Did they actually land on the moon ?

duh........JF kiboko!!sie dotcom huwa tunakaririkarri tu hivi vitu, lakini anyway maisha yanasonga
 
Afadhali umewaka wazi, watu wengi wanapenda kukubali tuu mambo wanayosoma bila kutumia akili zao za kuzaliwa kufikiri kwa kina. Wewe angalia tuu kompyuta zenyewe za miaka ya sitini zilikuwa kubwa kama nyumba na zilikuwa hazina computing power kama zilizopo kwenye smartphone, sasa unafikiri walikuwa na hiyo tekinolojia ya kupelela mtu mwezini? kitu kidogo tu kama ku-print document ambacho kinachukua sekunde kilichukua days miaka ile.

Umezumzia suala la mionzi (radiation), hivi kweli watu wanaelewa kiasi cha mionzi kilichopo huko angani katika umbali ule na jinsi ambavyo ingeweza ku-ionize delicate elecronic circuits za shuttle, hata kama vilikuwa na radiation shield, uwezekano wakuharibika ulikuwa mkubwa. Kumbuka tunaongelea miaka ya sitini hapa.

Hapo kwenye red; mkuu acha kusikiliza story za vijiweni!
 
Kukujibu maswali lako labda nianze hivi
Haya mapinduzi yote ya kwenda space yalianza tu baada ya vita ya pili ya Dunia, na ukweli juu ya hiyo ni kuwa, Hitler alikuwa yupo Advanced sana katika modern sciences by that time, Ukiangalia documentary na history mbalimbali za Hitler yeye alishafikia kwenye stage ya kutengeneza Jet engine, computers na vitu vingine vingi japo dunia ya Waamerika na Warusi walikuwa Hawajafikia hiyo stage

Wakati Warusi na Wamarekani na jamaa zake (Waingereza na Wafaransa) wanaingia German, Warusi waliingia upande wa East na wamarekani upande wa West, na walikutana Berlin na hapo ndipo ulipokuwa mpaka wa East na West German (Ukuta wa Berlin), Lakini Warusi ndio walikuwa wa Kwanza kuingia Berlini na walifanikiwa kuingia kwenye ma-Bunker ya Hitler na kuwakuta wanasayansi wengi wa Hitler Pamoja na Modern Equipments ambazo hata kwenyehiyo vita zilikuwa hazijatumika bado na wala wao (Warusi) hawakuwa nazo, Warusi walichukua vitu vingi pamoja na hao wanasayansi, Marekani alikuta mabaki tu na kwa miaka mingi ya mwanzo baada ya vita ya pili ya Dunia Marekani walikuwa wanaangaika kuwatafuta wanasayansi wa Hitler ili waweze kuwatumia kwenye mambo yao ya kisayansi

Warusi waliweza kuwatumia vizuri sana wanasayansi wa Hitler kwenye sector ya Silaha na hii ya Space, Robot, Computer, Jet engines nk, kiwango alichokifikia Mrusi kwenye sayansi hiyo kwa kipindi kile ilikuwa juu sana Zaidi ya Wamarekani na ndio maana hao Warusi ndio wanaonekana kama baba wa Space

Kwa kujibu maswali yako

1) Sio kwamba hiyo Technologia ya kwenda Mwezini na kurudi kwa sasa kuwa hipo, bali hata miaka ile ya 50’s na 60’s hiyo technologia ilikuwepo
Mwaka 1957 Warusi ndio walikuwa watu wa kwanza kuweka satellite kwenye orbit
1957 walifanikiwa kupeleka kiumbe hai (Mbwa-Laika) kwenye space
1961 chombo cha kwanza chenye mtu (manned spacecraft) kwenda Space na kufanya Mzunguko kwenye orbit (hapo alikuwa ni baba wa Space Yuri Gagarin alikufa 1968 kwenye crash ya MiG-15)
Mwaka 1965 mwana mama Valentina (mwanamke wa kwanza space), na mwaka huo huo Leonov alikuwa ni mtu wa kwanza kutembea space, pamoja na hayo yote Warusi walishapeleka Chombo mwezini na Maroboti na walikuja na evidence za 326g za mawe ya mwezini

Baada ya Wamarekani kuona hayo mafanikio makubwa ya Warusi na Wajamaa wote Duniani (Kumbuka dunia ilikuwa kwenye vita baridi), kwao ilikuwa haina budi kutengeneza kitu kikubwa cha kuweza kuiangusha Urusi kwenye hiyo record na ndio kisa cha kutengeneza hiyo movie ya Apollo 11 ndani ya jangwa la Nevada kwamba wamefika mwezini na kupata kilo 382 za mawe ya mwezini zaidi gramu 326 za Warusi (WaAustralia walikuwa na evidence nyingi mno za Apollo 11 kwani by that time wao walikuwa na uwezo wa kupata picha na sauti safi kutoka Jangwani Nevada ilipokuwa inafanyika hiyo movie kwani wamarekani waliirusha live, -NASA wamejitahidi kwa miaka mingi kuzitafuta kopi ili waziharibu- kwani kuna kipande cha picha za mwezini kilikuwa na Kopo la Cokacola)

Kwa hiyo uwezo wa kwenda na kurudi upo ila Warusi walishafanya research kubwa sana ya space na conclusion ilikuwa ni vigumu sana kwa kiumbe kuweza kufika na kutembea juu ya mwezi miongoni mwa hiso sababu ni Radiations/Cosmetic rays, Solar flares na Solar Winds

