DID GIANTS EXIST? Historia ya Majitu ya Kale

Ahsante kwa mchango wako lakini hapa bado inaniacha na maswali kidogo labda uniweke sawa

1. Kama waliangamizwa na gharika je hao 'MAJITU' yaliyokuja baada ya gharika mfano Goliath au Mfalme Ogu walitokea wapi??

2. Kama walitokana na malaika ina maana malaika walizaa upya na wanadamu baada ya gharika??

3. Kama walikuwepo baada ya gharika je kizazi chao kimeishia wapi kiasi leo hatunao tena duniani??

Tutoe tongotongo kidogo
kuna sehemu nilisikia kuna jitu moja ndio liliobaki ambalo maji yalikuwa yamemfikia kiunoni lililopewa kazi ya kuizuia ile safina isiweze kwenda mbali,naujiulize kwanini baada ya ghalika safina haikwenda mbali na eneo lile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
No ili jitu lilibaki nafamilia yake mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo sina uhakika ila Bible inaeleza alikuwa na miji zaidi ya 11 na ufalme wake kabisa ikimaanisha alikuwa na watoto na mke ila sijafahamu kwa ukubwa huo alitoa wapi mke?? Au kama alipona na mnefili mwenzake au walizaliwa wanefili wengine kupitia Ham ndio akaoa humo bado ni kitendawili mkuu

lakini kwa maoni yangu nadhani alipona peke yake ila alipata mke kupitia kwa watoto wa Ham ambao Biblia inawatambua kama Wanefili pia yaani GIANTS mfano caphtor alimzaa giants hadi goliath ni wa ukoo huo na alitokea kwa Ham, pia Giant kama Rapha aliyezaa warefai ambao waisrael walijiona kama panzi mbele yao nao walikuwa uzazi wa Ham so nafkiri jibu langu ndio hilo

Ubarikiwe
 
Habari za asbuhi wana jukwaa, niende moja kwa moja kwenye mada kama kichwa cha habari kinavyosema je Giants/Majitu makubwa yanayoelezwa kufika hadi futi 45 waliwahi kuishi hapa duniani?? na kama waliwahi kuishi walitoweka wapi?? Na kwanini siku hizi hawazaliwi tena??

Hadithi za uwepo wa hawa watu zipo karibu katika kila kabila na jamii hapa duniani kwa mfano wahispania wana historia ya Giant (basajaun) ubelgiji alikuwepo antigoon, indonesia (Buto), waebrania (Goliath), Irimu wa wakikuyu na Yalmavuz wa uturuki nikitaja kwa uchache.

Hata vitabu vya kidini na kihistoria zimewaongelea hawa watu embu tuone mifano kidogo

WANEFILI
Mwanzao 6:4
4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa

Kwa tafsiri ya kiingereza

Genesis 6:4
4There were giants in the earth in those days; and also after that, when the sons of God came in unto the daughters of men, and they bare children to them, the same became mighty men which were of old, men of renown.

Inaelezwa watu hawa walikuwa ni majitu makubwa yenye nguvu yanaongelewa pia kwenye vitabu vya kihistoria kma Book of giants tunaona watoto wa Semyaza kina ohyah na hahyah walikuwa ni majitu makubwa sana yanazidi futi 100!!!..... Pia kitabu cha Enoko (book of watchers) anaongelea watu hawa ambao walikuwa ni wakubwa sana na walikuwa wakitesa wanadamu maana walidai vyakula kuliko viwango vyao vya uzalishaji na wakaanza hadi kuwala wanadamu wenyewe.... So dunia ilijaa vurugu tupu kipindi cha kabla ya gharika sababu ya hawa WANEFILI

2. WANA WA ANAKI (ANNUNAKI)
Kwenye vitabu vya dini hawa pia wanaongelewa kama WANEFILI ambao ni majitu marefu yenye nguvu sana

Hesabu 13:33
32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.
33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.


