Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Wakati wamisionari walipoleta ukristo barani Afrika na waarabu walipoleta uislamu, hakukuwa na usafiri wa ndege. Hakukuwa na Emirates wala KLM. Wazungu na waarabu hao walikuja kwetu na majahazi. Tuliupokea utamaduni mgeni kwenye maisha yetu, tukajifunza mpaka tukazielewa tamaduni na mafundisho ya dini hizi.
Imepita miaka mingi, tumegeuka kuwa wajuzi wa dini hizi, kiasi cha kuikana asili yetu yote. Tumekuwa wataalam wa dini hizi kiasi cha kutoana ngeu kwa kisingizio cha mambo ya kiroho yameguswa. Waasisi wa nchi hii waliona mbali sana waliposema nchi haina dini ingawa watu wake wanazo dini. Lengo lilikuwa ni kuondoa tabia ya watu kutafuta uhalali kwa kutumia kigezo cha ufuasi wa dini. Waasisi walitumia busara ya kuua uchifu ili jamii itakayojengwa iweze kuwa ni ile iliyochangamana. Na somo la kutanguliza utu wetu badala ya kutanguliza dini na kabila la mtu, lilikuwa limetuingia vizuri sana, nikikumbuka wanafunzi niliosoma nao shule ya msingi na sekondari, nakuta kuwa majina yao ni mchanganyiko wa yale ya kiislam na kikristo.
Nakerwa sana na hii tabia ya mtu kujihalalisha kwa kutumia dini, ambayo ukichunguza sana utakuta haijui kulinganisha na wale walioleta Tanganyika wakiwa ndani ya majahazi. Kabla ya ujio wa dini za wazungu na waarabu, mababu na mabibi zetu walikuwa na ustaarabu wao wa maisha. Leo hii sisi wajukuu zao, tunaona kama vile ni kitu cha kujivunia kila mara tunapojitambulisha kidini huku tukiwa tayari kukashifu dini ya mtu mwingine, ingawa ukweli ni kuwa dini zote zililetwa na wakoloni, ambao kwa wao kuzileta kwetu, waliweza kutimiza malengo yaliyokuwa yamejificha ndani ya nafsi zao.
Waungwana dini hizi ambazo zinatufanya wakati mwingine tutukanane na kupeana majina ya kijinga, zililetwa na watu waliokuwa wamepanda majahazi ya mbao. Kwetu sisi kujifunza na kuzielewa, sio tiketi ya sisi kujifanya na wakristo zaidi ya wakristo waliotuletea ukristo. Kwetu sisi kujifunza na kuzielewa, sio kigezo cha sisi kujidai ni waislamu zaidi ya waislamu waliotuletea uislamu.
Hulka za kuendekeza chuki za kidini, zinaigawa nchi, hata siku moja haziwezi kuwa rafiki wa umoja wetu.