MMASSY
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 290
- 196
Mwalimi Julius Kambarage Nyerere(RIP) Alitufundisha kupitia ahadi za mwana TANU kuwa Afrika ni moja na Waafrika wote ni ndugu zangu. Binafsi nimekuwa na tafsiri tofauti kwa mtazamo kuwa kinachofanyika Nigeria hadi Johanesbourg kinafanana na kinachofanyika Jamhuri ya Africa ya Kati hadi daslamm.
Leo nimekesha nikisoma taarifa ya ufisadi wa aliyekuwa waziri mmoja katika serikali ya Jonathan wa Nigeria. Nimelazimika pia kusoma taarifa ya hali ya matajiri duniani katika jarida maarufu la Forbes.Katika jarida hilo, taarifa yake ya mwezi huu inaonyesha kuwa mtu tajiri kuliko wote duniani ni Billgate mwenye utajiri wa Dollar billion 79.2, kwa Afrika mtu tajiri kuliko wote ni Aliko Dangote mwenye utajiri wa dollar billion 14.7.
Sasa taarifa ya CNN imemkariri mwanamke mmoja machachari huko Nigeria aliyekuwa waziri wa masuala ya mafuta wa Nigeria Diezani Alison na mwanamke mweusi wa kwanza kuwa katibu mkuu wa OPEC.Serikali mpya ya Buhari ilianza kufanya uchunguzi dhidi ya huyu mama kwa scandal ya upotevu wa zaidi ya dollar billion 90. Yeye huyu mama msomi amedai kuwa hataki kelele atazirudisha zote yani 90$bn.
Afrika ni moja na waafrika wote ni ndugu zangu.Yani fedha alizoiba huyu mama ni zaidi ya utajiri wa Billgate wa dunia kwa dollar billioni 20.Kwa fedha alizoiba huyu mama anamzidi Dangote mara saba ya Dangote aliyetajiri kuliko wote Africa.Naendelea kuamini kuwa uongozi Afrika ni dili.
Nigeria ina watu millioni mia moja sabini, kwa fedha tu alizoiba waziri mmoja zingetosha kuwagawia kila mwananchi millioni 159 kwa miaka kadhaa wakaendeshea maisha yao.Nigeria ni moja ya nchi ambazo wananchi wake wanapitia umaskini mkubwa pamoja na kuwa na mafuta kibao.Mwanamama huyu alikuwa mstari wa mbele kutetea serikali ya Jonathan na kipindi cha kampeni alitoa fedha kibao kuhakikisha chama chao cha PDP kinashinda.Wananchi walisimama kidete na kuiangusha serikali ile.Leo hii chama pinzani kimeibua na kushinda wizi wa chama kilichotawala miongo kadhaa.
Picha ya Nigeria inampa changamoto moja kubwa rais wangu JPM wa #hapakazitu# kumulika mawaziri wake na waliomtangulia.Kuna ambao wako CCM na wengine upinzani.Yeye anayonguvu ya kupambana kurudisha rasilimali za nchi hii zilizomilikishwa wachache.
Naomba niishie hapo kwa leo ila endelea kutafakari na kuchukua hatua.
Niendelee kusoma nipate hasira.