DID GIANTS EXIST? Historia ya Majitu ya Kale

Biblia inaeleza hivyo kiongozi kuwa kuna malaika waasai 200 ambao baada ya kutupwa mbinguni waliwatamani binadamu na wakafanya nao mapenzi na hapo ndipo ulipotokea mfano wa hayo manefili
Ulikuwa mpango wa Mungu iwe hivyo? au ilitokea tuu kwa bahati mbaya ikawa hivyo
 
kama malaika waliwatamani binadamu wakawaingilia nakuzaa nao, je iyo michezo wameacha? na kama wanaendelea kuwaingilia dada zetu mbona hawazai ayo majitu.
Swali zuri sana...! Ngoja waje kukujibu tujue Inakuaje hapo, maana malaika bado wapo na wanadamu pia bado wapo.

NB:
Binafsi nachukulia ni hadithi tu za uongo njoo utamu kolea...!
 
Mkuu maraika ni roho, wanauwezo wa kuvaa mwili wa mwanadam. Wwkishavaa basi wanaweza fanya yote sisi tunayofanya. Mfano mzuri ni YESU!
Malaika ndio waliomvaa Yesu au Yesu mwenyewe ndio malaika? Ufafanuzi Kama hutojali.
 
kama malaika waliwatamani binadamu wakawaingilia nakuzaa nao, je iyo michezo wameacha? na kama wanaendelea kuwaingilia dada zetu mbona hawazai ayo majitu.
Swali zuri sana...! Ngoja waje kukujibu tujue Inakuaje hapo, maana malaika bado wapo na wanadamu pia bado wapo.

NB:
Binafsi nachukulia ni hadithi tu za uongo njoo utamu kolea...!
Mkuu hawa malaika kuendana na kitabu cha Henoko walitumwa duniani kuwa waangalizi wetu na ndio walitufundisha kutengeneza silaha,nyenzo za usafirishaji,usomaji nyota, uwindaji,ujenzi na elimu zingine kibao hivyo hawa malaika baada ya kuiingiliana na jamii ya wanadamu waliwapenda ndio wakataka kulala nao nahisi hii ni sababu ya kwamba waliletwa kuishi duniani na sisi kama ambavyo Yesu alikuja kuishi so walikuwa na element za ubinadamu kma Yesu alivyokuwa akisikia njaa kiu uchovu n.k ndio maana hta tamaa za ngono ziliwavaa

Hoja ya kusema mbona sasa hawawezi kuzaa.... Biblia ilishatoa hukumu kwa malaika hawa embu tusome

Yuda 1
6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele
.

Hivyo kujibu swali lako ni kwamba hawa malaika walishafungwa kuzimu huenda hata uwezo wa kuzaa wamefungwa n.k so hawawezi tena

Kwa uelewa wangu ndio naishia hapa ila labda wataalam wa elimu ya majini wanaweza kutusaidia

Cc Mshana Jr
 
Mkuu heshima kwako....

Nafurahi kukuona tena hapa kwa mara nyingine.Tumshukuru Mungu kwa pamoja mkuu na tuendelee kumuomba uzima zaidi na zaidi....

Nina machache ninayotaka kuongezea kwenye maelezo yako...

Hapo juu umeonesha hoja au swali tata kwamba historia inatuthibitishia kuwa hawa majitu walikuwepo lakini haisemi asili yao.Hoja hii ni nzito kweli kweli na huwezi kuamini naandika hapa nikiwa nasikia baridi kutokana na uzito wake.Nasikia baridi kwasababu inanisisimua na inaogopesha na kufurahisha kwa wakati mmoja....

Kuna mambo mengi sana hayapo sawa hasa haya ambayo mimi na wewe tunayaelewa.Sijajuwa kwa hakika ni kwanini hayako sawa ila nina asilimia kadhaa za uhakika kutokana na "dhana"kuwa kuna waliosababisha haya kwasababu mbali mbali....

Historia ikiwa ni moja ya haya "mambo" yasiyo sawa ndio sababu kuu ni kwanini haisemi asili ya hawa majitu ya enzi hizo.Lakini kingine cha kujiuliza ni kwamba,ni kwasababu ipi "wakubwa" wa dunia hawakiri hadharani kuwa kulikuwa na hawa majitu? Nasema hivi kwasababu sijapata kuona mahali wanakiri uwepo wake hadharani.Kama kuna mahali wamekiri basi itakuwa siyo mbaya ukanionesha mkuu...

Katika "pita pita" zangu naweza kusema kwamba zinaweza kuelezea kiduchu sana sababu ya historia kutosema asili ya hawa majitu...

Kwanza suala la wakubwa wa dunia kutokiri hadharani kuwa hapa duniani waliwahi kuwepo majitu linahusiana [kwa mtazamo wangu] moja kwa moja na historia kutosema asili yao.Ninavyoona wakubwa hawa watakapokiri hadharani kuwa majitu walikuwepo moja kwa moja swali litakalofuata ni asili yao na hili ndilo ambalo ni gumu zaidi na nina sababu za kuliona hivi hili...

Kutokana na "maendeleo" ya kiteknologia yaliyopo leo siyo kweli tumeshindwa kufahamu asili yao bali hawataki/hatutaki kusema asili yao kama vile ambavyo hawataki/hatutaki kukiri kuwa waliwahi kuwepo hawa majitu...

Ni ukweli [kwa mujibu wa pita pita zangu] kuwa duniani paliwahi kutembelewa na na viumbe ambao hawakuwa binadamu.Viumbe hawa inadaiwa walikuwepo hapa kabla ya binadam KUWEPO duniani na ujio wa binadamu hapa duniani ulionekana kama kikwazo kwao,naomba hapa nisiende ndani zaidi maana nitakuwa napotelea machakani kwenye ninachotaka kukisema...

Ushahidi wa kutembelewa kwa viumbe hawa nao ni tatizo kama vile ilivyo kuwa tatizo kuelezea asili ya majitu na kwa maana ile ile tunajikuta tunazunguka pale pale.Kwa nukta hii pia naomba nisijikite zaidi hapa maana tutaleta mada nyingine zaidi na ngumu zaidi...

Viumbe hawa ndiyo chanzo kikubwa sana cha tech tunayoiona leo [mtafute Phill Schneider utanielewa kidoogo kwenye hili].Viumbe hawa wameelezwa kwa namna tofauti tofauti kabisa katika masimulizi mbali mbali. Viumbe hawa ndio sababu ya jambo hili tunalolisema leo hii hapa,Majitu.....

Zipo nadharia mbali mbali za kuelezea jambo hili na nadharia ya Alien ni mojawapo na ndiyo sababu nadharia hiyo inapingwa vikali na hao hao wakubwa wa dunia.Uhusika wa viumbe hawa kwenye maarifa ya binadamu imepelekea usiri mkubwa kutokana na kile wanachokihitaji viumbe hao...

Kile wanachokihitaji ndicho kinafanya swali lako lisijibike leo au kesho maana likijibika ukweli utajulikana na kufanya "mission" yao kushindikanika....

Inategemea umesoma nini ili kujuwa wanachokihitaji viumbe hawa lakini niseme tu kuwa kinachofanya swali lako kushindikana ni MAHITAJI ya hawa viumbe kwetu na ikijulikana tu inakuwa tatizo na ndio maana wanaficha kweli kweli na kwa nguvu zote isijulikane...

Kule kisiwani Sardinia,kwa mfano,mafuvu na mifupa yote ya majitu iliyokuwa inafukuliwa na wenyeji wa maeneo yale ilizuiwa na serikali na baadaye kupelekwa Vatican na haikueleweka imeenda wapi baada ya hapo...

Kwenye milima yote ambapo iligundulika mashimo na mahandaki makubwa ambayo ndani yake kulikutwa mafuvu makubwa sana ya majitu haya,kule America ya Kusini [Latin America] milima hiyo yote ilichukuliwa na kanisa Katoliki na baadaye kujengwa kanisa juu ya milima hiyo [siyo mmoja ni mingi sana] na baadaye milango ya mahandaki hiyo kufungwa na kulindwa 24/7....

Maeneo yote ya "ajabu" au mabaki ya viumbe vya "ajabu" yamekuwa yakifungwa na serikali za nchi husika.Mkuu ni nini wanazuia kisijulikane? Kule Sardinia kuna Choppa maalum zinazurula kwenye maeneo "maalum" ambayo yanadaiwa yana mafuvu ya haya majitu...

Kuna eneo moja kuna maziko ya hawa majitu na kuna ngazi za kuingia kwenye jengo kubwa sana la ardhini ambalo ndilo lilitumika kuwazikia hawa majitu.Mzee mmoja anasema kuwa huwa wanashuka huko chini kwenda kufanya ibada zao na wanaamini mafuvu ya majitu hayo yatakuja kurudiwa na uhai tena.Mzee huyu anasema kwamba majitu yae yamezikwa kwa kusimama.....

Jengo hili ambao kwa juu hwezi kulifahamu lina eneo kubwa sana kwa chini na linalindwa hatari na huruhusiwi kuingia huko labda uwe mwenyeji na unafuailiwa unachoenda kufanya kule. Wanaruhusiwa wenyeji tu kuingia humo kwasababu wanakwenda kufanya ibada zao za kijadi hivyo hawawezi kuwa threat sana....

Kama mambo yapo hivi na zaidi ya hivi,unatarajia jibu la swali lako litapatikana kweli?

Viumbe waliosababisha mabadiliko haya ya kizazi ni viumbe gani na wanataka nini?

Sitaki kujibu swali hili japokuwa kuna aina ya majibu tayari wakuu wanayajadili kwenye huu uzi na nyuzi nyingine lakini,kama ulivyosema,umakini na tahadhari ni muhimu katika kuyafuatilia haya na kuamua kipi cha kuamini...

Kwa mtu mwingine haya yanaweza kuwa kama maneno ya mlevi na yasiyokuwa na maana lakini tuwe makini kweli kweli....

Sijaweza kuwa wazi sana na inaonekana kama nimeeleza nusu nusu,nimefanya hivi kwa sababu maalum.Lakini angalau tumepata "dhana" nyingine kuwa kuna wanachohitaji viumbe ambao nao ni kazi kubwa kuwatafutia uthibitisho wa uwepo wao au kujuwa kama kweli waliwahi kuwepo. Naomba tuendelee kutafakari mkuu na ninaamini kuna tutakachopata hapa...
Safi mkuu
Shukrani kwa kuja na kushusha nondo
Nitarudi na maswali kidogo
 
Shukrani mwalimu Wangu wa JF kuhusu masuala haya ,nimekusoma uzuri kbs
 
N
sio huko tu maeneo mengi sana yapo hivyo
Na kwa hapo katikati ya singida na Dom hasa maeneo ya kutoka Bahi kuelekea manyoni kuna pahali juu ya jiwe kuna unyayo mkubwa sana na mawe kupangwa vizuri hako kaeneo Kana stor flan hivi dah basi tu ngoja niishie hapa
Daaah hebu tupe hayo maarifa mkuu usiishie hapo
 
Hata Rombo alikuwepo mnefili mmoja aliitwa Horombo huyu alikuwa shida sema wakamba wakampiga mshale wa sumu vitani, Alikuwa na urefu wa futi 12 yaan watu wawili waliojaaliwa urefu
 
kule utemin ..watoto wawil wa chief senge nadhan nao ni mbegu ya wanefili!!!!
Duh hao watoto wa Chief senge wakoje unaweza tupa mbili tatu..... Na huyo horombo alikuwa ni nani mkuu tupeni nyama kidogo tuongeze maarifa
 
Ni kweli mkuu hii hoja yako hata mafuvu ya wanyama wa zamani sio kma ya hawa wa sasa sielewi kwanni

Mfano kwenye bible Ayubu anamuongelea mnyama anaitwa BEHEMOTH ambao wengine wanadai ni dinosaur.....huyo kiumbe kwa maelezo yake anasema ndio mnyama mkubwa duniani na alikuwa na mifupa kama CHUMA na anatema cheche!!! Hao wanyama sahvi hawapo sijui wametoweka wapi.... Ipo Ayubu 40 sura nzima anamsifia mnyama huyo

Ukijuliza sana mwanadamu kuishi miaka 1000 kweli sio jambo la kitoto lazima mwili wake uwe ''umejibeba'' haswaa ili aweze kuhimili magonjwa na mabadiliko ya hali ya hewa kwa miaka yote hiyo
Lakini mkuu miaka ya zamani ilihesabiwa kama sasa tunavyohesabu?
 
Hapana walihesabu tofauti ila kuna matukio yanathibitisha hilo ingawa yalitokea zamani hivyo hakuna uthibitisho wa kisayansi mfano uwepo wa Nimrod wakati wa kujenga mnara kabla hata Abraham hajazaliwa hadi kuongelewa kwa Nimrod kwenye nyaraka mbalimbali kama mfalme aliyepambana na Abraham akiwa na miaka 50..... Ikimaanisha Nimrod alikuwepo miaka 100 kabla ya Abraham hivyo kufanya kuwa na miaka zaidi ya 150+ wakati anakutana na Abraham. Hizi ni maelezo tu kwenye nyaraka zilizookotwa huko sumeria au zile za dead sea scrolls ambazo pia zimekuwa referenced kwenye vitabu vya dini

Kwa hiyo upo sahihi miaka haikuwa sawa na yetu maana kila jamii ilikuwa ina namna yake ya kutafsiri wakati ila misri ilikuwa inahesabu misimu yote minne na nchi za karibu hivyo kama inaongezwa ni michache tu ama nusu ya uhalisia ila inakaribiana na ya sasa

Hivyo tukiachana na kalenda ila tukaangalia matukio (kama yana ushahidi lakini) tutagundua kuna watu waliishi miaka zaidi ya 500+ kutokana na matukio na pia uvumbuzi wa mifupa ya majitu marefu kuanzia huko texas miaka ya 60 mpaka baalbek miaka ya 90 inaonyesha kuna uwezekano majitu haya yaliweza kuishi kwa miaka mingi Kutokana na uwezo wa miili yao kupambana na mazingira
 
Habari za asbuhi wana jukwaa, niende moja kwa moja kwenye mada kama kichwa cha habari kinavyosema je Giants/Majitu makubwa yanayoelezwa kufika hadi futi 45 waliwahi kuishi hapa duniani?? na kama waliwahi kuishi walitoweka wapi?? Na kwanini siku hizi hawazaliwi tena??

Hadithi za uwepo wa hawa watu zipo karibu katika kila kabila na jamii hapa duniani kwa mfano wahispania wana historia ya Giant (basajaun) ubelgiji alikuwepo antigoon, indonesia (Buto), waebrania (Goliath), Irimu wa wakikuyu na Yalmavuz wa uturuki nikitaja kwa uchache.

Hata vitabu vya kidini na kihistoria zimewaongelea hawa watu embu tuone mifano kidogo

WANEFILI
Mwanzao 6:4
4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa

Kwa tafsiri ya kiingereza

Genesis 6:4
4There were giants in the earth in those days; and also after that, when the sons of God came in unto the daughters of men, and they bare children to them, the same became mighty men which were of old, men of renown.

Inaelezwa watu hawa walikuwa ni majitu makubwa yenye nguvu yanaongelewa pia kwenye vitabu vya kihistoria kma Book of giants tunaona watoto wa Semyaza kina ohyah na hahyah walikuwa ni majitu makubwa sana yanazidi futi 100!!!..... Pia kitabu cha Enoko (book of watchers) anaongelea watu hawa ambao walikuwa ni wakubwa sana na walikuwa wakitesa wanadamu maana walidai vyakula kuliko viwango vyao vya uzalishaji na wakaanza hadi kuwala wanadamu wenyewe.... So dunia ilijaa vurugu tupu kipindi cha kabla ya gharika sababu ya hawa WANEFILI

2. WANA WA ANAKI (ANNUNAKI)
Kwenye vitabu vya dini hawa pia wanaongelewa kama WANEFILI ambao ni majitu marefu yenye nguvu sana

Hesabu 13:33
32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.
33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.

Walisema haya baada ya waisraeli kutuma wapelelezi kwenda kukagua nchi ya kanaan iliyokaliwa na wana wa Canaan mtoto wa Ham wakiwemo Waamori,waamaleki,wayebusi,wahiti,Hivitites,Gilgashites n.k ambao kwenye biblia wanaelezwa kma majitu makubwa na marefu yaliyoishi Canaan kipindi waisraeli wanataka kurudi kwenye nchi yao ya ahadi

Amos 2:9
9 Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini

NB:Mierezi ni miti mirefu sana sasa iliopatikana huko lebanon

QURAN TAKATIFU
Mfano ambao upo ndani ya Quran ni Mfalme Og wa Bashan au kwa kiarabu alifahamika kma Uj ibn Anaq huyu alikuwa mfalme wa kale ambaye alikuwa ni mrefu sana na ana mwili mkubwa tunaambiwa alikuwa na futi 13 na alikuwa na nguvu sana,pia kwenye Quran anatajwa Jitu linaitwa Jalut ambalo nalo linaelezwa alikuwa mtu mkubwa mwenye maguvu sana kuliko umbo la kawaida la mwanadamu.

GILGAMESH
Huyu ametajwa na Enocko kwenye book of giants kwamba alikuwa ni JITU kubwa sana lenye manguvu kiasi kwamba lilitangaza vita na Mbingu..... Inadaiwa alitawala ufalme wa sumeria (Uruk) enzi za kale na alitawala kwa miaka 126... Ana stori ndefu kidogo itabidi afunguliwe uzi siku moja (Epic of gilgamesh) ila kwa leo nimemtaja tu kma mmoja ya GIANTS

USHAHIDI WA KISAYANSI
Hii ni baadhi ya mifano tu ili twende pamoja... Na baadhi ya tafiti zimefanyika wamepata ushahidi wa miji walioishi hawa wanefili ambayo majengo yao tofali moja tu haliwezi bebwa na kifaa chochote cha sasa hivyo wameconclude ulijengwa na MAJITU haya ndio pekee yana uwezo wa kubeba tofali kma zile miji hii mfano ya maeneo hayo ni magharibi wa mto yordani, Pia Hebron, mesopotamia na maeneo ya mashariki ya kati. Kwa maeneo zaidi angalia kiambatanisho cha video hapo chini kuhusu majengo hayo afu uniambie kma mwanadamu wa kawaida angeweza kujenga kulingana na technologia ya kipindi kile!

Pia ushahidi mwingine ulipatikana na mtafiti Georges Vacher de Lapouge na mifupa akiita Giant of castelnau... Mifupa hiyo kwa picha inaonekana ni ya kibidanadam ila ni mikubwa kuliko ya mwanadamu wa kawaida maana estimation ilifika futi 12 hivi ya urefu kwa kutumia mifupa hiyo ya miguu

WALIISHIA WAPI HAWA MAJITU??
1.Kwenye vitabu vya kihistoria na dini wanadai kwamba wanefili walikufa kwenye gharika la Nuhu ila cha kujiuliza kma kweli walikufa kwenye gharika walirudije baadae mfano hao waamori au wayebusi walikuwa ni wanefili (wajuzi mtusaidie hapa)

2. Kuendana na kitabu cha Joshua tunasoma kwamba alidhamiria awaangamize wote ili waweze kuiteka Canaan na kuiweka mikononi mwao..... Ila tunaona HAKUUA wote sababu wengine walikimbia hivyo waliachwa wakaishi miji ya kusini (Gaza ya sasa)

Maswali ya kujiuliza

Je asili yao ni nini mpaka wakawa wakubwa hivyo??

Je uzao wao uliishia wapi??

Je watu hao walikuwepo kweli??

Je kwanini siku hizi hawazaliwi tena??

Ahsanteni kwa kusoma,karibuni kwa michango View attachment 748594 View attachment 748595 View attachment 748596 View attachment 748597

CC wanajukwaa wote bila kuwasahau
Malcom Lumumba, hearly Da'Vinci ,Te Lavista,Kiranga Elungata ,nyabhingi ,Mchawi Mkuu,Eiyer ,Mshana Jr n.k
Mkuu heshima yako.
Hii mada ya manafeli na asili yao nimejaribu kuwaza na kuwazua nilichogundua ni kwamba watu tunashindwa kuipa point moja katika maandiko uzito unao stahili. Point hiyo ni hii hapa;
.
Mwanzo 3
14 Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;
.
Hii hapa ni laana ya Mungu kwa nyoka baada ya kumdanganya Eva. Laana hii inambadilisha maumbile yake ya asili. Nyoka hakuwa na umbile hili alilo nalo sasa alikuwa ni kiumbe wa umbile la kitanashati (smart) kwa lugha ya sasa.
Sasa watu wanajichanganya kwa kufikiri shetani alimwingilia Eva kingono. Hapana! Shetani ni roho na roho haiwezi kuwa na uzao wa mwili wa damu na nyama kwa mwanadamu. Kilichofanyika ni shetani (roho), kumtumia mnyama nyoka kumwingilia Eva na hivyo kujipatia uzao kwake yaani kaini. Hivyo basi kaini alikuwa ni NAFELI na watoto wake ni manafeli.
Wana wa Mungu yaani malaika watu sii malaika roho, walijitwalia wake kutoka kwa manafeli na matokeo ya muungano huu yalileta kizazi cha MAJITU.
Majitu sio manafeli bali ni chotara la manafeli kwa wana wa Adam- Seth.
Majitu yalipoangamizwa kipindi cha gharika ya Nuhu, tunashangaa ni kwa nini tena yanakuja kupatikana ng'ambo ya pili baada ya ghariki.
Ukiyachunguza maandako vizuri utagundua kwamba wana wa Nuhu kama sii wote watatu waliingia safinani na wake waliotokana na jamii ya mijitu. Hivyo kukawa na uwezekano wa germ cell za majitu kuendelea kuwepo.
Huu ndio ufahamu wangu kwa uchache kuhusu asili ya Nafeli then Gitu.
 
Mkuu umefafanua vizuri sana kwa kweli!! Hii ndio reasoning ya vintage JF, ubarikiwe sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom