kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,622
- 14,069
Dini zetu hizi mbili zilikuja na wakoloni (watesi) wetu. Viongozi wa dini waliishi nyumba na mtaa mmoja na wakoloni (watesi) wetu, walisali pamoja, walikula na kunywa pamoja na wakoloni. Waliwabariki kwenye kazi zao za utesi na uporaji wa rasilimali zetu, kuwaombea mema na afya tele na kubatiza watoto wao. Wakoloni na dini ilikuwa ni kitu kimoja kilekile.
Viongozi wa dini walibaki wakati wenzao wakoloni wanaondoka shingo upande kurudi ulaya ili sisi tupate Uhuru.
Maswali ni mengi, lakini Yale machache ni haya:
1. Je, viongozi wa dini walifurahi au kuchukia wakati wakoloni wanaondoka?
2. Je, viongozi wa dini walifurahi Waafrika kujitawala?
3. Uhusiano kati ya dini hizi na wakoloni uliisha baada ya uhuru?
4. Viongozi wa dini waliomba msamaha kwa Waafrika kwa kishirikiana na wakoloni waliopora mali, kuua watu wetu, tamaduni zetu, na kudumaza maendeleo yetu?
View: https://youtu.be/BpswhiyKqpg?si=3vx7bzuU2k5j-Uys