Dickson, kwanini ulinitendea hivi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dickson, kwanini ulinitendea hivi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by vukani, Mar 28, 2010.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ni saa kumi jioni, ndio nimeamka kutoka katika usingizi wa mchana. Hapa nilipo nimesimama dirishani, nikitazama mandhari ya huko nje, kuna manyunyu kiasi na ngurumo za hapa na pale.

  Hali ya hewa imebadilika katika jiji hili la Dar na kuna hali ya kijiubaridi kwa mbali na hali ya mvua za kiasi na hivyo kupunguza hali ya joto ambalo limekuwa ni la kutisha lisilo na mfano utadhani tupo katika nchi ya Sudan au Chad, naambiwa kuwa hali ya joto imefikia kiasi cha digrii 37, hiki ni kiwango cha kutisha sana tofauti na miaka ya nyuma.

  Siku ya leo sikwenda kazini nilijihisi kuwa na homa ya malaria , nikaona ni vyema nikapate matibabu, na baada ya matibabu nikaona nijipumzishe.Kupitia dirishani, nawaona watoto wakicheza mpira, huku wakifurahia hii hali ya manyunyu. Wanacheza kwa furaha huku wakicheka, nadhani ni kutokana na hii hali ya hewa. Nikiwa bado nimewatumbulia macho, mtoto mmoja anaupiga mpira na kuingia ndani ya uzio wa nyumba yangu, kutokana na kuvutiwa na mchezo wao nikaamua kutoka na kuwarudishia mpira wao, nilitamani waendelee kucheza, kwani nilivutiwa sana na watoto wale kwa jinsi walivyokuwa wakicheza kwa furaha.

  Baada ya kuwarudishia mpira wao, walinishukuru na kunishangilia kisha wakaendelea na mchezo wao. Ilionekana walifurahishwa na kitendo changu hicho.

  Dickson, nimeamua kuchukua karatasi na kalamu ili kukusimulia haya kutokana na uchungu nilio nao, uchungu ambao kamwe sijui kama nitakuja kuusahau. Kidondo ulichoniachia bado hakijapona na kila uchao maumivu yako pale pale. Kwa kifupi sijapata tiba na sijajua ni lini kidonda hiki kitapona.

  DK, kama nilivyozoea kukuita wakati ule wa kilele cha mapenzi yetu, naomba nikuite kwa jina hili katika waraka huu, naamini haitakuwa ni tatizo kwako. Ni mwaka wa kumi sasa tangu uliponiacha na kuoa mwanamke mwingine eti kwa sababu sikubahatika kukuzalia mtoto. Pamoja na kunieleza kuwa ilitokana na shinikizo la wazazi wako, lakini naamini wewe ndiye uliyekuwa na uamuzi wa mwisho wa kuamua hatima ya mapenzi yetu.

  Kuwasingizia wazazi na ndugu zako naamini haikuwa ni sababu stahili ya kukwepa lawama. DK, naomba ukumbuke kiapo chetu, uliniambia kuwa mimi na wewe mpaka kufa, lakini mbona bado tuko hai, lakini umeniacha, DK, kwa nini lakini?

  Kumbuka kwamba matatizo niliyokuwa nayo, wewe ndiye chanzo chake, na ni wewe uliyenishawishi hadi kufikia uamuzi ambao ndio uliosababisha mie kutopata mtoto.

  Ilikuwa ni mwaka 1990, tulikuwa ndio tumengia kidato cha sita, na tulikuwa katika kilele cha mapenzi yetu. Ni katika kipindi hicho ndipo nilipojihisi kuwa mjamzito. Nilipokueleza ulishtuka sana, na ulinieleza kuwa hutarajii kuitwa baba kabla ya kumaliza masomo, ulinishawishi tuutoe ujauzito ule ili kuninusuru niendelee na masomo, ulidai kuwa isingekuwa vyema nisimamishwe shule kwa kuwa mjamzito halafu wewe uendelee kusoma peke yako. Tulikuwa tumejiwekea malengo, kuwa tuhakikishe tunasoma mpaka chuo kikuu, hukutaka tutibue malengo yetu.