2) Trip ya Kwenda Mars kwa (Unmanned spacecraft) inawezekana kabisa kuwa ya ukweli, japokuwa Wamarekani ndio waliotuma hicho kitu (Rover) Mars lakini Dunia nzima hasa ile yenye technologia (Russia, China na hata Japan) pia walifanikiwa kupata picha za huko through that Robot
Lakini Tatizo la kupeleka mtu kule (Mars) linabaki palepale (Radiations/Cosmetic rays, Solar flares na Solar Winds) na Tatizo lingine linalijitokeza ni Uzito wa chombo kitachoenda na mtu Mars (Consumables na fuel), niliwahi ona Documentary iliyotoka NASA to Puplic walikuwa wanazungumzia uwezekano wa kutengeza chombo ambacho kitakuwa na mechanism ya kuibadilisha hewa ya huko (N, H, C) pamoja na O2 ili kuwa Fuel itakayotumiwa na Hicho chombo wakati wa kurdi Duniani, yaani kitaenda na mafuta kidogo tu ya kufika huko na mafuta ya kurudi yatengenezwa huko huko

ni story nzuri anyway

Kwa jinsi maelezo yako yalivyo, hili jambo unalielewa kwa kiasi kikubwa, sijui ni kwanini unatumia uelewa wako ku-twist ukweli na kuwaingiza wenzio chaka. Yaani story yote umekwenda nayo vizuri sana ila mwisho, kwenye sinema ya nevada, ndipo ulipoacha njia kuu. Tafadhali kamalizie kupitia reference zako vizuri.
 
Tunaweza kukubali kwamba wamarekani walipiga fix kipindi hicho, Lakini landing on the moon is very possible.
 
Qur-an; sura ya 19 aya ya 57 " Na tulimuinua daraja ya juu." ushahidi unaonyesha safari ya kwenda juu ilianza mwaka 1957 (19 ni sura 57 ni aya)
 
Hata Mimi siamini kwamba wamarekani walienda coz ukiangalia video yake kuna bendera ya marekani iliwekwa na ikawa inapepea but kwa physics ya form 2 katika space hakuna hewa sasa bendera ilipepea kwa upepo gani?
Pia hata sauti ya Apollo ilikuwa inasikika katika video but sauti haipiti katika space so how?
Kwa kifupi kidogo tu hivo tukiacha sababu nyingine siamini Kama walifika mwezini
Semeni wadau
 
AldrinFlag1a.jpeg
 
I am also skeptical about the issue. It is probably the Us=NASA did not land a man on the moon in 1960's.
 
Hata Mimi siamini kwamba wamarekani walienda coz ukiangalia video yake kuna bendera ya marekani iliwekwa na ikawa inapepea but kwa physics ya form 2 katika space hakuna hewa sasa bendera ilipepea kwa upepo gani?
Pia hata sauti ya Apollo ilikuwa inasikika katika video but sauti haipiti katika space so how?
Kwa kifupi kidogo tu hivo tukiacha sababu nyingine siamini Kama walifika mwezini
Semeni wadau

sauti inapita nani kakuambia haipiti,na bendera inapepea who said haipepei ni physics gani unatumia?
 
Swali kubwa la kujiuliza kama wamarekani walishafika huko late 1960 na wana interest ya kwenda huko mbona hawakwenda tena na atempt zote zilizofuata Apollo 11 zilifail Americans bado wana explore jinsi ya kufika Mwezini

no one wants to go back due aliens landing over there and is due to fear on them too,the moon has got storms ,the moon has weird characters that are irrelevant to scientists knowledge,they dont want war with the space angels(aliens) they were warned,AND ITS TRUE AMERICANS LANDED ON THE MOON
 
Hata Mimi siamini kwamba wamarekani walienda coz ukiangalia video yake kuna bendera ya marekani iliwekwa na ikawa inapepea but kwa physics ya form 2 katika space hakuna hewa sasa bendera ilipepea kwa upepo gani?
Pia hata sauti ya Apollo ilikuwa inasikika katika video but sauti haipiti katika space so how?
Kwa kifupi kidogo tu hivo tukiacha sababu nyingine siamini Kama walifika mwezini
Semeni wadau

1.maelezo yako yanajichanganya.

2. Physics ya form two ipi wanafundisha mambo ya space?au mimi ndio nimesahau physics form si mambo ya newton,heat,expansion,energy,power?

3. Jifunze kutofautisha kati ya space na atmosphere.

4. Space ya kitu gani haina hewa?
 
Kuna dokumentari moja
niliiangalia mwakajuzi mwishoni, ikielezea uongo wa kufika mwezini. Vitu ambavyo vilikua vidhihirisha ni 1. Mwendo kasi wa upepo, ambao ulioneshwa hasa na bendera.
2. Kujiakisi kwa picha ya wapiga picha kwenye vioo vya kofia walizo
vaa.
3. Alama za viatu tofauti. Kwenye mwezi,
4. Uwezo wa kuizuia mionzi hiyo, kwakipindi kile.
5. Vivuli, ambavyo vilitofautiana mtu na chombo hicho,


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hata Mimi siamini kwamba wamarekani walienda coz ukiangalia video yake kuna bendera ya marekani iliwekwa na ikawa inapepea but kwa physics ya form 2 katika space hakuna hewa sasa bendera ilipepea kwa upepo gani?
Pia hata sauti ya Apollo ilikuwa inasikika katika video but sauti haipiti katika space so how?
Kwa kifupi kidogo tu hivo tukiacha sababu nyingine siamini Kama walifika mwezini
Semeni wadau

Do you watch Myth Busters?!
 
JF inanipanua upeo mno zaid ya shule kunanifanya nisumbue vilaza wezangu kitaa maana wao watu wa kukariri tu mi ndo naonekana msomi sasa na hii kesho naamka nayo kijiwen
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom