johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,840
- 141,763
Leo nimejifunza kitu kikubwa katika kuhusanisha dini na siasa kupitia maaskofu wa Kanisa Katoliki. Askofu Ruwaichi katika mahubiri yake kuanzia mwanzo hadi mwisho hakuzungumza hata sentensi moja iliyohusu siasa bali alijikita kwenye Injili.
Baada ya misa takatifu kukamilika wakati wa kusoma risala kwa mgeni wa heshima ndipo walau siasa kidogo ilionekana. Ninakumbuka wakati wa ule mgongano wa Kakobe na TRA siku ya ibada katikati ya mahubiri askofu Kakobe akaanza kuwashambulia maofisa wa TRA. Kadhalika wakati wa mgogoro wa Gwajima na Makonda ilikuwa ni katikati ya mahubiri askofu Gwajima alipoanza kumshambulia Makonda na karatasi aliyoiita ni cheti na kuanza kukisoma. Nawashauri hawa maaskofu wa Huduma za kiroho wajifunze kutoka Katoliki ibada ni lazima iheshimiwe na mambo ya siasa wayafanye baada ya ibada.
Kwa namna mahubiri ya Askofu Ruwaichi yalivyojaa hekima ya Mungu yalipelekea hata mgeni rasmi ambaye ni mwanasiasa kutumia zaidi maandiko ya Biblia katika salamu zake. Ahsante!