  Nilikupinga kwa maelezo kuwa hata nikisimama shule bado nitakuwa na nafasi ya kudurusu kidato cha sita baada ya kujifungua na nikakuhakikishia kuwa hata kama ukinitangulia sio vibaya, nitahakikisha namaliza chuo kikuu na kutimiza ndoto zetu. Ulinipinga sana, na baada ya kuvutana kwa muda mrefu huku miezi ikiendelea kuyoyoma hatimaye niliamua kukubaliana nawe, na tukiwa pamoja tulikwenda kuutoa ujauzito ule uliokwisha fikisha miezi minne.

  Haikuwa kazi rahisi, kwani daktari aliyefanikisha operesheni ile hakuifanya kwa ufanisi kwani hata baada ya kurudi nyumbani hali yangu haikuwa nzuri, niliendelea kusumbuliwa na tumbo. Tuliporudi hospitali nilisafishwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

  Tulirejea shuleni na kuendelea na masomo hadi tukamaliza kidato cha sita. Kwa bahati nzuri wote tulichaguliwa kujiunga na chuo kikuu mlimani, wewe ukisomea fani ya uhasibu na mimi nikisomea fani ya sosholojia.

  Tulifanikiwa kumaliza pamoja na kufaulu, tulifanya sherehe ya pamoja na kuingia katika ajira pamoja, mimi nikiajiriwa serikalini na wewe ukiajiriwa katika mojawapo ya mashirika ya Umoja wa Mataifa {UN}.

  Baada ya miaka miwili tangu kuingia katika ajira, tuliamua kufunga ndoa ambayo ilikuwa na mbwembwe nyingi. Maisha yetu ya ndoa yalikuwa ni ya upendo na amani. Sio kwamba tulikuwa hatugombani, la hasha, tulikuwa tunagombana lakini hiyo ilikuwa ni njia mojawapo ya kustawisha mapenzi yetu, kwani kupitia kugombana kwetu, tulipata fursa ya kila mmoja kufahamu hisia za mwenzie.

  Mwaka mmoja tangu tufunge ndoa tuliamua kuzaa mtoto, na baada ya majaribio kadhaa kushindikana tuliamua kwenda kwa watalamu wa tiba ili kupata ushauri. Ni katika kipindi hicho ndipo tulipopata taarifa ambazo zilinipenya moyoni kama msumari wa moto. Tuliambiwa kuwa siwezi kupata mtoto milele kwa kuwa mirija yangu ya uzazi imeathirika baada ya kile kitendo cha kutoa mimba tulichokifanya wakati ule.

  Hatukata tamaa, tuliwatembelea wataalamu kadhaa wa tiba wakiwemo wa tiba za asili lakini hatukufanikiwa kupata mtoto. Miaka minne baadae tangu tuoane ndugu zako walianza manung'uniko ya chinichini, lakini hata hivyo walifikia hatua ya kunieleza waziwazi kuwa mimi ni mgumba siwezi kukuzalia mtoto, maneno hayo yalinichoma rohoni, lakini nashukuru ulikuwa pamoja nami na uliniahidi kunilinda. Hukuishia hapo ulifikia hatua ya kula kiapo kuwa mimi na wewe mpaka kufa.

  Nilifarijika na msimamo wako, na ulinipa nguvu kila wakati. Mwaka mmoja baada ya kiapo chako ulianza kubadilika, ulikuwa ukichelewa kurudi nyumbani na nikikuuliza majibu yako yalikuwa ni ya mkato. Chakula ulikuwa huli nyumbani na kama hiyo haitosh ulifikia hatua ya kunipiga kwa sababu ya kukumbusha kule tulipotoka. Mateso yalizidi sana na ndugu zako walikuja kunieleza wazi kuwa unarajia kuoa hivyo nijiandae kuwa na mke mwenza, kwa kuwa huyo mchumba wako ameshakuzalia mtoto wa kiume.

  DK, umesahau kuwa hata mie kama nisingetoa ule ujauzito ningekuwa na mtoto wa kiume kama alivyotueleza yule daktari, na uamuzi wa kutoa ule ujauzito haukuwa ni wangu bali ilitokana na shinikizo lako.

  Nilipokuuliza kuhusu wanavyosema ndugu zako, ulinijibu kwa mkato kuwa ni kweli na ulidai kuwa haikuwa na ubaya wowote kwa kuwa amekuzalia mtoto, kitu ambacho mimi nimeshindwa.

  Nililia kwa uchungu sana na niliamua kuondoka, sikutaka kuishi na mke mwenza kwa kuwa hiyo ni kinyume na mafundisho ya dini yetu ya kikristo. Nilifanya juhudi za kutafuta suluhu kupitia kwa mchungaji wetu lakini haikuzaa matunda na hatimaye tukatengana, na wewe kumuoa huyo binti aliyekuzalia mtoto.

  Sikukata tamaa, niliamini tu kuwa iko siku nitakuja kupata mtoto siku moja. Mwaka jana niliamua kwenda nchini Afrika ya Kusini, hiyo ni baada ya kushauriwa na baadhi ya madaktari bingwa, na nilipofika kule nilipatiwa matibabu na kupandikizwa ujauzito. Hivi ninavyokuandikia waraka huu ninao ujauzito wa miezi saba, na ninatarajia kupata mtoto wa kiume mungu akinijaalia.

  Hiyo yote ni kutaka kukuthibitishia kuwa kwa mungu kila jambo linawezekana. Nilipokuwa nikiwaangalia wale watoto waliokuwa wakicheza mpira, nilikuwa nimeshika tumbo langu na nilihisi mwanangu na yeye akirukaruka kwa furaha akifurahia kile ninachokiona kupitia kwangu. Naamini na yeye atakuwa ni mchezaji mpira mahiri, kwa kuwa mama yake pia ni mshabiki wa mpira wa miguu.

  Naomba nihitimishe waraka huu kwa kukutakia maisha marefu ili uje kushuhudia miujiza ya Mwenye enzi mungu, kwamba kwake yeye kila jambo linawezekana.

  Ni mimi mke wako wa zamani.

  XYZ.


  NB: Jina la Dickson sio la muhusika.

  Simulizi hii ni mkasa wa kweli

   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,627
  Likes Received: 5,788
  Trophy Points: 280
  Ni mimi mke wako wa zamani.

  XYZ.

  NB: Jina la Dickson sio la muhusika.

  Simulizi hii ni mkasa wa kweli

  NANI ANAITAJI NOVEL HUKU JF???MBONA UJAANDIKA AUTHOR@!!!!!KAMA NI ZA KWELI MAJINA YA UONGO YA NINI HATUTAKI UNAFIKI TAJA MAMA MIAMBILI UMEANIACHA NIMEPATA MTOTO.......USIRUDIE TENA SIKU NYINGINE...UKIJA NA VISA HVI TAJA MAJINA

  ELSE NOVEL KAPELEKE KWA WAKUBWA
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  So sad a story. Kama ni kweli, pole kwa yote na hongera kwa juhudi zako. Wakati fulani sie wanaume ni washenzi. Wakati fulani sisi ni mashujaa pia, na kinyume chake. Go on and live your life b'se life goes on
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,627
  Likes Received: 5,788
  Trophy Points: 280
  polesana dia ukubwa huo siku nyingne usikubali kutoa mimba laana hata kwenye biblia ...kizazi chaki kinaweza kuwa chote kinatoa mimba haya matatzo watu awyajui...sad mungu awe nawe nakupa wimbo wa........

  Mwombee adui wako aishi miaka mingi aone baraka za bwana yeu juu yako akiwa hai......
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Kila Mwanamume anaoa kwa sababu zake, mwinge kwa MApenzi tu, mwingine anataka watoto, mwingine anataka Heshima tu ya kuitwa MR nk, sasa kama mtu alikuwa anataka mtoto ilikuwa ni shida kuishi na huyo mama ambaye mbele ya madaktri waliambiwa kuwa HAwezi kuzaa tena

  inauma lakini ndio sehemu ya maisha
   
 6. l

  liman Member

  #6
  Mar 28, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  XYZ,kuwa muwazi mtu mbaya kama uyo unamficha wa nini
  au bdo unamuitaji????????????
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,627
  Likes Received: 5,788
  Trophy Points: 280
  mi ndipo aliponiuzii kabla ya kuja kumwonea huruma

  washenziana kama hawa si watu wewee wawafichia nini??
   
