Dikteta uchwara (Protofascism) ni dhana ya kisiasa

Stabilaiza

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
1,843
1,143
Dhana ya dikteta uchwara (proto-fascism) inaongelewa kwa sasa nchini kwetu lakini haieleweki vema miongoni mwa wanasiasa. Nimejitahidi kuchungulia maandishi kwenye dunia hii ya utandawazi na kugundua kuwa Dikteta uchwara siyo mnyama, bali ni dhana katika ulingo wa siasa.

Kwa ufupi inamaanisha kuwa ni utawala unaoelekea kuwa wa kidkiteta. Watawala wanaoitwa ma-Fascist ni wale ambao hupenda kutoa miongozo kandamizi na ya kikatili kwa wananchi wake. Maandashi yanaonyesha kuwa watu ambao hawako upande wa fascist hupotezewa uhalali wao ikiwemo kupotezwa kwa maisha yao.

Hapa chini ninaweka maelezo mafupi na sehemu yanakopatikana yakielezea dhana ya Proto-fascism na fascism.

protofascist ‎(plural protofascists)
1. An individual whose opinions or policies show the beginnings of fascism (angalia Wiktionary)
2. A political movement or program tending toward or imitating fascism ( angalia merriam-webster.com)

Kutoka washingtonpost.com/news

3. Fascist leaders impose a brutal uniformity on the lives of their citizens.

Kwa mfano: "The Italian nation is an organism, having aims, life and means of action superior to those of the single or grouped individuals who compose it," stated Mussolini's Labor Charter in 1927.

4. Fascist leaders tried to eliminate differences. Members of disfavored groups lost their legal identities, rights and citizenship — if not their lives. Even favored groups were subjected to oppressive discipline.
 
mengi tunaendelea kusikia kama tulivyosema sisi kina gogo la shamba kwamba,miaka hii mitano tutasikia mengi ya ajabu
 
Semeni sera zenu za kurudisha nidhamu na uw
..Mzee Makamba alidai wapinzani watabatizwa kwa MOTO.

..wana ccm walilipuka kumshangilia.

..sasa ina maana hawakujua kwamba wanashangilia udikteta? Kubatiza kwa MOTO.

Semeni sera zenu za kurudisha nidhamu na uwajibikaji serikalini zimepata wakuzitendea haki mapema zaidi tofauti na mlivyodhani. Wakati wa mkwere Kila mtu humu alikuwa Anataka hii nchi itawaliwe ki DIKTETA ili watanzania tuweze ku practice accountability regardless watumishi wa umma au sekta binafsi. Ninachokiona hapa ni wapinzani kuanza kuishiwa hoja zenye mashiko hasa zenye kugusa maisha ya wanyonge tofauti na kipindi cha mzee wa trip. Sijui bwana labda mitaa hii tu ninayoishi ndio imepoooa Sana kwani wafuasi wa chadema na wananchi kwa ujumla hawana hata muda tena wa kujadili matamko ya chadema zaidi wanavutiwa tu na kubishana ukongwe na umahiri wa tundu lisu mahakamani. Kiukweli Hakuna mtu anautayari wa kuandamana wala ku support movements zisizo na mbele wala nyuma. Ushauri wangu kwenu wenye kuaminishwa bila kuchanganya na za kwenu siku hiyo mkae mkao wa kula tayari kwa kupokea kichapo. Huu muda ni wakufanya kazi mkisaidiana na wawakilishi wenu
 
We see it in Moral Philosophy and Political Philosophy!!
But well absorbed in moral Theology!!Huu ndio wakati wa Wabobezi wa Moral Theology na Moral Philosophy kama kina Pengo and his Co. To come out and air their opinions...I miss the TEC of Mwoleka,Mgulunde,Justine Samba,Mihayo,Castor Sekwa,Lebulu and other departed souls of their kind!Lazima wangesema neno
 
1968.jpg


Mbuyu huanza hivi hivi...!
Dikteta uchwara hafanikiwi kama hawapo wanaomshangilia na kumsifia.
Ole wao siku udikteta kamili unaiva, washangiliaji ni wa kwanza kuumia.
 
Hii ni propaganda ya kihuni inayotumika Kupima upepo wa Amiri Jeshi Mkuu.
Umemfikiria Amiri Jeshi Mkuu jwani tunaongekea vita hapa?

Hilo tu kinaonesha dhanabya udikteta ilivyoshika akili za watu.

Badalabya kumfikiria rais, kiongozi wa nchi, umemfikiria Amiri Jeshi Mkuu, kiongozi wa jeshi.

Akiki yako imekaa kuoewa amri kijeshi jeshi.

Udikteta uchwara ushakuchota.
 
Amejichanganya mwenyewe.

Hapo ndipo upumbavu wa binadamu ulipo. Mtu anaabudu shetani, anajaua kabisa anachokiabudu yeye ni shetani na anajua wenzake wanaabudu Mungu. Lakini bado analazimisha huyo shetnai wake atambulike Mungu wakati anajuilkana shetani.
Ukweli ni mwanzo mzuri wa uhuru.

Mtu kama ni dikteta ni dikteta tu hata apakwe rangi ipi. Ni vizuri akakubali ukweli kwamba yeye ni dikteta kwa sababu ndivyo alivyo.

Wewe mtu unatawala kwa misingi na rangi zote za udiktata uchwara. Umekwisha tamka hadharani kwamba watakaokupinga utawapoteza na wakipata nafasi ya kuishi basi utawashughulikia kikatili. Kwanza hapa ukiitwa dikteta uchwara inaonekana bado kwa mbali unasomeka kwa sababu hakuna tabia zinazozidi hapa zinazotambulisha utawala wa ki fascist.

Tutembee na TL hadi hapo tutakopoona mabadiliko ya tabiza a uongozi, kama tutakuwa tunaishi (kwa maana wale watakuwa bado hawajapotezwa).
 
1968.jpg


Mbuyu huanza hivi hivi...!
Dikteta uchwara hafanikiwi kama hawapo wanaomshangilia na kumsifia.
Ole wao siku udikteta kamili unaiva, washangiliaji ni wa kwanza kuumia.
Hii imetoka wapi mkuu?
 
Umemfikiria Amiri Jeshi Mkuu jwani tunaongekea vita hapa?

Hilo tu kinaonesha dhanabya udikteta ilivyoshika akili za watu.

Badalabya kumfikiria rais, kiongozi wa nchi, umemfikiria Amiri Jeshi Mkuu, kiongozi wa jeshi.

Akiki yako imekaa kuoewa amri kijeshi jeshi.

Udikteta uchwara ushakuchota.
Mkuu nakuaminia hebu ongeza notisi ili hii dhana ifahamike vizuri zaidi.
 
Back
Top Bottom