Dikteta ni nani? Na kwanini tunamhitaji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dikteta ni nani? Na kwanini tunamhitaji?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee wa Changamoto, Jun 14, 2009.

 1. M

  Mzee wa Changamoto New Member

  #1
  Jun 14, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninapoangalia namna "tunavyokaririshwa" maana za nani ni nani, na kwanini ni yeye na kwa manufaa ya nani na nani awe rafiki na nani awe adui yake nasikitika sana. Tumepangiwa kila kitu kwa tafsiri ya wenzetu ambayo kwa hakika ni kwa manufaa yao.

  Mandela alikuwa "mkorofi" ( na dikteta fulani hivi) kwa kudai uhuru ambao baada ya kutambulika sasa anaonekana ni shujaa japo hajabadili alichofanya, Saddam alikuwa shujaa aliposhirikiana na wao kisha akawa dikteta alipopingana nao. Gadafi aliyekuwa dikteta na kuonekana kama asiyewajali wananchi wake sasa kawa shujaa na "kiongozi safi" kwa kuwaruhusu "wakuu" kuingia na kukagua silaha zake japo hakuna alichobadili kwa wananchi.
  Luciano aliwahi kuimba kuwa "they're trying to control our minds, and treating us like swine. They telling us who to love or hate as if they're great"

  Najua akitokea mtu akalazimisha baadhi ya mambo ya maana kutendeka nyumbani basi ataitwa dikteta (na kwa bahati mbaya nasi tutashabikia hata kama si tafsiri yetu).

  Najiuliza akitokea "kiongozi" akalazimisha kusimamishwa kwa mikataba yote ya madini ili ipitiwe upya hataonekana dikteta?

  Je atakayelazimisha viongozi wakuu waliosababisha mabilioni ya hasara serikalini wachunguzwe licha ya katiba waliyoshindwa kuitii kutosema hivyo hataonekana dikteta?

  Je atakayelazimisha wabunge kujenga ofisi na kutumia muda mwingi majimboni mwao kama walivyoahidi wakati wa kampeni hataonekana dikteta?

  Atakayelazimisha utendaji wa mikoa kulingana na rasilimali zake kuwanufaisha wananchi wake na kisha nchi nzima huyo hataonekana dikteta?
  Najua kuwa atakayewafikisha viongozi wakuu mahabusu ataitwa dikteta kwa kuwa amekwenda kinyume cha katiba, lakini sijui kwa nini katiba imlinde yule ambaye ameivunja kujilimbikizia mali na kuitia serikali hasara kubwa?

  Kama huyu atakayetenda haya niliyosema hapo juu, atakayevunja mikataba ya ujenzi wa miundombinu yenye utata, atakayehakikisha ahadi za wananchi zinatekelezwa na waahidi hasa wabunge, atakayeshurutisha matumizi mazuri ya rasilimali za wananchi kwa manufaa ya sehemu husika, atakayeshinikiza malipo kwa wafanyakazi ambayo mpaka sasa haijajulikana kwanini hawajalipwa ilhali waheshimiwa wanapata pesa zao bila malimbikizo, atakayehakikisha kuwa mkulima wa anapata senti zake zote alizoikopesha serikali na ambazo anatumia pesa nyingi kufuatilia kuliko atakazolipwa, atakayesimamisha ziara za nje na ndani za viongozi (zisizo za lazima) na atakayeamua Tanzania iwe ya manufaa kwa wa Tanzania kwa kutumia kila kilichopo Tanzania ataitwa DIKTETA, basi namuombea awepo. Aje atufanyie hayo na nadhani tunamhitaji na anaweza kuwa suluhisho la awali kwa yaliyopo.

  Maana sasa imekuwa kama alivyosema Kaka Evarist Chahali (wa www.http://chahali.blogspot.com/) kuwa HAKI IMEKUWA FADHILA na twahitaji atakayeangalia haki na kama haki.

  Nionavyo ni kwamba mfumo unaotumika kumpata mtu atayewania uongozi unapita katika ngazi na misaada ambayo mpaka aje kupatikana mgombea anakuwa kashirikisha "wataalamu" wa ufujaji ambao akichukua madaraka hataweza kusema lolote juu yao.

  Pengine nionavyo mimi ndilo tatizo, lakini kuna ukweli kuwa tafsiri nyingine zinatufanya tuwachukie wale ambao wanaweza kutuletea mabadiliko ya kweli na badala yake tunaendeleza "kubebana na kufichana" ambako kunaendelea kutuweka tulipo.

  Ni Mtazamo wangu tu na naendelea kutunza haki ya kukosea na kukosolewa.
   
 2. dexterous

  dexterous JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2017
  Joined: Feb 26, 2014
  Messages: 1,002
  Likes Received: 794
  Trophy Points: 280
  2009-2015
   
 3. MLAU

  MLAU JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2017
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 4,498
  Likes Received: 3,068
  Trophy Points: 280
  Na maji tutaita.......mmaa
   
 4. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2017
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Daaaah, mpaka nimesisimka mwili. Wewe jamaa ni hatari sana, kuna kitu Mungu alikuonesha ndo maana ukaandika haya na miaka 7 baadae yanatokea copy and paste.

  Asante sana
   
 5. Copenhagen DN

  Copenhagen DN JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2017
  Joined: Oct 5, 2014
  Messages: 5,090
  Likes Received: 6,292
  Trophy Points: 280
  He who wishes to be obeyed must know how to command-

  The Prince

  Niccolo Machiaveli
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2017
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Dikteta, huyu
   

  Attached Files:

 7. s

  stemcell JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2017
  Joined: Apr 19, 2015
  Messages: 621
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 80
  Kuna mengi mazuri ila machache ya hatari,kama kutofuata taratibu za badget,kuona upinzani au mpiga kura asiyo kuchagua adui,uhuru wa kumkosoa,kutokuwa na waushauri,kuingilia uhuru wa mahakama na kuwaambiya wapindishe kesi Tra walipwe hela kisha na wenyewe mahakama walipwe,kutokujali wananchi wengi kwenye budget (wakulima) na kukimbizana na machache yanayoonekana mjini( ndege,flyover n.k) na kusahau yanayo hitajika vijijini kwenye watu wengi mfano chanjo vijijini, madawati bila darasa, kuwacha kudhibiti uuzaji wa chakula nje ya nchi kama alivyo ahidi mwanzo,kutosaidia wakulima kwenye maendeleo (mfano budget ya maendeleo kilimo 10% ndiyo iliyopelekwa)la hatari zaidi ni kurudisha sera ya kutaifisha mali ya watu na huku tunataka wawekezaji wajenge viwanda( mashamba ya watu,viwanja n.k).kama kweli unataka kusaidia angewacha ndege kisha alipe deni ya tanesco kisha umeme uwe rahisi kuliko kenya, lakini usahau wakulima na umeme ghali tutaota uchumi bora.ni mawazo yangu tu.
   
Loading...