Walisema haya baada ya waisraeli kutuma wapelelezi kwenda kukagua nchi ya kanaan iliyokaliwa na wana wa Canaan mtoto wa Ham wakiwemo Waamori,waamaleki,wayebusi,wahiti,Hivitites,Gilgashites n.k ambao kwenye biblia wanaelezwa kma majitu makubwa na marefu yaliyoishi Canaan kipindi waisraeli wanataka kurudi kwenye nchi yao ya ahadi

Amos 2:9
9 Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini

NB:Mierezi ni miti mirefu sana sasa iliopatikana huko lebanon

QURAN TAKATIFU
Mfano ambao upo ndani ya Quran ni Mfalme Og wa Bashan au kwa kiarabu alifahamika kma Uj ibn Anaq huyu alikuwa mfalme wa kale ambaye alikuwa ni mrefu sana na ana mwili mkubwa tunaambiwa alikuwa na futi 13 na alikuwa na nguvu sana,pia kwenye Quran anatajwa Jitu linaitwa Jalut ambalo nalo linaelezwa alikuwa mtu mkubwa mwenye maguvu sana kuliko umbo la kawaida la mwanadamu.

GILGAMESH
Huyu ametajwa na Enocko kwenye book of giants kwamba alikuwa ni JITU kubwa sana lenye manguvu kiasi kwamba lilitangaza vita na Mbingu..... Inadaiwa alitawala ufalme wa sumeria (Uruk) enzi za kale na alitawala kwa miaka 126... Ana stori ndefu kidogo itabidi afunguliwe uzi siku moja (Epic of gilgamesh) ila kwa leo nimemtaja tu kma mmoja ya GIANTS

USHAHIDI WA KISAYANSI
Hii ni baadhi ya mifano tu ili twende pamoja... Na baadhi ya tafiti zimefanyika wamepata ushahidi wa miji walioishi hawa wanefili ambayo majengo yao tofali moja tu haliwezi bebwa na kifaa chochote cha sasa hivyo wameconclude ulijengwa na MAJITU haya ndio pekee yana uwezo wa kubeba tofali kma zile miji hii mfano ya maeneo hayo ni magharibi wa mto yordani, Pia Hebron, mesopotamia na maeneo ya mashariki ya kati. Kwa maeneo zaidi angalia kiambatanisho cha video hapo chini kuhusu majengo hayo afu uniambie kma mwanadamu wa kawaida angeweza kujenga kulingana na technologia ya kipindi kile!

Pia ushahidi mwingine ulipatikana na mtafiti Georges Vacher de Lapouge na mifupa akiita Giant of castelnau... Mifupa hiyo kwa picha inaonekana ni ya kibidanadam ila ni mikubwa kuliko ya mwanadamu wa kawaida maana estimation ilifika futi 12 hivi ya urefu kwa kutumia mifupa hiyo ya miguu

WALIISHIA WAPI HAWA MAJITU??
1.Kwenye vitabu vya kihistoria na dini wanadai kwamba wanefili walikufa kwenye gharika la Nuhu ila cha kujiuliza kma kweli walikufa kwenye gharika walirudije baadae mfano hao waamori au wayebusi walikuwa ni wanefili (wajuzi mtusaidie hapa)

2. Kuendana na kitabu cha Joshua tunasoma kwamba alidhamiria awaangamize wote ili waweze kuiteka Canaan na kuiweka mikononi mwao..... Ila tunaona HAKUUA wote sababu wengine walikimbia hivyo waliachwa wakaishi miji ya kusini (Gaza ya sasa)

Maswali ya kujiuliza

Je asili yao ni nini mpaka wakawa wakubwa hivyo??

Je uzao wao uliishia wapi??

Je watu hao walikuwepo kweli??

Je kwanini siku hizi hawazaliwi tena??

Ahsanteni kwa kusoma,karibuni kwa michango View attachment 748594 View attachment 748595 View attachment 748596 View attachment 748597






CC wanajukwaa wote bila kuwasahau
Malcom Lumumba, hearly Da'Vinci ,Te Lavista,Kiranga Elungata ,nyabhingi ,Mchawi Mkuu,Eiyer ,Mshana Jr n.k

Giantism Never Die, Shall Survive and Stay Alive Forever and Ever!!! Sisi sote tunaishi kwenye falsafa hii ya Ujitu. Sisi ni Giantists!!
 
Giantism Never Die, Shall Survive and Stay Alive Forever and Ever!!! Sisi sote tunaishi kwenye falsafa hii ya Ujitu. Sisi ni Giantists!!
Finally we have a giant to adress our queries haahaaa (kidding thou).

In the light of the giantist philosophy, can u elaborate more; It sounds enticing to say the least.
 
Ume
Roho haizaliwi ila inazaliwa kwa mwanadamu kama ikiwa ndani ya mfumo wa mwili kwa hiyo Yesu ni Roho kweli ila kwakuwa alipokuja duniani hakuja kma MZIMU ila MWANADAMU hivyo aliweza kuzaliwa sababu alikuwa kwenye form ya MWILI

Hata wewe una Roho ndani ya mwili na siku ukifa Roho inatoka na mwili unabaki hivyo kabla hujazaliwa unakuwa roho ila ili uingie duniani unavaa mwili same case kwa Yesu

Pia Yesu si malaika ila wote ni ROHO/DIVINE BEINGS so wana tabia zinazofanana

Moja kauliza kama malaika wana sex?? Wakiwa kwenye form ya malaika hawawezi ila wakivaa mwili kma wwe ulivyovaa mwili basi wanaweza kusex na mwanamke au mwanaume

Hata kwenye biblia tunaona malaika wakimtembelea Abraham walikula,waliomba maji,walipumzika,walinawa n.k hivyo wakishavaa miili ya kibinadam wana uwezo wa kufanya kila kitu ambacho unaweza kufanya

Hope nmeeleweka
umesema yesu sio maraika ni nanituambie sasa tujue jua tuuh maraika ni son of god
 
Habari za humu wanajamvi, naamin mu wazima wa Afya, leo naomba kuwashirikisha Kuhusu unyanyasaji wa hawa ACACIA ambaye ni mshirika wa AFRICAN BARICK GOLD(ABG) ambao wanamiliki migodi ya dhahabu kamavile Buzwagi Gold mining, Geita Gold mining na Bulyanhulu Gold mining huko Kakola,kutokana na kazi mbalimbali za mgodini, hutokea wafanyakazi kupata ajali au ulemavu. Kwa mfano kuwa kiziwi, kuvunjika viungo vya mwili,matatzo ya uti wa mgongo, hii hutokea kutokana na uendeshaji wa mitambo mikubwa ndani ya mgodi.

Baada ya mfanyakazi kupata ulemavu, ACACIA huwaweka ktk makundi mawili, temporary disability na permanent disability. Kisha huwaachisha kazi kwa sababu za kiafya(medical reason) sasa makundi mawili yote hulipwa fidia, lakini yule mwenye temporary disability yeye hupata tiba, mfano aliyevunjika mguu, akishapata matibabu na kupona, analipwa fidia tu, Lkn mwenye permanent disability yeye hulipwa fidia, lkn ACACIA wanaendelea kumtibia na kumlipa hela ya matibabu ikiwemo na kumsimamia tiba ta vitendo(physiotherapy)

Kutokana na gharama kubwa za fidia, ACACIA hukwepa gharama hzo kwa baadhi ya wagonjwa kwa kuwafukuza kazini kwa readon ya utoro au kumsingzia wizi. Hili linanishangaza sana sababu hii ni kampuni kubwa, wamiliki n wazungu, viongozi wa ACICIA kwa sasa wengi ni wabongo, hawahawa wabongo ndo huwachapa rungu wafanyakazi walemavu na wagonjwa kwa kuwafukuza / kuwaachisha kazi kwa reason ya utoro ama kuwasingzia wizi, Pia ili kukwepa gharama za kuwahudumia ,ACACIA huwalipa fidia chache tu wahanga, pia baadhi ya watu walopata permanent disability huacha ghafla kuwasimamia matibabu endelevu kwa:

1.Dr. wa kampuni kuidhinisha/kupotosha kuwa mgonjwa kapona
2.Kutoa rushwa kwa ma~physiotherapist wa hosptal za rufaa,ili watoe ripot kuwa mgonjwa kapona
3.Kutoa rushwa kwa watendaji ama medical officer wa OSHA(Hii ni mamlaka inahusika na kusimamia haki za wafanyakazi waloumia katka mazingira ya kazi) sasa huyu daktari wa OSHA hupotosha kuwa ULEMAVU WA MGONJWA HAUJATOKANA NA KAZI ZA BUZWAGI.
4.ACACIA huhonga mahakimu ama mawakili wa wagonjwa ili kesi iishe haraka, why, ili ACACIA isichafuliwe mbele ya serikali kuwa inanyanyasa wafanyakazi. Na hili huwa wanawatamkia wagonjwa waziwazi kuwa ata ukifungua kesi hutafika popote.

Mgonjwa akiwa na BACK-UP KUBWA, huwa wanamuita na kumwambia aifunge kesi ili wamlipe kiasi akitakacho #mfano milion 200 ili kesi iishe, kisha walalahoi wasokuwa na back~up hufyekelewa mbali.

Baadhi ya wagonjwa hawa hukomaa na kesi, mwishowe hela sa kusafiri kwenda mahakaman(mahakama kuu au ya rufaa) huwa wanakuwa watoro kesi zikitajwa hivyo ACACIA huibuka mshindi.

kwa hiyo kuna kundi kubwa la wafanyakazi walopata ulemavu kazini, wakatelekezwa na kampuni.
NB#
KTK ACACIA NA MIGODI MINGINE MIKUBWA, WAFANYAKAZI WOTE HUPIMWA AFYA YA MWILI NA AKILI, HII NI PAMOJA NA UTIMAMU WA VIUNGO VYA MWILI, MTU AKIFUZU VIPIMO HIVI MARIDADI NDIPO HUSAINISHWA MKATABA NA KAMPUNI, KWA HIYO MTU AKIWA NA TATIZO KIMWILI ,KIAFYA KAMWE HAWAMWAJIRI.

nmekulia mazingira ya migodi hii ya ACACIA, na baadhi ya wahanga nawajua, wiki hii nmebahatika kukutana na mmoja wao, ambaye ni mama wa watoto wawili, yeye aliajiriwa na AFRICAN BARICK GOLD,(kipindi hicho bado ACACIA hajachukua madaraka)

ilikuwa ni 2012, alipasi#KUFUZU vipmo vya mwili,afya na akili, hivo akaajiriwa kuendesha mitambo mikubwa mikubwa(HEAVY MACHINE OPERATOR), (miezi mitatu ya kwanza unakuwa chin ya uangalizi,baada ya hapo unakuwa permanent employed.)
Alifanya kazi kwa weledi wote, lkn miaka miwili baadaye, alianza kupata maumivu ya mgongo, ilikuwa 2014, mwanzoni wa 2015 aliletwa Dar es salaam, MOI kwa vipimo,alisafirishwa na ndege ya kampuni akiwa na wafanyakazi wengne wagonjwa.

ambapo baada ya kupimwa MRI NA CT SCAN ,ilijulikana kuwa , mifupa ya uti wa mgongo iliyo L3&l4(L=lumbar area) imesagika, mild bifecetal arthritis.. hivo akaandikiwa dawa na ahudhurie physiotherapy. Madaktari wa muhimbili, MOI walisema chanzo mojawapo cha tatzo ni kuendesha mitambo yenye mitikisiko mikubwa.

hivyo alirudi Kahama, akaendelea na dawa na kuhudhuria physiotherapy(Akitumia bima ya kampuni,ACACIA wanatumia bima ya afya ya AAR HEALTH INSUARANCE)

alipokuwa akijiuguza ,ilipelekea asiende kazini, hivyo HR wa ACACIA akamuachisha kazi kwa reason ya UTORO na arirudsha ID ya bima ya AAR. lkn huku ACACIA wakijua ni mgonjwa.

2015 akafungua kesi mahakama ya mwanzo kahama, kesi ikahamishiwa shinyanga, baada ya mikiki mikiki ya kesi , 2017 yeye na wenzake baadhi walishinda kesi hivo ACACIA wakawalipa fidia ya kuwasababishia ugonjwa kazini. lkn pia huyu mama ilitakuwa aendelee kupatiwa matibabu na ACACIA, ACACIA wakagoma kuwa Disability haijasababshwa na kazi, mwaka 2017 kwa Gharama zake bnafisi alijuja Dar es salaam, MOI, kurudia vipmo vya MRI, NA CT SCAN ,ambapo madaktari wa MOI wakagundua madudu mengne ambayo yalifichwa na ripoti ya mwanzo iliyoratibiwa chini ya usimamizi wa ACACIA, madaktari wakasema siyo tu kuwa ana bifecetal arthritis between l3&l4, bali pia ana DISC PLORAPSE BETWEEN L3&L4
hivo anahitaji operation haraka la sivyo hatatembea tena akikawia operation. Operation inagharimu zaid ya million 4.

hivo huyu mama Jane feza arirudi ACACIA kuomba wamtibie kama sheria na katiba inavyosema, wakakataa kuwa tatizo lake halijatokana na kazi, Bi Jane Feza alienda kuwashitaki OSHA. huko OSHA nao walimzungusha na dalili za rushwa zikionekana.

Wiki ilopita ACACIA walimpigia simu kuwa aende OSHA kufata conclusion ya suala lake, sintofahamu ingne, ni kuwa walimpatia nauli elf 60 nauli ya Bus kutoka Kahama kuja Dar es salaam, why ? mgonjwa wa uti wa mgongo asafirishwr kwa basi? why asilipiwe ndege kana awali? badi Jumapili kaja Dar. kwa basi, walimlipia hoteli, jumatatu apumzike, jumanne aende OSHA kufata majibu. Jumanne tar 8 january 2019 alifika Ofisi za OSHA kinondoni, wailimpatia ripoti ya suala lake kuwa HALIJATOKANA NA KAZI ZA BUZWAGI GOLD MINE. Tafsiri ni kuwa ACACIA isihusike na kumtibu, BAADA YA KUPATA RIPOTI HIYO BI JANE FEZA ALIZIMIA, Daktari wa OSHA akampeleke hospitali jirani ya KINONDONI HOSPITAL ambapo alipata first aid, akazinduka, hospital ikahitaji malipo, Osha wakasema MWAJIRI WAKE ACACIA WATALIPA, kweli wanalipia care anayopata hapo kinondoni hospital, madaktar wa hapo wameshauri wampe rufaa kwenda MOI ili apate operation ya tatzo lake, maana sasa ananyanyuka kwa shida, akikawia hatatembea tena, ACACIA WAMEGOMA KUGHARAMIA OPETATIPN, WANATUMIA RIPOTI YA OSHA KUMNYANYASA.

Surely kuna harufu ya rushwa toka ACACIA kwenda OSHA.
nimemuuliza , acacia wanalipa gharama za kulazwa na chakula, akasema wanawapigia simu ACACIA, mpaka kaka yake JOSEPH FEZA akoromeane nao ndo wanatuma elfu 30 ya chakula, wakat mwingine hawapokei simu.

lkn pia amesema tokea 2015 hawez kuinama,kufua na kufanya kaz za nguvu, musa wote ananunua dawa alizoandikuwa MOI ili kupunguza maumivu ya mgongo na miguu, dawa hizo ni Neurotone,Prigabalin na ketoprofen gel ya kuchua.

SASA WANAJAMVI, TUMSAIDIE BI JANE, HILI SUALA LIFIKE KWA RAIS MAGUFULI NA WIZARA YA KAZI ILI BI JANE FEZA APATE OPERATION NA ACACIA WAENDELEE KUMTIBU. NTASOMA KILA MAONI YENU, PUCHA CHINI NI MKATABA WA KAZI, MAJIBU HALISI YA MOI, MOJA YA RUFAA YA BUZWAGI KUMPELEKA MOI, PIA NA MAJIBU YA OSHA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole
 
Ume

umesema yesu sio maraika ni nanituambie sasa tujue jua tuuh maraika ni son of god
Malaika ni son of God? Mstari gani umeandika hivyo mkuu? Nachojua Yesu ana coexist na Mungu Baba (John 1:1-5) ndio maana bible inamuita First born of all creation (Col 1:15) kwahiyo mpaka hapo sio level moja na malaika ambao wamewekwa level moja na binadamu (Ufu 22:9) kwahiyo haiwezekani wawe na character sawa kati ya Boss na kijakazi!!

Tukisema son of God kwa context ya malaika au binadamu haimaanishi ni lateral sons of God ila tu sababu ni wafuasi wake (Yoh 1:12) nothing more or less.
 
Huu uzi kuna maswali nitakuja kuuliza but naomba niache swali hili,
๐ˆ๐ง๐š๐ฌ๐ž๐ฆ๐ž๐ค๐š๐ง๐š ๐ค๐ฐ๐ž๐ง๐ฒ๐ž ๐ ๐š๐ซ๐ข๐ค๐š ๐ฒ๐š ๐๐ฎ๐ก๐ฎ ๐ค๐ฎ๐ง๐š ๐ฆ๐ญ๐ฎ ๐ฆ๐ฆ๐จ๐ฃ๐š ๐š๐ฆ๐›๐š๐ฒ๐ž ๐š๐ฅ๐ข๐ฌ๐š๐ฅ๐ข๐š ๐ฒ๐ž๐ฒ๐ž ๐š๐ค๐ฎ๐ฐ๐š ๐ฉ๐š๐ซ๐ญ ๐จ๐Ÿ ๐Ÿ๐š๐ฆ๐ข๐ฅ๐ฅ ๐ฒ๐š ๐๐ฎ๐ก๐ฎ ๐ฐ๐š๐ฅ๐š ๐ก๐š๐ค๐ฎ๐ข๐ง๐ ๐ข๐š ๐ค๐ฐ๐ž๐ง๐ฒ๐ž ๐ฌ๐š๐Ÿ๐ข๐ง๐š ๐ข๐ฅ๐š ๐š๐ฅ๐ข๐ฉ๐š๐ง๐๐š ๐ฆ๐ข๐ฅ๐ข๐ฆ๐š ๐ฆ๐ข๐ซ๐ž๐Ÿ๐ฎ ๐ง๐๐จ ๐š๐ค๐š๐ฉ๐จ๐ง๐š ๐ฃ๐ž ๐ก๐ข๐ข ๐ข๐ง๐š๐ฎ๐ค๐ฐ๐ž๐ฅ๐ข ๐ ๐š๐ง๐ข ๐š๐ฎ ๐ง๐ข ๐ฌ๐ญ๐จ๐ซ๐ฒ ๐ณ๐š ๐ฏ๐ข๐ฃ๐ข๐ฐ๐ž๐ง๐ข
 
Huu uzi kuna maswali nitakuja kuuliza but naomba niache swali hili,
๐ˆ๐ง๐š๐ฌ๐ž๐ฆ๐ž๐ค๐š๐ง๐š ๐ค๐ฐ๐ž๐ง๐ฒ๐ž ๐ ๐š๐ซ๐ข๐ค๐š ๐ฒ๐š ๐๐ฎ๐ก๐ฎ ๐ค๐ฎ๐ง๐š ๐ฆ๐ญ๐ฎ ๐ฆ๐ฆ๐จ๐ฃ๐š ๐š๐ฆ๐›๐š๐ฒ๐ž ๐š๐ฅ๐ข๐ฌ๐š๐ฅ๐ข๐š ๐ฒ๐ž๐ฒ๐ž ๐š๐ค๐ฎ๐ฐ๐š ๐ฉ๐š๐ซ๐ญ ๐จ๐Ÿ ๐Ÿ๐š๐ฆ๐ข๐ฅ๐ฅ ๐ฒ๐š ๐๐ฎ๐ก๐ฎ ๐ฐ๐š๐ฅ๐š ๐ก๐š๐ค๐ฎ๐ข๐ง๐ ๐ข๐š ๐ค๐ฐ๐ž๐ง๐ฒ๐ž ๐ฌ๐š๐Ÿ๐ข๐ง๐š ๐ข๐ฅ๐š ๐š๐ฅ๐ข๐ฉ๐š๐ง๐๐š ๐ฆ๐ข๐ฅ๐ข๐ฆ๐š ๐ฆ๐ข๐ซ๐ž๐Ÿ๐ฎ ๐ง๐๐จ ๐š๐ค๐š๐ฉ๐จ๐ง๐š ๐ฃ๐ž ๐ก๐ข๐ข ๐ข๐ง๐š๐ฎ๐ค๐ฐ๐ž๐ฅ๐ข ๐ ๐š๐ง๐ข ๐š๐ฎ ๐ง๐ข ๐ฌ๐ญ๐จ๐ซ๐ฒ ๐ณ๐š ๐ฏ๐ข๐ฃ๐ข๐ฐ๐ž๐ง๐ข
Hizo ni story za vijiwen maana kwanza ulza mvua ilnyesha kwa siku ngap!? Hapo utapata jbu kuwa ni story za vijwen
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom