Diana Edward; Beauty with purpose, Masai dondosha Wembe - Stop FGM

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Ukeketaji kwa wanawake husababisha maumivu makali na madhara ya kisaikolojia ambayo hudumu kwa muda mrefu.

Ukeketaji wa wanawake ni kitendo kinachohusisha kuondolewa kwa kinembe, midomo ya ndani-na-nje ya uke, na au kushona kwa pamoja pande z mbili zamashavu ya uke na kuacha tu shimo dogo kwa ajili ya kupita mkojo na damu ya hedhi. Kwa kawaida ukeketaji unafanywa kwa kutumia wembekwa wasichana wenye umri kati ya miaka nne na 12, bila dawa ya ganzi.

Kuna aina tatu za ukeketaji. Aina ya kwanza ya ukeketaji moja ni sawa na kuondoa korodani kwa mwanaume, wakati aina ya tatu ni sawa na kuondoa makende na uume kwa pamoja.

Ukeketaji unaweza kusababisha kutokwa damu nyingi, maumivu, kukosa hisia, matatizo wakati wa kujifungua, utasa, maumivu makali wakati wa ngono, maambukizi ya mara kwa mara na kuziba kwa mkojo.

Na katika baadhi ya matukio inasababisha kifo. Tofauti na tohara kwa wanaume, ukeketaji kwa wanawake pia inaondoa raha wakati wa kufanya mapenzi.

 
Mkuu Miss Zomboko
Nimeipenda Avatar Yako Yaani Mada Sijaielewa Ila Avatar Ndiyo Nimeilewa Sana Kama Mtihani Ningefaulu.
 
Kijana amejitahidi kuelimisha jamii. Hii ndio kazi alioingia nayo mlimbwende wetu kwenye Miss World. Naam amejitahidi sana. Hata kama hata shinda lakini ni bonge la skripti
 
Back
Top Bottom