Dini na Imani za watu

0743919950

Member
Sep 20, 2021
7
0
Imani kwa tafsiri ijulikanyo na wengi nikuwa na matumaini na mambo yatarajiwayo.Unapokua na tumaini na jambo ambalo hulijui kwamba jambo hilo lipo na linawezaje kubadii maisha yako tunasema wewe una imani.Watu wengi huzani imani ipo kwenye dini tu, lakini la hashz imani ipo katika nyanja mbalimbali za maisha ikiwemo uchumi, elimu, safari, kilimo na hata afya.

Mgonjwa ana imani atapona, wanandoa wana imani ya kuishi pamoja mpaka kufa, mwanafunzi ana imani ya kufaulu vizuri masomo yake,mgonjwa ana imani ya kupona nakadharika.Katika maisha ya sasa imani imekuwa sio matumaini tena kwa watu waaminio bali ni mabishano, malumbano, na kuvunjana mioyo miongoni mwa watu.Na matatizo yote haya ni kutokana na dini kuingilia maisha ya watu.

Dini zetu zimetutenga na ndugu jamaa na marafiki,lakini pia zimetengeneza tabaka kubwa kati ya makundi mbalimbali katika jamii yetu.Mfano leo hii katika makanisa matajiri wanajulikana na wanapewa nafasi kubwa kuliko maskini, lakini pia baadhi ya dini zinaonekana zina maslahi makubwa kuliko nyingine.Dhamna hii imesababisha mpaka sasa baadhi ya maeneo kuna vita kati ya watu wa dini moja na dini nyingine , lakini pia kutokuwepo na melewano baina yao.

Hivyo basi, dini kama kitovu kikuu cha imani zimegeuka na kuwa vivuli vya kuficha wahalifu, wanyang'anyi pamoja na watu wasio na lengo jema.Na ile dhana ya kwamba dini ni kusanyiko la watu wenye matumaini na Mungu wao linatoweka kwasababu imani hizo zimegeuka na kuwa sio tena matumaini bali lungu la kuwanyanyasa waumini na wanajamii kiujumla.Mfano; kupitia dini baadhi ya watu wanawadanganyawatu wao kwa maslahi yao binafsi ikiwemo kujiongezea kipato, kupata madaraka na pia kujisafisha maovu yao.

Ushauri wangu ni kwamba dini zetu sio kitu kibaya bali sisi watumiaji wake tunaharibu uhalisia wake, hivyo basi sisi kama watu wenye imani tofauti tofauti tujaribu kutumia dini zetu kwa imani za kweli pasipo kuharibu amani wala maisha ya wenzetu.Tukusanyike pamoja kwa imani zetu na matumaini yetu pasipo kudharau watu wa imani nyingine.
 
Back
Top Bottom