Nani mkali kati ya Diblo Dibala na Dally Kimoko

kakuruvi,
Leo nimekukumbuka...Kula hii kitu...safi sana..slow rhumba

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=2f1rHvJ3mY8&feature=related[/ame]
 
Safari,

mambo mazuri haya, extra boy unaweza kuipata?

Kwa upande wangu, nina audio ya Extra Ball, almost the whole album!

Wadau,

Kwanza nianze kusema kuwa LOKETO haikuwa BENDI gorup.
Hawa jamaa walikuwa na bendi zao za kila siku na time to time wanaamua kukutana na kula good time pamoja. Ndiyo maana safu zao siku zote zilikuwa zinabadilika ingawa kuna jamaa siku zote walikuwa hapo.

Loketo ama KIUNO walipata sifa kubwa sana kwa muda mfupi kwani walikuwa ni watu wanafahamu nini wanataka na kukifanya kwa umahiri mkubwa na hamna eti MTU WA KUJAZIA. Mwanzo walianza na Diblo Dibala aliyetoka kwa Kanda Bongo Man na kuanzisha kundi lake mwenyewe baadaye. Baadaye wakawa na Dally Kimoko. Moja ya watu mashuhuri aliyekuwa kwenye kundi hili ila siku hizo hafahamiki ni Awilo Longomba.

http://www.youtube.com/watch?v=QBCCcH-QJWY
(Ukianzia 4:00 utamsikia Awilo akiimba/Rap na mbele kidogo mama anasema Dally Kimoko).

http://www.youtube.com/watch?v=UNXVIXcpbUo

(Ukianzia 3:15 utasikia wakitaja jina la Awilo Longomba ambaye siku hizo ni Mpiga drums unazosikia kwenye wimbo hapo juu).


Ki ufundi, Diblo Dibala alikuwa akipiga gitaa ki-Afrika zaidi yaani nyuzi moja moja. Dally Kimoko alianza kuweka zile sauti za gitaa kama za Rock Musics yaani ufundi wa akina Slash wa Gun N' Roses au Mzee Jimmy Hendrix. Ila wengine pia walianza baadaye kuiga kama akina Zaiko langa langa na Waafrika tuliipenda maana walikuwa wakiweka sauti tu ila upigaji unabaki ule ule.

Ni kweli kbs bro, Awilo ameshiriki sana ku-rap katika album za jamaa zake wengi sana wa Loketo. Ukisikiliza album ya Lucien Bokilo ya 'One Way' utamsikia akirap, hali kadhalika anasikika katika album ya Aurlus Mabele ya 'Embargo'. Jamaa katoka mbali (kama mpiga ngoma wa kundi la Loketo)

Bendi ya Diblo ikiitwa Matchacha

Sure, na album yake Diblo ikiitwa 'Laissez Passer'.

Hata hivyo nashangaa nyie magwiji mnamsahau kijana Kaen Madoka, ambaye ni mpiga gitaa wa Loketo baada ya Dally Kimoko na Diblo kulitosa kundi. Huyu ni jamaa aliyepiga gitaa katika album ya Loketo ya "Generation Wachiwa", ambayo ina wimbo wa 'Khadija' pamoja na album za kijana Djunny Claude ambaye pia ni mmoja wa wanakikundi wa Loketo enzi hizo.
Nina hizi audio, huwa nasuuzika sana nikizisikiliza, hata Magic Fm hawafui dafu hapa!
 
mkuuu uzeee afu usisahau enzi huja na kupita ila DIBLOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO wacha kabisa

Heshima Kakuruvi,

Kweli hawa jamaa walikuwa moto wa kuotea mbali.Diblo Dibala,Dally Kimoko na Neneh Chakuchaku walitawala vyema mpini wa solo kwa upande wa bass alikuwepo ngouma lokito na rhyzm alikuwepo Lokasa ya mbongo.

Kwenye anga za muziki hawa jamaa hawasikiki kabisa sijui kimewasibu nini.
 
mkuuu kwenye xtra ball aliyepiga solo ni DIBLO MKUUU
daly kimoko alipiga gitaa ktk albam moja ya aurlus mabele ya extra ball yaani mpaka leo kazi zao za zamani zinawika utazani zimeingia jana sokoni hazichuji ni kama ragae za bob marley hazichuji milele na kazi za hawa watu 2 ni mpya kila siku.
 
Leka huyu aliitwa Le Professoeur Vata Mombasa, jamaa alikuwa balaa, nadhani hawa kina Diblo na Dally walijifunza kutoka kwa huyu mtaalamu. Kuna mtaalamu mwingine wa kupuza saxaphone, Kiamangwana Mateta Verkys, huyo nae bora usikie tu.
 
..Siutani mazee..kwani ile mipini ya hawa jamaa mnaionaje?? Hamza Kalala, John Maida, Abel Bartazar, Joseph Mulenga, Saidi Mabela, Kasim Rashid " Kizunga",Kasim Mponda na wengineo iko juu kishenzi nadhani walikosa exposure tu kiasi kwamba hawakuvumia mbali sana!!! Big up Bujibuji..

Abel bartazar na Mulenga!!!! Walikua balaaaaaa!
Nakumbuka wimbo wa Bima lee "mzigo umeutua" ndani lilipigwa gitaa la njaaa
 

Heshima Kakuruvi,

Kweli hawa jamaa walikuwa moto wa kuotea mbali.Diblo Dibala,Dally Kimoko na Neneh Chakuchaku walitawala vyema mpini wa solo kwa upande wa bass alikuwepo ngouma lokito na rhyzm alikuwepo Lokasa ya mbongo.

Kwenye anga za muziki hawa jamaa hawasikiki kabisa sijui kimewasibu nini.

Mkuu hapo kwa Ngouma Lokito a.k.a Le Proffeser ndio patamu,jamaa anajua kucharaza Base mbaya bila kumsahau Saladin,kwenye wembo wa Soukous Stars Mama Rhoda ndio utajua uchawi wao.
 
Diblo si wa mchezo mchezo ndugu yangu.
Mpaka leo nikikaa na kusikiliza gita linavyo vuma!! acha tu.
 
wakat lingala inatisha kulikuwa na wapiga gitaa wengi sana mfano,dali kimoko,diblo,benico,allain makaba,burkina faso kasongo,nene tchaku,sheshe kalonda,wakipigia sehem mbambali wakat huo nakumbuka la nouvelle generaciones awillo longomba akipiga drums,hatarii
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom