Dini ni Utamaduni wa watu fulani

kufa,na hazikupata ujumbe wowote wa nabii issa,lau kama jamii hizi zingepata huo ujumbe wa nabii issa je ingekuwa ni wajibu kwao kufuata ujumbe huo au hata wangeuwacha wasingekuwa na dhima yeyote ?
Naona sasa mjadala umeisha, na bila shaka umekubali huu ni ummah, sasa suala la kukubali au kutokubali ujumbe, hakufanyi ya kuwa wao walifikiwa na ujumbe na jambo hili mimi wala wewe hakuna anayeweza thibitisha ya kuwa ujumbe wangeukubali au kinyume yake, na hii ni hoja mufulisi.

Sada hapo ndipo kunaingia jitihada za wanazuoni, na ndiyo maana wakaweka makundi matatu na mawili wakahukumu yanaenda motoni.
 
Hao wote walikuwa ni ahlul fatrah ndiyo maana imaam al Bukhari anaposema ahlul Fatrah ana maanisha watu ambao waliishi kipindi ambacho ni baina ya nabii Issa na Mtume Muhammad, ila kwa juhudi za wanazuoni na kuangalia mambo kiundani wakaweka mgawanyo huo.
Hao watu walioishia baina ya nabii issa na muhammad ina maana walifikowa na ujumbe wa nabii issa ambaye alikuweko kabla yao wakaukataa huo ujumbe ?

Ama hawakuupata kabisa huo ujumbe wa nabii issa ?

Na je wangeupata ingewawajibikia kwao kuufuata ?
 
Naona sasa mjadala umeisha, na bila shaka umekubali huu ni ummah, sasa suala la kukubali au kutokubali ujumbe, hakufanyi ya kuwa wao walifikiwa na ujumbe na jambo hili mimi wala wewe hakuna anayeweza thibitisha ya kuwa ujumbe wangeukubali au kinyume yake, na hii ni hoja mufulisi.
Kwa hiyo lau kama wangefikiwa na huo ujumbe na wakaukataa huo ujumbe siku ya kiama wangeadhibiwa kwa sababu walikataa ujumbe wa nabii issa ?
 
Tuchukue baada ya nabii issa mpaka kabla ya mtume huu ummah wa baada ya nabii issa tuwape jina la watanzania.

Sasa je hawa watanzania(walioishi baada ya nabii issa) waliupata ujumbe wa nabii issa wakauwacha kwa kuwa sio mtume wao?

Au hawakufikiwa kabisa na ujumbe wa nabii issa kwa maana ya kuwa ungewafikia ujumbe huo wangewajibika kuufuata ?
Nacheka sana, kwahiyo huu umekubali sasa ni ummah au bado ni kikundi cha watu...?

Kama ni ummah, hili limeisha na unitake radhi kwa kunipotezea muda kwa jambo hukuwa na elimu nalo.

Hili hakuna anaejua kamawangekubali au wasingekubali, ndiyo maana mtume akahukumu watapewa mtihani siku ya Qiyama.
 
Sada hapo ndipo kunaingia jitihada za wanazuoni, na ndiyo maana wakaweka makundi matatu na mawili wakahukumu yanaenda motoni
Wewe unadhani kuwa ni ahlul fitrah kwa sababu hawakupata ujumbe wa nabii issa ?

Au unadhani ni ahlul fitrah kwa sababu ujumbe uliwafika ila waliukataa kwa sababu nabii issa alishapita kitambo ?

Ukisema hawakufikiwa na ujumbe maana yake unakibali kuwa huo ujumbe wa nabii jssa nao uliwahusu ila haukuwafikia.

Au unakataa kuwa hao watu ujumbe wa nabii issa ikuwa hauwahusu hata kama ungewafikia walitakiwa waupuuze ?
 
Hao watu walioishia baina ya nabii issa na muhammad ina maana walifikowa na ujumbe wa nabii issa ambaye alikuweko kabla yao wakaukataa huo ujumbe ?

Ama hawakuupata kabisa huo ujumbe wa nabii issa ?

Na je wangeupata ingewawajibikia kwao kuufuata ?
Hili suala lingine mzee, halihusiani na mada yetu, hoja msingi ya umma imeisha.

Dini yetu haitaki kubahatisha ndiyo maana mtume akawataja watu aina nne watakso pewa mtihwni siku ya Qiyama.

Hili, limeisha.
 
Hili hakuna anaejua kamawangekubali au wasingekubali, ndiyo maana mtume akahukumu watapewa mtihani siku ya Qiyama.
Nimekuuliza hivi bwana mkubwa..

Hao watu wa baada ya nabii issa je ujumbe wa nabii issa lau ungewafikia je wangetakiwa waufuate au ule ujumbe wa nabii issa hauwahusu ?

Hakuna pahala nimesema ni ummah,bali wewe ndo wasema.

Jibu kwanza swala langu..

Watu wa baada ya nabii issa ule ujumbe wa nabii issa lau wangeupata ingekuwa ni wajibu kwao kuufuata au ingekuwa hiari kwa kuwa tu huyo nabii issa ni mtume wa nyuma ?
 
Hili suala lingine mzee, halihusiani na mada yetu, hoja msingi ya umma imeisha.

Dini yetu haitaki kubahatisha ndiyo maana mtume akawataja watu aina nne watakso pewa mtihwni siku ya Qiyama.

Hili, limeisha.
Hili suala lazma ulikwepe kwa sababu linakufunga mazima.

Bila shaka unakubali kuwa hao watu wangefikiwa na ujumbe wa nabii issa basi ingewalazimu kufuata,na huwezi kusema kuwa isingekuwa lazima kwao kufuata,hilo huwezi kusema.

Bali utakubaliana na mimi kuwa lau wangeupata huo ujumbe basi wangekalifishwa kuufuata,kama unabisha bisha hapa hadharani tuone.

Sasa hii ina maana ya kuwa watu hao walikuwa ni ummah wa nabii issa kwa sababu ujumbe wa nabii issa iwahusu na wao ila haukuwafikia kwa sababu mbali mbali.

Na hii ni dhaahiri sasa kuwa huo umma alitumwa nabii issa kwao lakini baadhi yao sasa hawakupata ujumbe huo wa nabii issa kutokana na sababu mbalimbali kama vile kupita kwa muda mrefu baina ya mtume na watu hao n.k

Nasubiri ubishe hili sauala la kuwa watu wa baada ya nabii issa wangeupata ujumbe wa nabii issa wangewajibika kuufuata,nasubiri ubishe hapo.

Na huwezi kubisha katu.
 
mkuu umeongea jambo kubwa sana hasa katika hiyo dua.

"ewe mola niruzuku elimu na uniruzuku ufahamu"

Mtu anaweza akawa na elimu ila akakosa ufahamu,na mtu anaweza kuwa na ufahamu ila akakosa elimu,hawa wote wanaweza kuharibu zaidi ikiwa watapishwa kuzungumza kwa ajili ya maslahi ya wengi.

Kinachotakiwa ni elimu na ufahamu.

Mtu anaweza kuwa na elimu ya hadithi lakini kuzifahamu ni shida,kuzifanyia bahthi na kuzichambua ndio tatizo wakati kauli za Allah na Mtume zinakusanya mafundisho mengi ambayo kama mtu hauna ufahamu utaona dhaahiri ya mambo tu.

Wakati zurri anasema kuwa afrika hakukuwa na Mtume ,uislamu unasema kila ummah ulikuwa na Mtume tena mitume laki na kitu.

Sasa mtu unajiuliza hawa laki na kitu ndo huku afrika hakukuwa na mtume kabisa ilhali hawa waafrika nao ni ummah wa watu ambao wanastahiki kupewa mitume ?

Utaona kuwa hapo panahitaji tafakkuri ya ndani sana kuzielewa aya na hadithi za mtume wetu muhammad.

Umegusia jambo zuri sana n muhimu mnoo bwana mokaze.

Mkuu Safuher, mimi sina chochote kabisa katika hiyo dua, hiyo dua ni kutoka kwa mwalimu wa waalimu, mtukufu wa daraja , kipenzi chetu, mtume Muhammad (saw), nilichofanya ni kumnukuu tu yeye, ni yeye ametufundisha tuwe tukiomba dua hiyo.

Yeye mwenyewe (kwa maana sisi sote) ameambiwa na Allah aombe dua hii:- رب زدنى علما, (Qur'an 20:114).

Hakika tunapaswa kumshukuru Allah kuwa kwetu Waisilamu pia tumshukuru zaidi kwa kutuletea Mtume (saw) na Qur'an.
 
unasemaje juu ya maswaa ambayo nimekuuliza mimi hko juu,unakuwa kama hujayaona alafu unataka nikujibu wakati na wewe hujibu.

Unauliza maana ya ustaarabu kwani wewe wakati unadai waarabu sio wastaarabu ulikuwa umeweka mfukoni maana ipi ya ustaarabu mkuu ?
Maswali yako yanaonesha unaongelea kitu kingine tofauti au tafsiri ya ustaarabu umeipundua kwa makusudi ili kuhalalisha unyama wa muarabu kwa watoto

Ustaarabu ni nini?

Kipi kipimo cha kujua huyu mstaarabu na huyu siye?
 
Mkuu umeandika kwa tahadhari kubwa ,unaweza kufunguka zaidi mkuu juu ya haya mas'ala tunyoyajadili hapa.

Umegusia suala la kumezeshwa elimu,hili jambo watu wengi tunalo sana zama hizi zetu pengine hata mimi sijasalimika nalo ktika baadhi ya maeneo.

Unaweza kufafanua zaidi juu ya mambo haya tunayojadiliana na bwana zurri hapa kuhusu kila ummah kupata mjumbe,bwana zurri anadai kwa kunukuu vitabu kuwa kuna ummah hazikupata mjumbe.

Una lolote la kuchangia katika hili mkuu ?
Itikadi ni kusadikishwa kimoyo, kifikra na kiakili. Muafaka huu hutegemea ni nani anayekunyweshwa jambo katika fikra mpaka kufikia hatua ya kuwa na uyakini usiyofikiwa na wasi wasi unafikia hatua ya kuuenzi na kuufanyia kazi.

Huu urithi ili ufanyie kazi sawa sawa unabidi upikwe na elimu ilyokuwa sawa sawa. Ukipikwa kinyume chake matokeo yake ni ghasia! Utakuwa na itikadi isiyotanguliwa na elimu yenye ufahamu.

Hii hali ndiyo anayo mkuu Zurri, yeye ameshapikwa hivyo na itikadi yake ndiyo ipo hivyo! Kikimjia chakula kingine itikadi aliyopikwa nayo inamwambia anatoka katika misingi hali ya kuwa si kweli. Laiti angelipikwa kwenye misingi elimu kama ilivyo maana na tafsiri ya elimu asingelikuwa kama alivyo.

Itikadi aliyopikwa nayo ndugu Zurri elimu aliyonayo yeye ndiyo sahihi na mafuhumu yake ndiyo yapo hivi nje ya mafuhumu hayo hakuna usahihi. Aliye hivi likiwekwa suala la elimu mezani mtajadiliana nini tena? Uyakinifu wake haukujengwa kielimu bali kuitikadishwa. Hili lipo hivi lipo hivi, basi hakuna jengine.

Mtu wa namna hii mizani yake ya kuyaendea kuyafikira masuala hayapo kieleimu bali yapo alivyoitikadishwa. Ndiyo maana hayupo kwa kuelewa bali yupo kukitetea kile alichopikwa nacho. Hafungui milango ya kuelewa bali anafungua milango ya kile alichoamnishwa! Kwa maana nyengine ufahamu wake umekatishwa tamaa ya kuwa nje ya hiki hakuna nje ya hiki.

Aliyepikwa hivi ukijadili naye kieleimu yeye haiangalii elimu. Yeye ataangalia itikadi yake. Ameaminishwa alichokuwa nacho ndicho aula! Kwa alichokielewa ndiyo sahihi zaidi mwengine anapwaya! Ndiyo maana ukijadili naye haleti ufahamu bali analeta nukuu ya kile alichoitikadishwa nacho chenye msimamo wa kwake.

Bila shaka ameaminishwa mafunzo ya Uislam marefu na mapana ni hayo aliyopewa. Ndiyo maana majibu yake ukiyaangalia yeye ni Akbar! Kwa maana usahihi ninao mimi. Lakini wewe ndugu Safuher upo kimsingi wa kielimu, kuwa huu ufahamu sawa umeuitakidi upo hivi kwa kuwa hiyo itikadi uliyoiweka hivyo ina misingi yake ya kielimu basi tuufikie kwa misingi yake ya kielimu.

Kwenye hili ambalo unajadiliana na ndugu Zurri njia ulizopita ndizo njia ninazopita mimi na umenipa faida nimejifunza mambo kutoka kwako! nimefaidika pakubwa sana kwa elimu uliyoitoa. Shukrani na Mungu akulipe kheri zaidi.

Zurri na Kiranga wametofautiana sehemu moja tu.
 
Hao watu wa baada ya nabii issa je ujumbe wa nabii issa lau ungewafikia je wangetakiwa waufuate au ule ujumbe wa nabii issa hauwahusu ?
Ungewafikia vipi wakati haukuwafikia, na hakutumwa kwao ? Katika dini hakuna kubahatisha, ndiyo maana wanazuoni wetu kuna maswali fulani hasa yakutunga huwa wanajibu kwa kusema hivi "Subirini kwanza jambo likitokea ndiyo mtuulize tuwape majibu".

Maana unaposeme "inge" na haikutokea huoni kama ni kupoteza muda na kuitumia akili vibaya ?
 
Hili suala lazma ulikwepe kwa sababu linakufunga mazima.

Bila shaka unakubali kuwa hao watu wangefikiwa na ujumbe wa nabii issa basi ingewalazimu kufuata,na huwezi kusema kuwa isingekuwa lazima kwao kufuata,hilo huwezi kusema.
Halinifungi kwa lolote na ni swali la kijinga sababu, haikutokea na mtume ameshapitisha hukumu.

Kwahiyo sijibu maswali ambayo kwa vyovyote hayabadilishi ukweli ulivyo.
 
Halinifungi kwa lolote na ni swali la kijinga sababu, haikutokea na mtume ameshapitisha hukumu.

Kwahiyo sijibu maswali ambayo kwa vyovyote hayabadilishi ukweli ulivyo.
Huwezi kujibu swali hilo mkuu na huwezi kukataa katu.

Hao watu walishushiwa mtume ambaye ni nabii issa lakini ujumbe wake tu haukuwafika na lau ungewafika wangekuwa wanakalifishwa na sheria hiyo.

Hakuna ummah ambao haukuwa na mtume bali kuna ummah ambao haukufikiwa na ujumbe wa Mtume,kila ummah una mtume.
 
Ungewafikia vipi wakati haukuwafikia, na hakutumwa kwao ?
Kama ni hivyo kwa nini wazazi wa mtume wako motoni,wao walifikiwa na ujumbe wa mtume gani mpaka iwe wako motoni ?

Kwa sababu wazazi wa Mtume ni katika watu wa zama za baada ya nabii issa na kabla ya mtume muhammad.

Sasa tuambie wewe kuwa hawa wazazi wa Mtume wako motoni kwa kosa gani wakati hawakuwa na mtume katika wakati wao ?
 
Maana unaposeme "inge" na haikutokea huoni kama ni kupoteza muda na kuitumia akili vibaya ?
Hauko sahihi mkuu..

Mbona mifano ya "inge" ipo mingi sana....

Angalia tu mpaka katika Qurani ipo mingi sana..

قُل لَّوْ شَاءَ اللَّهُ مَا تَلَوْتُهُ عَلَيْكُمْ وَلَا أَدْرَاكُم بِهِ ۖ فَقَدْ لَبِثْتُ فِيكُمْ عُمُرًا مِّن قَبْلِهِ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ

[ YUNUS - 16 ]
Sema: Mwenyezi Mungu angeli taka nisingeli kusomeeni, wala nisingeli kujuvyeni. Kwani nalikwisha kaa nanyi umri mzima kabla yake! Basi, je! Hamzingatii?

Unaona neni "angeli" hapo....

Hapo maana yake ni hoja kubwa hiyo kwamba lau Mungu ANGELITAKA msemaji asingewasomea.

Kutumia neno "angelitaka " ni hoja ambayo inatufikirisha kuwa je kweli angelitaka ingekuwa hivyo.

Sasa kutumika kwa neno angeli au ingeli hakufanyi kitu kisiwe hoja bali kinafanya hoja hiyo lau ingekuwa kinyume chake.

Sasa kwa mtazamo wako unaweza kusema hata hiyo aya msemaji hakupaswa kutumia neno "engeli" kwa kuwa tu haijatokea hivyo ambavyo amesema.

Sasa unatakiwa ujibu hoja,na sio kukimbia hoja kwa sababu imetumika neno ingeli au angeli..

Pia angalia aya nyingine..

لو أراد الله أن يتخذ ولدا لاصطفى مما يخلق ما يشاء سبحانه هو الله الواحد القهار

[ AZZUMAR - 4 ]
Lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka kuwa na mwana, basi bila ya shaka angeli teua amtakaye katika alio waumba. Subhanahu, Ametakasika na hayo! Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda atakalo.

Qurani imetumia neno "ANGELI.."

kwa maana ya kuwa laiti ingekuwa hivyo.

Na kutumia neno angelitaka katika aya hiyo hakujafanya hoja isiwe hoja,bali ni hoja hasa,ila wewe ungeliikataa kwa sababu ya neno angeli ambalo humaanisha lau ingekuwa hivyo.

Sasa hao wanachuoni unaowadai ikiwa kama hawataki neno "ingeli au angeli" basi wagahamishe kuwa Qurani imetumia mara nyingi sana maneno hayo.

Katika hili sidhani kama una hoja madhubuti ya kukamatia...
 
Itikadi ni kusadikishwa kimoyo, kifikra na kiakili. Muafaka huu hutegemea ni nani anayekunyweshwa jambo katika fikra mpaka kufikia hatua ya kuwa na uyakini usiyofikiwa na wasi wasi unafikia hatua ya kuuenzi na kuufanyia kazi.

Huu urithi ili ufanyie kazi sawa sawa unabidi upikwe na elimu ilyokuwa sawa sawa. Ukipikwa kinyume chake matokeo yake ni ghasia! Utakuwa na itikadi isiyotanguliwa na elimu yenye ufahamu.

Hii hali ndiyo anayo mkuu Zurri, yeye ameshapikwa hivyo na itikadi yake ndiyo ipo hivyo! Kikimjia chakula kingine itikadi aliyopikwa nayo inamwambia anatoka katika misingi hali ya kuwa si kweli. Laiti angelipikwa kwenye misingi elimu kama ilivyo maana na tafsiri ya elimu asingelikuwa kama alivyo.

Itikadi aliyopikwa nayo ndugu Zurri elimu aliyonayo yeye ndiyo sahihi na mafuhumu yake ndiyo yapo hivi nje ya mafuhumu hayo hakuna usahihi. Aliye hivi likiwekwa suala la elimu mezani mtajadiliana nini tena? Uyakinifu wake haukujengwa kielimu bali kuitikadishwa. Hili lipo hivi lipo hivi, basi hakuna jengine.

Mtu wa namna hii mizani yake ya kuyaendea kuyafikira masuala hayapo kieleimu bali yapo alivyoitikadishwa. Ndiyo maana hayupo kwa kuelewa bali yupo kukitetea kile alichopikwa nacho. Hafungui milango ya kuelewa bali anafungua milango ya kile alichoamnishwa! Kwa maana nyengine ufahamu wake umekatishwa tamaa ya kuwa nje ya hiki hakuna nje ya hiki.

Aliyepikwa hivi ukijadili naye kieleimu yeye haiangalii elimu. Yeye ataangalia itikadi yake. Ameaminishwa alichokuwa nacho ndicho aula! Kwa alichokielewa ndiyo sahihi zaidi mwengine anapwaya! Ndiyo maana ukijadili naye haleti ufahamu bali analeta nukuu ya kile alichoitikadishwa nacho chenye msimamo wa kwake.

Bila shaka ameaminishwa mafunzo ya Uislam marefu na mapana ni hayo aliyopewa. Ndiyo maana majibu yake ukiyaangalia yeye ni Akbar! Kwa maana usahihi ninao mimi. Lakini wewe ndugu Safuher upo kimsingi wa kielimu, kuwa huu ufahamu sawa umeuitakidi upo hivi kwa kuwa hiyo itikadi uliyoiweka hivyo ina misingi yake ya kielimu basi tuufikie kwa misingi yake ya kielimu.

Kwenye hili ambalo unajadiliana na ndugu Zurri njia ulizopita ndizo njia ninazopita mimi na umenipa faida nimejifunza mambo kutoka kwako! nimefaidika pakubwa sana kwa elimu uliyoitoa. Shukrani na Mungu akulipe kheri zaidi.

Zurri na Kiranga wametofautiana sehemu moja tu.
Lau zurri angezisoma nasaha zako hizi basi angepata faida kama ambavyo mimi nimezipata faida hizo katika maneno yako haya.

Bwana zurri umemchambua vyema na hata mimi nakiri ndivyo alivyo na wadau wengi watakubali hilo.

Ni mtu ambae anadhani kuhoji kunaishia katika elimu,kumbe hata elimu inapaswa kuhojiwa na kufahamika.

Kimsingi nimekuelewa kaka,na mimi nasaha ulizompa zurrri nitazichukua kama za kwangu na kuzidi kuzifanyia kazi.

Tokea nianze kuyajadili mambo ya elimu peke yangu nimegundua mambo mengi sana ambayo bwana zurri kama hatobadilika hawezi kuyagundua.

Masiku machache nilimuambia kuwa sheikh muqbili amesema kuwa hakatazi watu kufunga masiku yote kumi ya dhul hijja na wala hawezi kuwatia katika kundi la kuwa wanafanya bidaa kwa sababu hadithi imeenea.

Bwana zurri kwa kukosa subira ya kielimu akadai kuwa bwana muqbili anayemjua yeye hawezi kusema maneno hayo,yaani kabla sijampa nukuu anatia comment wakati ambao alitakiwa afanye subra.

Nikampa nukuu ya sheikh na pahala ilipo akatulia.

Kimsingi zurri ana mambo mengi ya kujifunza yeye pamoja na sisi pia.

Mfumo anaokwenda nao zurii andio mfumo wanaokwenda nao masalafi wengi sana na ndio maana mengi katika mambo wanaharibu bali hata wao kwa wao wanakatana mapande kutokana na kushiba elimu huku wakiwa na njaa ya ufahamu katika fikra zao.

Jambo hili linafanya safu za masalafi mfano wa kina zurri kupasuka vipande kila siku ya Mungu kwa sababu ya tatizo alilonalo zurri la kuwa MIMI NDO NIKO SAHIHI,WEWE UKO WRONG.

Kimsingi zurri yuko hivyo kwa sababu ya huko anakopikwa kielimu.

Allah akubariki na wewe mkuu
 
Kama ni hivyo kwa nini wazazi wa mtume wako motoni,wao walifikiwa na ujumbe wa mtume gani mpaka iwe wako motoni ?

Kwa sababu wazazi wa Mtume ni katika watu wa zama za baada ya nabii issa na kabla ya mtume muhammad.

Sasa tuambie wewe kuwa hawa wazazi wa Mtume wako motoni kwa kosa gani wakati hawakuwa na mtume katika wakati wao ?
Hilo nimelieleza katika ule mgawanyo wa wanazuoni. Ambao makundi mawili ni ya motoni.
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom