Baada ya wanyama kuwa na maisha yasiyoeleweka ya mkanganyiko mkubwa ilifikia wakati mzee tembo kuitisha mkutano na kupendekeza achaguliwe mnyama atakayekuwa kiongozi wao ili kupeleka maisha yao mbele.
Ulipoitishwa uchaguzi wanyama wote walishiriki katika uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na kuwa na haki ya kuchaguliwa/kugombea nafasi mbalimbali za uwakilishi wao.Baada ya kumaliza zoezi la kupiga kura ikaonekana dhahiri kuwa mnyama Simba ameshinda kwa kishindo na kutawazwa kuwa mfalme wa nyika,na ndio maana toka zama za kale hadi sasa Simba anajulikana kama mfalme wa nyika japokuwa wapo walio na maumbile makubwa kama tembo,kifaru,nyati n.k.
Baada ya Simba kutawazwa mfalme wa nyika akaamua kuitisha mkutano mkubwa ili aweze kutoa shukrani kwa wanyama wote kupitia wale waliopo msituni na kueleza kipaumbele cha utawala wake.
Cha ajabu ikatokea wanyama wadogo waitwao Digidigi wao hawakukubaliana na utawala wa Simba kwa madai kuwa Simba ndiye anayeongoza kuwashambulia na kuwatafuna Digidigi hao sasa iweje leo apewe dhamana ya kuwatalawa!Kwa mujibu wa Digidigi hao jambo hilo ni sawa na kumpa rungu kichaa.
Wakati simba anaandaa makabrasha yake aanze kuchana verse,Digidigi hao makundi kwa makundi wakatoka katika ule mkutano na kuwaacha wanyama wengine wakiwadhihaki kuwa 'mnamuuzi mchinja mbwa,mjue wazimu utawarudia'.
Tokea siku ile basi ikawa ni mawindo ya Digidigi kila anapoonekana,Simba,Chui,Fisi n.k ni lazima wawashughulikie hata kama hawana njaa.