lini Kamala alipata shahada ya Uzamivu (PhD) kiasi cha kustahili kuitwa Dokta? Na je kama hakuwa Dokta (naamini hivyo vinginevyo asingekuwa ana graduate kesho) ndio kusema alikuwa nanalipwa mshahara asiostahili akiwa Mhadhiri pale Mzumbe wakati stahili yake ikiwa ni Mhadhiri Msaidizi? Na je hizi sifa za kitaaluma si ndio zilizombeba mpaka kuwa Mbunge mwaka 2005? Je, ni adhabu gani kisheria anapaswa kupewa mtu ambaye amedanganya kuhusu taaluma yake? Huyu ana tofauti gani na aliyekuwa Mbunge wa Temeke ndugu Kihiyo ambaye alivuliwa ubunge kwa kudanganya elimu yake?

Ni miaka kama miwili hivi iliyopita aliibuka Mtu anayeitwa Kainerugaba Msemakweli na orodha yake ya mafisadi wa Elimu ambapo pamoja na watu wengine Dk Kamala, Nchimbi, Makongoro, Mary Nagu na Lukuvi walitajwa kwamba hawakuwa na sifa za kielimu zilizokuwa zinaonyeshwa kwenye tovuti ya Bunge na baadhi yao akiwemo Mh Balozi Kamala walitishia kwenda mahakamani kitu ambacho hawajakifanya mpaka leo.

Waheshimiwa wakiongozwa na Mh Kamala wana uhalali bado wa kuendelea na nyadhifa zao kwa kashafa hii?

Post kwenye ukurasa wa serikali kwenye facebook

"PONGEZI KWA WAHITIMU CHUO KIKUU MZUMBE.

3,050 Kuhitimu kesho wakitunukiwa Degrees kwenye maafali ya 11, katika Chuo kikuu cha Mzumbe. Kati ya hao, yupo balozi wetu anayetuwakilisha nchini Ubelgiji(Belgium) Mhe. Diodorus Kamala.

Mungu awaongoze katika kulijenga Taifa letu"
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,863
2,000
Huyu jamaa ni tapeli wa kawaida ambaye alighushi udaktari. Hata alipodaiwa kuwa alighushi hakukanusha zaidi ya kutoa vitisho ambavyo hata hivyo hakuvitekeleza.

Yeye na akina Mary Nagu, Makongoro Mahanga, Didace Masaburi, na Emanuel Nchimbi ni vihiyo wa kawaida wanaopenda kuitwa madaktari wakati siyo. Shame on them all! Hii ni mara ya pili kusikia kuwa mhusika mwingine anapata PhD toka Mzumbe.

Hata Nchimbi alifanya hivyo hivyo baada ya kustukiwa. Je Mzumbe ni kiwanda kingine cha kutengeneza PhDs fake? Kuna haja ya kuitafiti zaidi.
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,863
2,000
Mwanangu SGB wengine wanaziita voda fasta. Kesho tutasikia wakiziita jiko la mchina. Si unajua tena. Kweli nchi yetu imebakwa kweli kweli.
 
Mheshimiwa Mwl Steve

Senior Member
Nov 3, 2012
139
0
Huyu jamaa ni tapeli wa kawaida ambaye alighushi udaktari. Hata alipodaiwa kuwa alighushi hakukanusha zaidi ya kutoa vitisho ambavyo hata hivyo hakuvitekeleza. Yeye na akina Mary Nagu, Makongoro Mahanga, Didace Masaburi, na Emanuel Nchimbi ni vihiyo wa kawaida wanaopenda kuitwa madaktari wakati siyo. Shame on them all! Hii ni mara ya pili kusikia kuwa mhusika mwingine anapata PhD toka Mzumbe. Hata Nchimbi alifanya hivyo hivyo baada ya kustukiwa. Je Mzumbe ni kiwanda kingine cha kutengeneza PhDs fake? Kuna haja ya kuitafiti zaidi.

Nchi inatawaliwa kimagumashi,rais anachekelea kuitwa dakt bila ya kuwa hata na master.Kwa nin akina kamala na nchimbi wenye digree feki za uzamili wasijiite wenye digrii za uzamivu kwenye nchi ya magumashi.Huu ni mwendelezo wa maajabu ktk elimu ya Tz ambapo watoto wanafaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi bila kujua kusoma na kuandika.Naibu waziri wa elimu kujigamba kwamba tanzania ni muungano wa visiwa vya pemba na zimbabwe vilivyoungana mwaka 11964 na tanganyika Sishangai siku ukiambiwa tuwa tunasoma kinyumenyume yaani unanzia chuo kikuu then sekondari,msingi then chekechea.NDICHO WANACHOKIFANYA AKINA NAGU,NCHIMBI,KAMALA &CO. Nashangaa wanazuoni wapo tu wakati elimu inadhalilishwa kiasi hicho
 
Huna haja ya kuwalaumu wanazuoni iwapo madaraka yamo mikononi mwa wapumbavu. Again the price a good person can pay is his or her silence when evil people rule. Wanazuoni wetu nao wamechakachuliwa. Nenda chuo kikuu cha Manzese (UDSM0. Utakuta wasomi wengi wakihenyeshwa na ufugaji wa kuku nguruwe huku wake zao wakiuza vitumbua. Ni kweli nchi yetu imebakwa na kutekwa na manyang'au. Tusipobadilika na kufanya nchi isitawaliwe tungoje wajuu na vitukuu vyetu wakojolee makaburi yetu.
 
Mtoto wa tembo

Senior Member
Oct 4, 2012
198

hii ni kweli kabisa,hebu tutafakari hili jamani.wata hani kaburi kwa lipi jema??
 
usungilo

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
527
500
Mzumbe chuo kilichogeuka sehemu ya kutoa degree feki. Ni bora ilivyokuwa IDM lakini sasa hivi imegeuka janga la taifa.
 
Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,640
2,000
Huna haja ya kuwalaumu wanazuoni iwapo madaraka yamo mikononi mwa wapumbavu. Again the price a good person can pay is his or her silence when evil people rule. Wanazuoni wetu nao wamechakachuliwa. Nenda chuo kikuu cha Manzese (UDSM0. Utakuta wasomi wengi wakihenyeshwa na ufugaji wa kuku nguruwe huku wake zao wakiuza vitumbua. Ni kweli nchi yetu imebakwa na kutekwa na manyang'au. Tusipobadilika na kufanya nchi isitawaliwe tungoje wajuu na vitukuu vyetu wakojolee makaburi yetu.

Aisee sasa saa ngapi atapata muda wa kupiti assignment na kusahihisha test maana yupo busy na shughuli zingine za kiuchumi kutokana na kutelekezwa.
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,863
2,000
Aisee sasa saa ngapi atapata muda wa kupiti assignment na kusahihisha test maana yupo busy na shughuli zingine za kiuchumi kutokana na kutelekezwa.

Mwanangu Jadoki Kalimilo usijisumbue kufikiria assignments. Wenzako wanapewa kila upendeleo hata kwenye marking. Wanachofanya ni kujisajili chuoni na kazi wanafanya wengine. Nchi yetu imechakachuliwa kulhali.
 
Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,640
2,000
Mwanangu Jadoki Kalimilo usijisumbue kufikiria assignments. Wenzako wanapewa kila upendeleo hata kwenye marking. Wanachofanya ni kujisajili chuoni na kazi wanafanya wengine. Nchi yetu imechakachuliwa kulhali.

Hili linajulikana, hakuna kufeli kwa hawa watu na walivyo busy huo muda wa kusoma PHD sijui kama wanao kwani hiyo masters tu kuna wananchi wengine inawapeleka puta kukamilisha research sasa hawa wazee wa muda mwingi wapo majukwaani, ila sijasikia ya Magufuli nadhani yeye ya kwake ipo safi
 
muhogomtamu

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
412
195
Nikusahishe kidogo mkuu, mahafali ni tarehe 7 Ijumaa na sio kesho (alhamisi) na kwa taarifa sahihi nilizonazo, kesho kutakuwa na convocation ambapo wahitimu na wahadhiri mbalimbali watapewa pia zawadi za kufanya vizuri katika academia kwa mwaka huu wa masomo! Kwa hiyo kwa ajili ya kumbukumbu na kutowachanganya watu, MAHAFALI , TENA YA MAIN CAMPUS MOROGORO NI TAREHE 7, IJUMAA.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom