Dini zimechangia kudumaza ufahamu wa mwafrika

Andrew Tate

JF-Expert Member
Jun 28, 2020
3,824
5,811
Straight to the topic.

Africans wengi wanaamini kwenye dini kuliko chochote kile hapa duniani.

Na watu wanaomini kwenye dini wanaamini wapo hapa duniani ili kumuabudu mungu tu na si kingine.

Well hapa kwetu africa kuna dini kubwa mbili yaani uislamu na ukristo.

Na kwenye hizo dini kubwa mbili kila mtu anajiona yuko sahihi na kitabu chake ni sahii na dini ndio sahihi.
Na dini nyingine zaidi ya kwake ni ya uongo wala si ya kweli.

Cha ajabu hizi dini sio za africa bali zinatoka nje ya africa. Unaona akili ya mwafrika ilivyo hapo?

Na cha kushangaza zaidi hizi dini kwa karibu asilimia 90% zinatoka kwa wakoloni walioivamia africa.

Na sio wakoloni tu waliotukandamiza watu weusi, hapana hata hizo dini zimekandamiza watu weusi.

Na bila shaka hizo dini zilikuwa na mipango ya muda mrefu kuanzia miaka 100 mbele ili zifanikiwe na kweli zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Kumbuka ukitaka kumteka mtu kwenye kila kitu basi anza kumteka ufahamu wake.

Dini za wakoloni ndio chanzo mojawapo leo tuko hapa.

**********

Binadamu unatakiwa uwe na uwezo wa kujitambua na kujielewa ili kuepuka kuendeshwa na hisia ila ukishindwa kujitambua na kujielewa basi tegemea uwe controlled na hisia na hiyo ni sign ya ukosefu wa hivyo vitu hapo juu na vingine vya ziada yaani

=Kujitambua
=Kujielewa


Unajua kuna vitu vya kuchagua na kuvifanya au kuvitenda na kuna vitu vya kuacha. Hayo yote yanategemea na ufahamu wako.

Sasa huyu muafrika kwa yote yale aliyofanyiwa kuteswa, kudhihakiwa, kudharirishwa na mengine mengi mabaya.
Still mwafrika huyu alikubali kupokea dini hizi za mkoloni na kukubali kuwa ndio ufahamu wake na kila kitu kwenye hiyo dini kipo sahihi na hatoruhusiwa kupinga au kuhoji chochote juu ya hiyo dini au atalaaniwa.

Mwafrika huyu mweusi amekubali kupokea dini ambayo.
=Amepewa na watu weupe waliomfanyia kila aina ya ubaya na ukatili.
=Kila mtume kwenye hizo dini ni mweupe
=Hata mungu wa kwenye hizo dini katuma watu weupe waje kutangaza hizo dini weusi sijui kwanini kawaacha
=Alikubali kupokea dini ambazo mtu mweusi ni nembo ya shetani na nyeupe ni nuru ya malaika.
(Huo ni ubaguzi pure)
=Dini ambazo inasema mweusi amelaaniwa nk

Hapohapo Yaani mwafrika yupo tayari
=Akuue
=Akutukane
=Akudharirishe
=Akudharau
=Akupige
=Akudhihaki au chochote kile kibaya mwafrika atamfanyia mwafrika mwenzake sababu ya dini aliyopewa na mtu aliyemtesa, kumtukana, kumdhihaki na kumdharirisha.

Still mwafrika mweusi huyohuyo anaamini yeye amelaaniwa kwa rangi yake na yeye si chochote mbele ya mweupe kwani mweupe amebarikiwa.
Hapo hakumbuki kama hiyo dini kampa huyohuyo mweupe aliyemtesa na kumpiga mijeredi ya mgongo ili asiangushe pembe za tembo.

Yes huyo ndio mwafrika wa africa usijali hata humu watajitokeza watu kama hao. Asilimia kadhaa za hao watu wapo humu jf.

Na hapo mwafrika huyo bado ataendelea kumchukia mwafrika wa dini nyingine kivyovyote vile.

*******

Labda mababu zetu walikosa hivyo vitu yaani kujielewa na kujitambua hivyo wakawa wanaendeshwa na hisia bila wao kujua hivyo ikawafanya wasie na akili wala maarifa ya kueleweka.
Lakini binadamu anabadirika kadri muda unavyozidi kwenda
Hivyo hata sisi tunaweza kubadirika na kuanza kujitambua na kujielewa na sio kuendeshwa na hisia tena au Africans itakuwa ngumu kubadirika.

kila kitu kimerahisishwa na hao wazungu ambavyo si vya kupotosha na kukandamiza kama dini hivyo tunaweza kutumia hivyo vitu vizuri kuweza kubadirika na kujiongeza na sio kuendelea kubomoka.

Kumbuka nilikwambia binadamu anatakiwa awe na sifa ya kujitambua na kujielewa ili aisendeshwa na hisia au imani hivyo ni lazima kujua kipi cha kuchukua na kuacha na sio kupelekeshwa kama fuso bovu na hizo hisia kama mababu zetu waliokubali hizi imani.

*******

SASA HII IMEATHIRI VIPI UFAHAMU AU UBONGO WA MWAFRIKA.

=Well baada ya hapo mwafrika akawa muoga wa kuhoji "kwanini. sababu ya kuogopa kukufuru na kulaaniwa alafu alishaalaniwa mara kwanza.
=Mwafrika akawa mvivu wa kufikiri kwa kusema kila kitu anapanga mungu hivyo huyo mwafrika kubweteka chini akitegemea mungu atamfanya apate anachokitaka huku amekaa tu chini ya mwembe. Hadi leo hawa watu wapo na ndio masikini wa kwanza yaani mafukara.
=mwafrika huyu anaamini wazungu ndio wamebarikiwa na ndio maana wameendelea.
=mwafrika ubongo wake wote umelala sababu ameaminishwa yeye si chochote kwani amelaaniwa na ndo maana rangi yake nyeusi.
=mwafrika anaamini duniani anapita tu na yupo hapa kumuabudu mungu tu.
Hivyo huyo mwafrika kuendelea kufa masikini na kuendelea kuishi na changamoto sababu yeye kaja kumuabudu mungu tu na kuijaza dunia na si kingine wakati huo weupe wakiendelea kukua kila siku.
=Mwafrika anaogopa kutumia na kutegemea ufahamu wake sababu dini imemwambia asitumie ufahamu wake sababu mungu yupo.
Na anashindwa kujiuliza vitu vyote anavyotumia vimetokana na ufahamu.
=Na watu kugombana sababu ya dini iliyoletwa na weupe hata huyo mweupe akiona anaweza shangaa akili zao zilivyo za ajabu hao Africans wakimpigania mtume mweupe wa kwenye kitabu.

Na mpaka leo africa hatuna kitu ambacho kimetokana na sisi wenyewe, labda kama wangetuacha kipindi kike labda tungechelewa lakini tungepata ufahamu taratibu kuliko kutuharibu kabisa na hizi dini.

Mbona china wana dini zao lakini wana maendeleo makubwa sana na ni wamoja tena wana ufahamu mkubwa ukilinganisha na sisi.

Africans hatuna umoja wala ushirikiano sababu tunachukiana na kubaguana kidini kwa dini ambazo zililetwa na watu kutoka nje kitu ambacho ni ujinga.

Najua wengi mmerukia mwisho sababu ndio tabia zenu za kutokupenda kushughulisha vichwa vyenu.
Sasa nakuambia popote utakapomtukana mtu yoyote sababu ya tofauti za kidini basi tambua hiyo dini si asili yako bali ulipewa na mweupe ili apate kukuendesha na kukucontroll so think again.

Nadhani baada ya hapo tutaacha kutukanana, kudhihakiana, kudharauriana, kubaguana sababu ya dini na hapo ndio mwanzo wa kujitambua.

na wote kuwa kitu kimoja kitu ambacho hakiwezekani.
 
Tafadhali naomba urekebishe mada yako, ukristo sio dini. Kwaza kabisa kristo ni Mungu mtu. Ukristo ni Imani ya kuamini katika kristo. Dini ni mfumo,taratibu,sheria na kanuni anuai zinazoendesha imani ya kikristo
Wewe ni nani jf wa kuniambia mimi nirekebishe mada yangu?

Una mamlaka yoyote kuniambia hivyo?
Unadhani kwanini mods wameipitisha?
 
Ninukuu maneno ya rais Xi Jin Ping

1. The only thing black man has inherited from Arab and European colonization is the religion that he practices and that’s exactly what the colonizers wanted.2. Notice that in black countries, the education is a disaster, the administration is corrupt, health is deplorable, but relagion is doing wonderfully well.

3. Black people rebels against everything Except religion. They even think they are more religious than those who brought them this concepts and that the colonizers are not good Christians.

4. Black people even claimed themselves to be original race of which JESUS Christ has descended. This is how black people stupidity can go.

5. Notice that any society that is full with superstitions. Religious indoctrination, lack of education and nationalism, is always ridden with violence.

Tafsiri isiyo rasmi

1. Kitu pekee ambacho mtu mweusi amerithi kutoka kwa ukoloni wa Kiarabu na Ulaya ni dini ambayo anafanya na ndivyo haswa wakoloni walivyotaka. Ona kwamba katika nchi nyeusi, elimu ni janga, utawala ni rushwa, afya ni mbaya, lakini dini linafanya vizuri sana.

3. Watu weusi wanaasi kila kitu Isipokuwa dini. Wanafikiri hata wao ni waumini kuliko wale waliowaletea dhana hizi na kwamba wakoloni sio Wakristo wazuri.

4. Watu weusi hata walidai wenyewe kuwa ni jamii asili ambayo YESU Kristo ameshuka. Hivi ndivyo upumbavu wa watu weusi wanaweza kwenda.

5. Ona kuwa jamii yoyote ambayo imejaa ushirikina. Ufundishaji wa kidini, ukosefu wa elimu na utaifa, daima hujaa vurugu.

Haya maneno yanafikirisha sana
 
Sijakukosoa nimekurekebisha, elewa context ya maneno yangu.
Habari za uzi wangu tuziache, Wewe unaweza kuupoteza muda wangu au mm kupoteza muda wako?? Ajabu hii ndio nasikia kwako. Explain me how can you

Wee jamaa unjikutaga great thinker kumbe huna lolote. Nilikuwaga nakudhania hivyo zamani lkn nilipokugundua nikakudharau mazima
 
You're troubled, can't deal with emotionally and Mentally troubled people.
I'm Out mate, Peace ✌✌
Mkuu mbona unanisikitisha sana?

Signature yako ndiyo inayoonesha wewe ndiye mwenye matatizo ya emotionally and mentally hata mada zako nyingi zinaonesha hivyo na michango yako mingi inaonyesha ni mtu anayetafuta huruma ya watu wengine na unajiona usiye na hatia.

Wewe mwenyewe umeshajiita worthless useless and stupid person sasa mimi nishajua kwanini umeniita emotionally and mentally troubled sababu hayo matatizo ni yako na unadhani kila mtu anayo.

Hivyo mimi sio kama wewe mkuu ugua pole.
 
Mkuu Da'Vinci kama umeshindwa kuelewa kitu kidogo kama "kupotezeana muda" sasa una uhakika gani wa kuelewa msingi wa mada yangu nzima?

Hapa ninapotype natumia muda wangu hivyo siwezi nikatumia 20minutes straight kubishana mambo ambayo hayana maana wala msingi wenye mantiki.
 
Siyo kweli, kwa mfano Tanzania Ukristo una miaka 100-150 tu, kabla ya hapo mbona hakukuwa na hayo maendeleo? Isitoshe kama yangekuwepo tusingetawaliwa, usisahau Shule za kwanza kama tuzijuavyo leo hii zilijengwa na watu wa Dini, pia Wamasai wengi hawana Dini ua Kiabrahamu mbona hawana hayo maendeleo?
 
Dini ni mifumo ya wanadamu waliyo ibuni pia dini haijakataza watu kufanya maendeleo, Africa tujilaumu kwa ujinga wetu tusisingizie dini kabisa tujilaumu wenyewe, mfano ufisadi, ujinga maradhi na huduma muhimu za kijamii kushindwa kuxitekeleza hapo dini imeingia vipi?
 
Siyo kweli, kwa mfano Tanzania Ukristo una miaka 100-150 tu, kabla ya hapo mbona hakukuwa na hayo maendeleo? Isitoshe kama yangekuwepo tusingetawaliwa, usisahau Shule za kwanza kama tuzijuavyo leo hii zilijengwa na watu wa Dini, isitoshe Wamasai wengi hawana Dini ua Kiabrahamu mbona hawana hayo maendeleo?
Mada ifungwe tu Sasa maana umemaliza
 
Mkuu safuher post yako uliyofuta dk20 nyuma uliandika

"mada refu sana hivyo huwezi kusoma yote watu wanarukia kwenye point sababu uzi mzima nimeongelea kitu kimoja"

Sasa kama hujasoma yote umejuaje nimeongelea kitu kimoja na mada yenyewe hujaisoma yote?
Na utalukiaje point kama hujui msingi wa mada?

Najua waafrika ni wavivu kusoma vitu virefu.
 
Mkuu safuher post yako uliyofuta dk20 nyuma uliandika

"mada refu sana hivyo huwezi kusoma yote watu wanarukia kwenye point sababu uzi mzima nimeongelea kitu kimoja"

Sasa kama hujasoma yote umejuaje nimeongelea kitu kimoja na mada yenyewe hujaisoma yote?
Na utalukiaje point kama hujui msingi wa mada?

Najua waafrika ni wavivu kusoma vitu virefu.
Kumbe na wewe una shida ya kusoma kisichoandikwa.

Sijasema "umeandika kitu kimoja"

Unazua tu sikuandika hivyo.

Kumbe mbali na kukubali dini mtu anaweza kuwa na mashaka kama haya
 
Siyo kweli, kwa mfano Tanzania Ukristo una miaka 100-150 tu, kabla ya hapo mbona hakukuwa na hayo maendeleo? Isitoshe kama yangekuwepo tusingetawaliwa, usisahau Shule za kwanza kama tuzijuavyo leo hii zilijengwa na watu wa Dini, pia Wamasai wengi hawana Dini ua Kiabrahamu mbona hawana hayo maendeleo?
Kabla ya hiyo miaka Africa mlikua manaabudu dini ya mizimu ambapo mzungu akaja kuiharamisha kua ni upagani akawafanyia updtate kwa kuwaletea dini ya mungu wa kizungu

Asilimia kubwa ya jamii inayoishi maporini au mapangoni bado wana system hii ya kuabudu dini ya mizimu hata hao wamasai huko maporini bado wanaienzi
 
Mkuu safuher post yako uliyofuta dk20 nyuma uliandika

"mada refu sana hivyo huwezi kusoma yote watu wanarukia kwenye point sababu uzi mzima nimeongelea kitu kimoja"

Sasa kama hujasoma yote umejuaje nimeongelea kitu kimoja na mada yenyewe hujaisoma yote?
Na utalukiaje point kama hujui msingi wa mada?

Najua waafrika ni wavivu kusoma vitu virefu.
Nimekuuliza dini inakatazaje watu au inazuiaje watu kufikiria kutengeneza magari ya kisasa ama kuvumbua vifaa mbalimbali vya technolojia vya kisasa ?

Mwafrika kadumazwa kivipi ?
 
Siyo kweli, kwa mfano Tanzania Ukristo una miaka 100-150 tu, kabla ya hapo mbona hakukuwa na hayo maendeleo? Isitoshe kama yangekuwepo tusingetawaliwa, usisahau Shule za kwanza kama tuzijuavyo leo hii zilijengwa na watu wa Dini, pia Wamasai wengi hawana Dini ua Kiabrahamu mbona hawana hayo maendeleo?
Wamasai wengi wangapi mkuu?
Mimi nimechukulia asilimia kubwa ya waafrika ndio inayomatter.

Sijakataa kabla ya dini za kikoloni kulikuwa hakuna maendeleo.
Lakini nadhani kama wakoloni wangetuacha bila dini bila shaka tusingekuwa hivi tulivyo leo hata kama bila ya maendeleo at least tungekuwa na umoja ambao ndio kila kitu na sio jinsi tulivyo leo na matabaka ya kuchukiana.
Na pia tusingekuwa na limited mind zilizo jificha kwenye vitabu vya dini.

dini na hata huo mfumo wa elimu ni chanzo cha mengi niliyoyaweka kwenye uzi ikiwemo huo umasikini, chuki, uvivu wa kufikiri na kubaguana wenyewe kwa wenyewe.
 
Mimi nimechukulia asilimia kubwa ya waafrika ndio inayomatter
Kwa hiyo unataka kutuambia dini ili ilemaze na kumtia mtu ujinga basi lazima dini hiyo ipokelewe na watu wengi saaaaaana ?

na sio kwamba inatosha kwa mtu mmoja kuathiriwa na fikra za dini hiyo na kumdumaza endapo ataiamini ?
 
Nimekuuliza dini inakatazaje watu au inazuiaje watu kufikiria kutengeneza magari ya kisasa ama kuvumbua vifaa mbalimbali vya technolojia vya kisasa ?

Mwafrika kadumazwa kivipi ?
Hayo nimeandika kwenye uzi na wewe uliniambia huwezi kusoma uzi wote.

Bahati mbaya Mimi sina muda wa kupoteza kuelezea vitu ambavyo nimeshaelezea.

Soma uzi wote.
 
Wamasai wengi wangapi mkuu?
Mimi nimechukulia asilimia kubwa ya waafrika ndio inayomatter.

Sijakataa kabla ya dini za kikoloni kulikuwa hakuna maendeleo.
Lakini nadhani kama wakoloni wangetuacha bila dini bila shaka tusingekuwa hivi tulivyo leo hata kama bila ya maendeleo at least tungekuwa na umoja ambao ndio kila kitu na sio jinsi tulivyo leo na matabaka ya kuchukiana.
Na pia tusingekuwa na limited mind zilizo jificha kwenye vitabu vya dini.

dini na hata huo mfumo wa elimu ni chanzo cha mengi niliyoyaweka kwenye uzi ikiwemo huo umasikini, chuki, uvivu wa kufikiri na kubaguana wenyewe kwa wenyewe.


Ethiopia haijatawaliwa na Mkoloni yoyote yule na wameachwa kama unavyosema, sasa wako kimaendeleo?
 
Back
Top Bottom