zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,037
- 28,685
Habari za asbuhi wana jukwaa, niende moja kwa moja kwenye mada kama kichwa cha habari kinavyosema je Giants/Majitu makubwa yanayoelezwa kufika hadi futi 45 waliwahi kuishi hapa duniani?? na kama waliwahi kuishi walitoweka wapi?? Na kwanini siku hizi hawazaliwi tena??
Hadithi za uwepo wa hawa watu zipo karibu katika kila kabila na jamii hapa duniani kwa mfano wahispania wana historia ya Giant (basajaun) ubelgiji alikuwepo antigoon, indonesia (Buto), waebrania (Goliath), Irimu wa wakikuyu na Yalmavuz wa uturuki nikitaja kwa uchache.
Hata vitabu vya kidini na kihistoria zimewaongelea hawa watu embu tuone mifano kidogo
WANEFILI
Mwanzao 6:4
4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa
Kwa tafsiri ya kiingereza
Genesis 6:4
4There were giants in the earth in those days; and also after that, when the sons of God came in unto the daughters of men, and they bare children to them, the same became mighty men which were of old, men of renown.
Inaelezwa watu hawa walikuwa ni majitu makubwa yenye nguvu yanaongelewa pia kwenye vitabu vya kihistoria kma Book of giants tunaona watoto wa Semyaza kina ohyah na hahyah walikuwa ni majitu makubwa sana yanazidi futi 100!!!..... Pia kitabu cha Enoko (book of watchers) anaongelea watu hawa ambao walikuwa ni wakubwa sana na walikuwa wakitesa wanadamu maana walidai vyakula kuliko viwango vyao vya uzalishaji na wakaanza hadi kuwala wanadamu wenyewe.... So dunia ilijaa vurugu tupu kipindi cha kabla ya gharika sababu ya hawa WANEFILI
2. WANA WA ANAKI (ANNUNAKI)
Kwenye vitabu vya dini hawa pia wanaongelewa kama WANEFILI ambao ni majitu marefu yenye nguvu sana
Hesabu 13:33
32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.
33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.
Walisema haya baada ya waisraeli kutuma wapelelezi kwenda kukagua nchi ya kanaan iliyokaliwa na wana wa Canaan mtoto wa Ham wakiwemo Waamori,waamaleki,wayebusi,wahiti,Hivitites,Gilgashites n.k ambao kwenye biblia wanaelezwa kma majitu makubwa na marefu yaliyoishi Canaan kipindi waisraeli wanataka kurudi kwenye nchi yao ya ahadi
Amos 2:9
9 Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini
NB:Mierezi ni miti mirefu sana sasa iliopatikana huko lebanon
QURAN TAKATIFU
Mfano ambao upo ndani ya Quran ni Mfalme Og wa Bashan au kwa kiarabu alifahamika kma Uj ibn Anaq huyu alikuwa mfalme wa kale ambaye alikuwa ni mrefu sana na ana mwili mkubwa tunaambiwa alikuwa na futi 13 na alikuwa na nguvu sana,pia kwenye Quran anatajwa Jitu linaitwa Jalut ambalo nalo linaelezwa alikuwa mtu mkubwa mwenye maguvu sana kuliko umbo la kawaida la mwanadamu.
GILGAMESH
Huyu ametajwa na Enocko kwenye book of giants kwamba alikuwa ni JITU kubwa sana lenye manguvu kiasi kwamba lilitangaza vita na Mbingu..... Inadaiwa alitawala ufalme wa sumeria (Uruk) enzi za kale na alitawala kwa miaka 126... Ana stori ndefu kidogo itabidi afunguliwe uzi siku moja (Epic of gilgamesh) ila kwa leo nimemtaja tu kma mmoja ya GIANTS
USHAHIDI WA KISAYANSI
Hii ni baadhi ya mifano tu ili twende pamoja... Na baadhi ya tafiti zimefanyika wamepata ushahidi wa miji walioishi hawa wanefili ambayo majengo yao tofali moja tu haliwezi bebwa na kifaa chochote cha sasa hivyo wameconclude ulijengwa na MAJITU haya ndio pekee yana uwezo wa kubeba tofali kma zile miji hii mfano ya maeneo hayo ni magharibi wa mto yordani, Pia Hebron, mesopotamia na maeneo ya mashariki ya kati. Kwa maeneo zaidi angalia kiambatanisho cha video hapo chini kuhusu majengo hayo afu uniambie kma mwanadamu wa kawaida angeweza kujenga kulingana na technologia ya kipindi kile!
Pia ushahidi mwingine ulipatikana na mtafiti Georges Vacher de Lapouge na mifupa akiita Giant of castelnau... Mifupa hiyo kwa picha inaonekana ni ya kibidanadam ila ni mikubwa kuliko ya mwanadamu wa kawaida maana estimation ilifika futi 12 hivi ya urefu kwa kutumia mifupa hiyo ya miguu
WALIISHIA WAPI HAWA MAJITU??
1.Kwenye vitabu vya kihistoria na dini wanadai kwamba wanefili walikufa kwenye gharika la Nuhu ila cha kujiuliza kma kweli walikufa kwenye gharika walirudije baadae mfano hao waamori au wayebusi walikuwa ni wanefili (wajuzi mtusaidie hapa)
2. Kuendana na kitabu cha Joshua tunasoma kwamba alidhamiria awaangamize wote ili waweze kuiteka Canaan na kuiweka mikononi mwao..... Ila tunaona HAKUUA wote sababu wengine walikimbia hivyo waliachwa wakaishi miji ya kusini (Gaza ya sasa)
Maswali ya kujiuliza
Je asili yao ni nini mpaka wakawa wakubwa hivyo??
Je uzao wao uliishia wapi??
Je watu hao walikuwepo kweli??
Je kwanini siku hizi hawazaliwi tena??
Ahsanteni kwa kusoma,karibuni kwa michango
CC wanajukwaa wote bila kuwasahau
Malcom Lumumba, hearly Da'Vinci ,Te Lavista,Kiranga Elungata ,nyabhingi ,Mchawi Mkuu,Eiyer ,Mshana Jr n.k