Digital Marketing:Mfumo wa marketing usiofahamika kwa wengi unaoenda kuua matangazo ya redio na tv

Mtoa mada ka-copy gazeti toka Marekani akaona kayapatia!
Nikweli mkuu sema kashindwa kutoa nfano vizuri wakueleweka viru, kwenye tembeatembea yangu nimengundua wabongo wako mbali sana.

kuna Kampiny moja ya kibongo wanafanya biashara online inaitwa www.digxam.co jamaa wako mbali sana,digital marketing iko mbali sana mkuu hawa jamaa wako kwenye list ya google kati ya makampuni yanayokua kwa kasi sana

tujifunze mambo mapya tuache kubeza kilajambo tuache tusikariri tekinoloji mambo yanabadilika kwa kasi sana
 
Nikweli mkuu sema kashindwa kutoa nfano vizuri wakueleweka viru, kwenye tembeatembea yangu nimengundua wabongo wako mbali sana.

kuna Kampiny moja ya kibongo wanafanya biashara online inaitwa www.digxam.co jamaa wako mbali sana,digital marketing iko mbali sana mkuu hawa jamaa wako kwenye list ya google kati ya makampuni yanayokua kwa kasi sana

tujifunze mambo mapya tuache kubeza kilajambo tuache tusikariri tekinoloji mambo yanabadilika kwa kasi sana
Tuache kubagazana
 
Nikweli mkuu sema kashindwa kutoa nfano vizuri wakueleweka viru, kwenye tembeatembea yangu nimengundua wabongo wako mbali sana.

kuna Kampiny moja ya kibongo wanafanya biashara online inaitwa www.digxam.co jamaa wako mbali sana,digital marketing iko mbali sana mkuu hawa jamaa wako kwenye list ya google kati ya makampuni yanayokua kwa kasi sana

tujifunze mambo mapya tuache kubeza kilajambo tuache tusikariri tekinoloji mambo yanabadilika kwa kasi sana
Wako vizuri sana.
 
Dah HAMKOSAGI KUKANDIA HATAKAMA JAMBO NI ZURI.
Hapa ni kwetu inabidi tupapende kama palivyo wabongo tunashindwa nini ?

Bongo siwezikushangaa kuajiriwa mtu mwenye elimu ya std 7 anaachwa mwenye PHD ni kawaida bongo.

Mleta mada kaongea kwa ufupi sana hii digital marketing inau biashara nyingi zaidi ya loitaja ndio maana baadhi ya watu hapa awataki kabisa kusikia .

Nani anakumbuka kabla ya smart phone hawa watu walipiga pesa sana leo wako wapi wauza:
  1. Saa
  2. Touch
  3. Studio za picha
  4. Wapiga picha
  5. Redio
  6. Calendar
  7. Betry za Tiger
  8. Calculator
  9. ..........
Watu ni waoga sana wa tekinolojia kwasabu baadhi wanafaidika na mifumo ya kianalogia baadhi ni mazoe watu waishazoe biashara ni kuamka asubuhi kupanda gari au kuchapa nguu kwenda dukani, watu waisha zoea kufanya kazi ni kuamka asubuhi kugombania daladala ndio kufanya kazi.

Kundi la kwanza wanufaika wa mifumo ya kianalogia hili kundi wajiandae watakwenda na maji kama wauza saa touch na betry za tiger kwasabu watu tangu Covid wanafanya online business kufanya kazi zao za makazini makwao kwa njia za online itakuwa ngumu tena kumuibia mtu
  1. Simu
  2. Pochi
  3. Pesa
  4. Dunga dunga kwenye daladala itabaki historia
  5. rushwa makazini
  6. Wachawi
  7. naujinga kibao utakoma
Kundi la pili la watu waoga wa kidigital hawa watabadilishwa na mazingira watadilishwa na wakati wasitumize kichwa.
 
Hapa ni kwetu inabidi tupapende kama palivyo wabongo tunashindwa nini ?

Bongo siwezikushangaa kuajiriwa mtu mwenye elimu ya std 7 anaachwa mwenye PHD ni kawaida bongo.

Mleta mada kaongea kwa ufupi sana hii digital marketing inau biashara nyingi zaidi ya loitaja ndio maana baadhi ya watu hapa awataki kabisa kusikia .

Nani anakumbuka kabla ya smart phone hawa watu walipiga pesa sana leo wako wapi wauza:
  1. Saa
  2. Touch
  3. Studio za picha
  4. Wapiga picha
  5. Redio
  6. Calendar
  7. Betry za Tiger
  8. Calculator
  9. ..........
Watu ni waoga sana wa tekinolojia kwasabu baadhi wanafaidika na mifumo ya kianalogia baadhi ni mazoe watu waishazoe biashara ni kuamka asubuhi kupanda gari au kuchapa nguu kwenda dukani, watu waisha zoea kufanya kazi ni kuamka asubuhi kugombania daladala ndio kufanya kazi.

Kundi la kwanza wanufaika wa mifumo ya kianalogia hili kundi wajiandae watakwenda na maji kama wauza saa touch na betry za tiger kwasabu watu tangu Covid wanafanya online business kufanya kazi zao za makazini makwao kwa njia za online itakuwa ngumu tena kumuibia mtu
  1. Simu
  2. Pochi
  3. Pesa
  4. Dunga dunga kwenye daladala itabaki historia
  5. rushwa makazini
  6. Wachawi
  7. naujinga kibao utakoma
Kundi la pili la watu waoga wa kidigital hawa watabadilishwa na mazingira watadilishwa na wakati wasitumize kichwa.
I see
 
Nauliza unawezaje pata target ya age gruop au gender?
mfano nna brand mpya ya condoms ya kiume
tangazo liwa target watu wa umri wa miaka 15-40 wanaume na nataka watu laki mbili liwafikie
Onawezeka kabisa ndio maana inaitwa digital utaweza kutangaza kwa kundi la watu walengwa tu unachagua na location
 
Habari wakuu..

Ninaimani mpo njema mkiimalizia weekend.Ningependa kuchukua muda huu kushare a.b.c juu ya mfumo wa kisasa wa masoko wa digital marketing.Mfumo ambao unaaminika kila mfanyabiashara anahitaji kuufahamu katika karne hii ya teknolojia.Haijalishi unauza bidhaa au unatoa huduma hizi zote zinahitaji kufanyiwa masoko ili ziweze kuwafikia wateja.

Kutokana na mabadiliko makubwa ya kiteknolojia na mifumo mingi kuhitaji kuendana na mabadiliko haya ya kiteknolojia nataka tuangalie na namna gani mfumo wa biashara na masoko nao unahitaji kutoka katika mfumo uliozoeleka wa masoko na kuingia katika mfumo wa digital marketing.

Kabla ya yote ningeomba niweke angalizo kidogo watu wengi wamekuwa wakitafsiri vibaya digital marketing kama ni kutumia account zetu za mitandao ya kijamii na kupost biashara zetu.Nikiongelea digital marketing sizungumzii kupost biashara kwenye kurasa zetu binafsi za mitandao ya kijamii au status za whatsapp maana hiyo itabaki kuwa ni kushare tu kwa watu wako wa karibu na kupata tu pongezi kutoka kwa ndugu na jamaa zako ambao mara nyingi huwa sio wateja wa mara kwa mara.

Ninachotaka kuzungumzia hapa ni namna utakayoweza kuwafikia wahitaji wa bidhaa au huduma zako popote walipo hata kama hufahamiani nao (Si tafsiri rasmi ila ninajaribu kuweka maneno marahisi kwa kadiri itakavyoweza kueleweka) ningependa hii ndio iwe point kuu ya uzi huu wa leo.

Inawezekana kabisa uzi huu ukabadilisha mtazamo wako juu ya namna ya kutumia digital marketing katika biashara yako aidha uwe mfanyabishara mdogo,au wa kati au hata mjasiriamali.

Tuje kwenye reality ya maisha ya kuanzisha biashara.Watu wengi wamekuwa wakiuliza na kuhitaji maeneo yenye mzunguko mkubwa wa watu(mfano ni mijini au eneo ambalo lipo barabarani) wakiamini watu wengi watakatiza maeneo hayo na wataona biashara zao.

Ni strategy nzuri kwa kuwa unakuwa na uhakika wa kupata wateja kwakuwa maeneo ya mijini au barabarani wanakatiza watu wenye uhitaji wa bidhaa au huduma mbalimbali au saa zingine linaweza kuwa eneo maarufu na linalofahamika kwa aina fulani ya biashara.

Tunajua ugumu wa upatikanaji au gharama kubwa itakayokuingia kuweza kupata nafasi katika maeneo hayo.Mbali na hivyo maeneo kama hayo huwa yanaushindani mkubwa sana kwakuwa na watu wengi wanaofanya biashara ya aina moja.

Huwezi kupata ofisi yenye ukubwa wa kutosha ya kuweka biashra yako maeneo yenye mzunguko mkubwa kwa gharama ya chini ya milioni moja (1,000,000) kwa mwezi.Hapo itakubidi uandae si chini ya milioni 6,000,000 kwa malipo ya miezi 6 tu.Daaahhh its pain kwa kweli.

Achana tu na kupata eneo la kufungulia biashara yako kutangaza biashara ni moja ya muhimili mkubwa wa maendeleo ya biashara.Na kutokutangaza biashara limekuwa ni kosa kubwa sana la wafanyabiashara wengi.Wengi wao wamekuwa wakidharau suala la advertising (matangazo) na kuridhika na wateja wachache wanaowafahamu.

“The Business That Can Spend The Most To Acquire A CustomerWins” Dan Kennedy huyu ni mshauri maarufu wa masuala ya biashara

Hapo anamaanisha biashara yoyote itakayojidhatiti kugharamia suala la kumnasa mteja basi itafanikiwa.

Haijalishi una bidhaa au huduma bora kiasi gani bila matangazo biashara yako itakuwa ni yenye kusua sua tu katika ukuaji na kuendelea.
Suala la matangazo limekuwa likiwatia hofu wafanyabiashara wengi kutokana na gharama za matangazo kuwa kubwa na wengi wa wafanyabiashara wakihofia kutoweza kurudisha gharama hizo walizotumia katika matangazo.

Hapa chini ni gharama za matangazo kutoka katika kituo kimoja wapo cha redio

MATANGAZO YA REDIO KATIKA MUDA MAALUMU NI KIASI MAALUMU CHA SEKUNDE UNAZOPEWA

View attachment 1213411

GHARAMA YA MATANGAZO YA REDIO KWA MWEZI MZIMA

View attachment 1213412
Ukiangalia gharama za matangazo ya redio ambayo ndio nafuu zaidi utahitaji sio chini ya 2,000,000 kwa mwezi kama kweli unataka kufikia wateja wako.

Matatizo haya yote kwa sasa yanatatuliwa na mfumo mpya wa masoko ambao ndio digital marketing.Kama ambavyo tunataka biashara yetu iwe maeneo yenye mzunguko mkubwa wa watu na iweze kuonekana basi hakuna eneo lenye mzunguko mkubwa kama Mtandaoni (Internet).

Kutokana na hilo haijalishi biashara yako ipo mbagala kizuiani au tegeta mivumoni na hata mtaa wa aggrey kariakoo.Unapokuwa mtandaoni jua kabisa upo eneo leny mzunguko mkuwa wa watu wa aina zote ambao ungewahitaji.Hapo kinachobakia tu ni Targeting kwa maana ni namna ya kumpata mlengwa wa bidhaa au huduma yako.

Wafanyabiashara wengi wemekuwa wakitengeneza account zao katika mitandao ya kijamii na kutumia kama njia ya kunasa wateja.Ni njia nzuri sana ijapokuwa itakuhitaji utumie nguvu kubwa sana ya kushare content kwa wale wachache wanaokufahamu ili baadaye uweze kufanya nao biashara.

Njia hii sio matumizi effective ya digital marketing na teknolojia katika biashara.Kwa mtu aliye serious na biashara yake anahitaji kuwa na online presence.Hapa namaanisha kama ni bidhaa basi uwe na online store au website yenye kuonesha huduma unazotoa ambayo itaonesha bidhaa zote ulizonazo hapa huhitaji kuhofia ushindani kwani mamilioni ya watu wanaozunguka mitandaoni wanapofika kwenye online store au website yako ndio kafika dukani/ofisini kwako kazi yako ni kumhudumia.

Online store / website hizi gharama zake haziwezi kuzidi 1,000,000 kwa malipo ya mara moja tu ambapo huhitaji malipo ya kila mwezi bali ni gharama ndogo tu za kulipia kila mwaka zisizozidi 300,000 kwa mwaka.

Jaribu kufanya uchunguzi kwa kugoogle au kuingia katika mitandao ya kijamii na kuangalia ni wangapi kati ya wafanyabiashara ambao wanafanya biashara kama unayofanya wewe au unayonuia kuifanya kama wanamiliki online store au website ya kutangaza bidhaa au huduma zao. Utagundua ni fursa kwako kuliteka soko mapema iwezekanavyo kabla washindani wako hawajashtuka.

Hapo utaona kupitia teknolojia tumetatua gharama kubwa ya upangishaji wa maeneo ya biashara kutoka 12,000,000 kwa mwaka mpaka 1,000,000 na unaweza kupata chini ya gharama hii kulingana na mahitaji yako.

Jambo lingine baada ya kuwa na online store ni kutangaza biashara yako.
Ninaenda kukuonesha ni kwa kiasi gani gharama ya kufanya marketing mtandaoni ni nafuu sana na ili hali watu wengi hawafahamu au hawajui namna ya kuweka matangazo mitandaoni.

Fahamu ya kuwa watu wengi mamilioni wamehama kutoka kwenye matumizi ya redio,t.v na hata magazeti katika kupata habari,elimu pamoja na burudani.

TAKWIMU KUTOKA FACEBOOK JUU YA WATUMIAJI WA MTANDAO HUO KUTOKA TANZANIA

View attachment 1213507

KUNA WATUMIAJI MILIONI 3-3.5 WA FACEBOOK KUTOKA TANZANIA (HAWA NI WATEJA WAKO UKIJUA NAMNA YA KUWAPATA)


HII HAPA CHINI NI ACCOUNT YANGU YA KUFANYIA MARKETING KUPITIA FACEBOOK


View attachment 1213424

Hapo juu ni screeshot ya account yangu ya kufanyia marketing mtandaoni.Na mtandao ninatumia ni Facebook.Kuna mitandao mingi tu unayoweza kutumia kulingana na aina ya wateja unaohitaji kuna google,facebook & instagram,linkedin au twitter.

Jaribu kutazama idadi ya watu niliyowafikia 32,672 kwa gharama ya usd 21.22 ambayo ni sawa na 50,000 tu.

Katika hali ya kawaida tu huwezi kukosa wateja wa bidhaa au huduma yako kutoka kwa watu elfu 32. Naamini hii ni zaidi ya eneo la biashara lenye mzunguko mkubwa.Na kazi hii unaweza ukaifanya ukiwa na ka laptop chako kunasa wateja usiku na mchana bila kujali masaa ya kazi. Hii yote ni kwakuwa watu hawa wote utawapeleka katika online store yako. Ambayo haifunguliwi saa 2 na kufungwa saa 12 bali ipo open masaa 24.

Napia faida kubwa ya digital marketing inayoipiku njia tuliyozoea ya marketing ni ultra targeting.

Nini maana ya ultra targeting?

Hii ni namna ya kuchagua ni watu gani wa kuwaonesha tangazo lako ili kuweza kuokoa pesa za matangazo.Matangazo ya redio au t.v huwa yanaenda kwa yeyote aliyewasha t.v au redio halichagui mtu wa kumfikia. tangazo linamfikia na piaMatangazo haya hayawezi kukuonesha ni aina gani ya watu wamevutiwa na tangazo lako zaidi kutokana na tofauti ya kijinsia,umri na mambo ya kijamii mtu anayopendelea.Hizi ni takwimu muhimu sana katika kufanya marketing.

View attachment 1213430

Ukiangalia hapo takwimu zinanionesha matumizi ya pesa yangu pamoja na idadi ya watu waliofikiwa kwa kutengenisha jinsia pamoja na umri.Kwa maana hiyo ninapokuja kutangaza kwa mara nyingine ninaweza kujua ni aina gani ya watu natakiwa kuwa target na watavutiwa na biashara yangu.

Hii ni sawa na kusema nataka kuweka biashara yangu kwenye eneo wanalokatiza sana sana wanauma wenye umri kuanzia miak a65 na kuendelea ..suala ambalo ni gumu kidogo. Katika matangazo ya redio au t.v huwezi weka tangazo la namna hiyoo.

Au ni sawa na kwenda kituo cha redio au tv na kuwaambia naomba tangazo langu lionekane kwa wanaume tu wenye umri kuanzia miaka 45..ni suala lisilowezekana.

Matatizo hayo ndio digital marketing imekuja kuya solve.Unaweza kuweka tangazo na kutaka lionekane kwa jinsia fulani tu au umri fulani tu au watu wa eneo fulani tu.

View attachment 1213437

Ukiangalia mfano wa hapo juu.Labda mimi ninamiliki duka la nguo au bidhaa za akina dada. Au tuseme huduma tu inayowalenga wanawake na ninahitaji kupata wateja waliopo maeneo ya magomeni tu. Hapo tangazo langu litawafikia wanawake tu wanaoishi maomeni wenye umri wa kuanzia miaka 25-45. Na ukiangalia ninaweza kuwafikia watu 1700 - 4900. Na hapo ni gharama isiyozidi dollar 5 (Tsh 12,000).

Katika hali hii unahitaji kugombania fremu kariakoo.Hali ya kuwa unaweza kufanya marketing kwa mwezi (12,000 * 30) ni 360,000/= Hali yakuwa uko kitandani kwako tu bila kufukuzana na wateja bali wao wanakuja tu katika store yako tu.

Huo ni mfano tu wa bidhaa mojawapo niliyoamua kutolea mfano.Ila suala hili unaweza kufanya katika bidhaa au huduma yoyote ile.
Tufahamu ya kuwa katika nchi zilizoendelea maduka ya mitaani yanafungwa na kuhamia online.

View attachment 1213512



Tajiri namba moja duniani kwa sasa jeff bezos mmiliki wa amazon ndio anaofanya watu wafunge maduka yao huko marekani.kwakuwa bidhaa nyingi zinauzwa online katika website yake.

33% YA e commerce inayofanyika duniani inapita amazon.. Na hili ndio litakuja tu katika nchi zetu japokuwa haiwezi kuwa leo au kesho au mwakani..ila unaweza ukalifanya na matokeo yake utayaona.

Nahisi nimeandika mengi japokuwa kuna maeneo ninaweza kuwa sijayagusa kwa kiasi fulani naamini wapo wadau wengine watakaokuja kuongezea.
NImeamua kushare fursa hii kwakuwa mimi mwenyewe ninaitumia katika shughuli zangu.

Najua wengi wetu ni wageni wa masuala haya ya mitandao na digital marketing hii inawafanya wasiweze kutumia fursa hii adhimu ya teknolojia.

Ikiwa wewe ni miongoni kati yao nakukaribisha sana kwa ushauri na hata msaada wa namna ya kufungua na kuanzisha online business na kutumia fursa hii ya teknolojia kukuza na kuendeleza biashara yako ya sasa.


Imeletwa kwenu na:

Jaffari Yusuph
Digital Marketer | Online Entrepreneur | Programmer | Web & Mobile App Developer
KARIBUNI SANA.

0782 780 980 AU 0677 81 82 83

Asante kwa somo zuri mno!
Nitakutafuta !
 
Kongole kwako mtoa hoja.
Binafsi nipo kwenye mchakato wa kufanya digital umesoma kama freelancer. Nimeshasoma courses kadhaa gogle na coursera na nyingine naendelea nazo. Then ntatafuta uzoefu kabla ya kuanza kutafuta clients.
 
Back
Top Bottom