 8. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Du ita happens a lot this thing mnooo
   
 9. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Imeandikwa vizuri... thanks for sharing
   
 10. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ni jambo la kusikitisha kuona kuwa umekosa subira, hivi hakuna lugha nzuri ambayo ungeweza kuitumia kufikisha ujumbe wako mpaka kunikashifu.....
  Hii sio Novel kama ulivyotuhumu, ki kisa cha kweli ambacho kimemtokea ndugu yangu na hakupenda niweke utambulisho wake hapa, bali alitaka watu wajifunze kupitia uzoefu wake.
  Kama wewe haikusaidii basi hukulazimishwa kusoma, kuna habari nyingi sana humu ambazo ungeweza kusoma pia.
  nakutakia kila la heri katika maisha yako..............
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,627
  Likes Received: 5,788
  Trophy Points: 280
  NA WEWE VUKANI KUNIGOMBANISHA NA MTOTO WA MWENZIO MAANAKE NINI JAMANI AMA K=UKUSOMA NILICHOFWATA

  Quote: liman
  xyz,kuwa muwazi mtu mbaya kama uyo unamficha wa nini
  au bdo unamuitaji????????????

  mi ndipo aliponiuzii kabla ya kuja kumwonea huruma

  washenziana kama hawa si watu wewee wawafichia nini??
   
 12. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mama Mia r u sure you are not high today? :D
   
 13. A

  Artman Member

  #13
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana, Mungu akujalie mtoto anayekuwa tumboni awe na afya njema.
  Sasa huyo mtoto uliyepandikizwa baba yake unamjua?
   
 14. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nakala zote zimehifadhiwa ukihitaji ni PM
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,627
  Likes Received: 5,788
  Trophy Points: 280
  mpwa shemeji kaniulizia nini ni pm basi
  mwambie nilikuwa nashtua
   
 16. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hapo mlitendana, kwa sababu nawe pia ulihusika kwa kiasi kikubwa kufikia uamuzi huo wa kutoa mimba. Na kuvunjika ndoa ni jambo linalotokea tu, huwezi kujua hata kama usingekuwa mgumba ndoa yako ingeweza kuvunjika vilevile. Wangapi wamezaa na bado wameachwa? Wengi tu.

  Acha kung'ang'ania kumbukumbu za maumivu, hazitakusaidia kitu. Ukurasa huo umekwisha, ufunge, endelea na maisha yako, bado kuna mambo kibao ya kufurahia.
   
 17. M

  Mtu Kwao JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2010
  Joined: Jan 15, 2008
  Messages: 258
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni kisa cha kuhuzunisha sana,na hapa tunapewa fundisho.We Dickson popote ulipo utalaaniwa na huwezi kuwa na maisha ya furaha bila kurudi kwa huyo XYZ kumuomba msamaha ndugu.Pole sana DADA XYZ.
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,928
  Likes Received: 83,495
  Trophy Points: 280
  Duuhhhh! Imenigusa sana hii story yako. Ahsante sana kwa kuamua kushare nasi na hongera sana kwa ujauzito wako na Mungu akujalie ujifungue salama salimini~AMEN
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,928
  Likes Received: 83,495
  Trophy Points: 280
  Acha hizo! ahhhhhh! unataka ataje jina litakusaidia nini wewe? Unamjua huyo jamaa au huyu binti? Unajuaje hilo jina la DK kama si jina la kweli? Mtu kaamua kushare story yake ambayo imekuwa ikimuumiza moyoni mwake kwa miaka mingi tu halafu unamgeuzia kibao na kuanza kumsemea hovyo. Acha hizo!!!!
   
 20. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hakuna laana yoyote, watu wanaodhulumu na kuishi kwa kuwaumiza wenzao utawaona siku zote wanafanikiwa kwa sana. Mbona mafisadi hapa nchini wanawaibia maskini kabisa ambao hata chakula cha siku moja ni shida, na bado Mungu anaendelea kuwabariki na kuwaongezea tu. Hii theory inayoitwa laana, sometimes huwa haifanyi kazi.
   
Loading...