Diaspora waguswa na kampeni ya ujenzi ofisi za walimu 402 Dar es Salaam

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Jumuiya ya watanzania wanaoishi Diaspora (Marekani) ijulikanayo kama Sixth Region Diaspora Caucus Washington kwa pamoja wameamua kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda kutatua changamoto za ofisi za walimu wa mkoa huu kwa kutoa makontena 36 ya samani mbalimbali zikiwemo viti vya kisasa zaidi ya 5000,meza za umeme 2500,meza za kawaida 2500,makabati ya vitabu makubwa 1300 na bao (writing boards) za kuandikia 700.

Mchango huu wa samani ambao una thamani ya zaidi ya dola za kimarekani $ 800,000 ambazo ni sawa na shilingi 1,800,000,000 za kitanzania utatumika katika ofisi mpya 402 za walimu zilizoanza kujengwa kupitia kampeni iliyoanzishwa na Mh Paul Makonda mapema Agosti mwaka huu.

Kupitia samani hizi adhma ya Mh Paul Makonda ya kutengeneza mazingira rafiki ya utoaji wa elimu kwa walimu wa Mkoa wa Dar es salaam itakuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na matarajio ya kupandisha kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kufikiwa kama matokeo ya miundo mbinu rafiki kwa wote.

Makontena hayo yanatarajiwa kufika nchini mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.

Mh Makonda amewashukuru wadau hawa ambao bila kuzingatia umbali waliopo na nchi yao bado wameonyesha hari ya kuguswa na changamoto za watanzania wenzao hapa nchini, na kutoa rai kwa watanzania wengine kuendelea kuunga mkono kampeni hii ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam kwa namna watakavyo weza kwani hatma ya ustawi wa maendeleo ya Tanzania ni wajibu wa kila mtanzania.

Imetolewa na kitengo cha habari na uhusiano,ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es salaam.
 
Habari hii sio ya kupendezwa kwa wavuta BANGI wa pale UFIPA watakuja na kupinga hili big up Paul Christian Magonda aka Daudi Bashite
 
Diaspora kwenye kuandika mwenye mitandao hamjambo lakini sasa kwenye utekelezaji!!!!

upload_2017-11-11_13-32-33.jpeg
upload_2017-11-11_13-32-33.jpeg
 
Hii habari ni nzuri sn, ila mheshimiwa Makonda anatakiwa aanzishe kampeni mpya baada ya hii ya kuboresha maslahi duni ya walimu. Mwl hata akikaa kwnye ofisi nzuri kiasi gani kama mshahara haufiki hata Tar 10 ya mwezi unaofatia ni kupaka rangi upepo.
 
Hivi vyote haciwezi kurudisha nyuma udhalilishaji aliowafanyia walimu /nyumbu mana naovhwwajielewi
 
Jumuiya ya watanzania wanaoishi Diaspora (Marekani) ijulikanayo kama Sixth Region Diaspora Caucus Washington kwa pamoja wameamua kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda kutatua changamoto za ofisi za walimu wa mkoa huu kwa kutoa makontena 36 ya samani mbalimbali zikiwemo viti vya kisasa zaidi ya 5000,meza za umeme 2500,meza za kawaida 2500,makabati ya vitabu makubwa 1300 na bao (writing boards) za kuandikia 700.

Mchango huu wa samani ambao una thamani ya zaidi ya dola za kimarekani $ 800,000 ambazo ni sawa na shilingi 1,800,000,000 za kitanzania utatumika katika ofisi mpya 402 za walimu zilizoanza kujengwa kupitia kampeni iliyoanzishwa na Mh Paul Makonda mapema Agosti mwaka huu.

Kupitia samani hizi adhma ya Mh Paul Makonda ya kutengeneza mazingira rafiki ya utoaji wa elimu kwa walimu wa Mkoa wa Dar es salaam itakuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na matarajio ya kupandisha kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kufikiwa kama matokeo ya miundo mbinu rafiki kwa wote.

Makontena hayo yanatarajiwa kufika nchini mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.

Mh Makonda amewashukuru wadau hawa ambao bila kuzingatia umbali waliopo na nchi yao bado wameonyesha hari ya kuguswa na changamoto za watanzania wenzao hapa nchini, na kutoa rai kwa watanzania wengine kuendelea kuunga mkono kampeni hii ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam kwa namna watakavyo weza kwani hatma ya ustawi wa maendeleo ya Tanzania ni wajibu wa kila mtanzania.

Imetolewa na kitengo cha habari na uhusiano,ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es salaam.

Dogo Makonda" huruka ya binadamu ni kuthamini utu, siyo vitu unajitahidi sana kuishawishi jamii kwa vitu ila umekosa utu. jitafakari upya usipoteze muda, kwa kazi ambayo mwishowe haitakuwa na appreciation
 
Energy drainers hamkosekani!
 
Hongera sana kwao waliofikiria juu ya hili kutokea Washington State, USA.

Makonda oyeeeeee
 
Diaspora wenyewe njaa kari hata container ya 20 ft hawana uwezo wa kuijaza acheni usanii
 
Hii haingii akilini kbsa yani eti wabongo diaspora watoe mchango jmn hta kaphoto tu katakakosimama kama identity kwa waliotuma au wawakilishi a aaaaah jmn msitufanyie hvo bhan. au ndio 900 ITAPENDEZA
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Acha udaku
Ndio mjue hata anayewapatia uongo hajui nchi anayoishi kuna states zipi... ushamba umewajaaa

Yaani ni mburura grade A
Na wewe na wenzako wote mjipige vibao mlie

Eeeeeh kapatikana kwa uongo... akili zote anadai anazo ndio zinaonyesha kuwa yeye muongo sanaaaaaa eti ktumia akili ha ha haaaaaaaa

Unajua namuongelea nani

Ha ha haaaaaaaaa
 
Lemutuz unatumia account ya kike hatare Sana hiyo
 
  • Thanks
Reactions: Gut
Hii habari km ya mtangazaji wa TBC kuhusu Rais wa marekani. Mwezako alichukuliwa hatua wawe sijui watachukua nini maana 0!!!
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom