johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,796
- 141,695
- Thread starter
- #41
Unapoona hadi mwislamu anakiri hadharani kuwa yeye ni mwenye dhambi basi ujue leo Neno lilipata Mnenaji na Injili imefika mahali pake!Ile teolojia aliyoshusha askofu mkuu Ruwaich pale naamin wengi wameambulia patupu hata baadhi ya wakatoliki, ni shule yenye kiwango cha juu mno, sio rahisi kupata nje ya kanisa katoliki, ndo maana hadi viongozi wa serikali waliogopa wakabaki "kutubu" tu kwamba ni "wadhambi".... Ninavyojua Mimi na uelewa wangu huu mdogo, "Mahubiri" yana namna yake ya kuyaandaa, inaitwa "Homilia Takatifu", ni tofauti na risala, hotuba au maoni binafsi ya kasisi, hii ni shule muhimu sana kwa wahubiri wetu wote na wakitaka wanaweza kuisoma, bahati mbaya sana wengi wao hawaonekani kujali hili, wanayo mambo yao mengi mengine.