Kutoka FB
Sio kwa ubaya, lakini hii "Kitchen Party Gala" naiona zaidi kama jambo linalowafaa single mothers. Wenye ndoa achaneni nayo kama inakwenda kinyume na misingi ya familia zenu.
Najua wanawake wengi watanipinga hapa, lakini mara nyingi kwenye mijadala kama hii wanaume huonekana wabaya pekee. Je, hakuna mema yoyote wanayofanya? Kwa nini kila siku tuzungumzie mabaya yao bila kutambua mazuri yaliyopo?
Dina Marios nafikiri ingefika mahali ukaelekeza nguvu zako kusaka mume na kujenga familia na ndoa badala ya kutumia gharama kubwa kuhalalisha mtazamo unaoweza kuwafanya baadhi ya wanawake waone wanaume hawana thamani kwenye maisha yao. Sisemi kwamba mwanamke asijitegemee au asitafute mafanikio, lakini mafanikio ya kifedha hayafuti umuhimu na thamani ya mwanaume
Mimi ni single mother, lakini sijawahi kuyaona maisha haya kama jambo la kujivunia au la kutamaniwa. Badala yake, nimekuwa nikihamasisha wanawake waliojaliwa ndoa kuzithamini na kuzilinda.
Kwangu mimi, pesa na mali ndani ya ndoa ni mali ya familia. Huo ndio msingi wa ushirikiano wa kweli. Kama tunataka kuzungumzia uhuru wa kifedha, basi tuweke wazi kwamba tunazungumzia watu wasio kwenye ndoa au mahusiano ya kifamilia yenye wajibu wa pamoja.
Pesa na mali haviwezi kuondoa thamani ya mwanaume katika maisha ya mwanamke, kama ambavyo haviwezi kuondoa thamani ya mwanamke katika maisha ya mwanaume. Familia hujengwa kwa ushirikiano, heshima na upendo, si kwa fedha na mali pekee.
Tusiwafundishe watoto wetu kwamba kuwa single mother ndio hatua ya juu ya mafanikio au kwamba wanaume ndio chanzo cha kila tatizo. Tuwaonyeshe umuhimu wa familia, uwajibikaji na kuheshimiana.
Huyu mama mtoa mada nina uhakika ni single mama kwake ni fahari mtoto wake wa kike afate njia zake, Mtanichukia au kunipinga, lakini ujumbe wangu ni huu: mali na pesa si kila kitu katika maisha ya mwanamke. Na ndani ya ndoa, mali na pesa ni za familia. Hutaki mfumo huo, basi usiolewe wala usioe.
Kama kuna jambo sijawahi kujivunia kwenye maishayangu ni kuwa single mother aisee kwangu naona kama ni doa kubwa sana na sitamani nijapokua na mtoto wa kike aje kupita nilipopita ni mtihani tuu wa dunia but am not proud to be single mother in this world but ninajivunia kuwa mama bora kwa mwanangu that's all.
#sesiliasalleko