Dick Sound: Milionea aliyeanza kuuza maji, kufunga muziki Magomeni

Nimevutiwa na utajiri mkubwa huyu kijana mwenye miaka 31.

Amekuwa akiuza maji kabla ya kujiajiri kwa kazi be ya kufunga mziki magari na kuyapimpu.Kazi hii kafanya kwa miaka zaidi ya ishirini.

Ana miliki nyumba yenye thamani ya zaidi ya milioni 350 TSH, pamoja na magari ya kifahari ya thamani ya zaidi milioni 850.

Hakika kijana huyu ni kielelezo cha vijana wenye mafanikio makubwa kwa kujiajiri wenyewe bila ya kutegemea ajira ya serikalini, mafanikio ya kijana huyu ni zaidi ya wasomi walioajiriwa wakisubiri mshahara kiduchu kwa mwezi.

Hongera yake.
Mtakaosikiliza hizo videos naomba mtujuze content yake zikoje. Nimeweka hapa kwa atakayetaka..
 
Watu hawataki kukubali jamaa ashatusua "
Mleta mada hii ndio hali halisi ya watanzania,,, ukiwa nacho unapondwa usipokuwa nacho pia unapondwa ....
Watu wala hawapigi kelele kwakuwa katusua,watu wanachoongelea ni huo umri ndio kwenye shida.Inamaana hta wewe hapo kwenye age huoni kama hakupo sawa????au ndio wenzetu kila kitu kupiga makofi
 
Kwa Radi ni upande wa kushoto kama unatoka bamaga Kwa Mbele kidogo baada ya kushuka kituo cha kumekucha uelekeo kama unaenda kijiwen kushuka kituo cha kumekucha.upande wa kushoto Duka la spare..upande wa kulia garage.

Kwa magoti ni upande kushoto kama unatoka kijiwe.kituo ni kumekucha karibu kabisa na duka la nguo za watoto hapo kituoni kumekucha.
Opposite na kanisa la KKKT sinza kumekucha

Karibuni jamani muwape riziki marafiki zangu
Sawa dear..nimeshapafahamu
 
Na hawatokaa watobowe ng'oo, hapa mjini si kila ofisi unayoiona ndio source of income ya muhusika.

Hizo ofisi ni cover tu, watu wana mambo yao mengine.

Hii dunia ina siri kubwa, utashangaa siku ukimkuta mchungaji yupo kwa mganga wa kienyeji kunyoosha mambo yake, kesho kanisani anakemea wachawi na mapepo hii ndio dunia ilivyo.
Siku moja nimeenda kwa mganga mida ya asbh ... yule mganga akawa kama kachoka hivi.. nikamuuliza vipi mzee? Akadai hajalala usiku mzima alikuwa anawaganga wachungaji. Nilishangaa sana
 
Uzuri dogo ana connection na watu maarufu wote unaowajua ww tanzania hii so kufanikiwa easy tuu. Kazi kubwa ya kujivunia ni kufanikiwa kujenga connection baaas
Connection haziji tu kama ushuzi

Ni akili tu mtu wangu

Wajinga-wajinga wengi huishia kujuana na walevi tu bar
 
Siku moja nimeenda kwa mganga mida ya asbh ... yule mganga akawa kama kachoka hivi.. nikamuuliza vipi mzee? Akadai hajalala usiku mzima alikuwa anawaganga wachungaji. Nilishangaa sana
We ulienda kufanyaje?!!
 
Hizi Stori zenu tatzo mnazileta na chumvi nyingi sn.Mnaharibu mnakuja kuonekana waongo au tukikosoa tunaonekana tuna wivu

Mtu ana miaka 31 alafu ameanza kazi ya kupimpu magari zaidi ya miaka 20,yaani alianza kazi ya kupimpu magari na kufunga mziki akiwa na miaka 7 au 8?
Usisahau kamaliza darasa la saba akiwa na miaka 3,akafaulu na kuendelea na elimu ya secondary mpk form 4 akamaliza akiwa na miaka 6,then akaingia mtaani kuuza maji kwa miaka 2....kesho ntamalizia wasifu wake
 
Back
Top Bottom